Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote.. Baba wa Mbinguni,Mungu wetu na Baba yetu.. Jehova nissi..!Jehovah shalom..!Jehovha shammah..! Jehovah Roi,Jehovah Jireh..!Jehovah Rapha..! Alpha na Omega,Mungu wa Abarahamu,Isaka na Yakobo..! Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu.. Asante kwa ulinzi wako wakati wote.. Asante kwakutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii.. Si kwamba sisi ni wema sana au sisi niwazuri sana... Si kwa nguvu/utashi wetu Mungu ni kwa neema/rehema zako.. Tunakua mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Baba.. Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya.. Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua. Baba wa rehema tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea...
Siku ya ishirini na nne ya mwezi huo wa saba, watu wa Israeli walikusanyika, wakifunga na kuvaa mavazi ya magunia na kujipaka udongo kichwani kuonesha majuto yao. Wakati huo, walikuwa wamejitenga mbali na watu wa mataifa mengine, wakasimama na kuungama dhambi zao na maovu ya babu zao. Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Kuliwekwa jukwaa la Walawi; hapo walisimama Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebania, Buni, Sherebia, Bani na Kenani. Wakamwomba kwa sauti kubwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wao. Walawi, yaani: Yeshua, Kadmieli, Bani, Hashabuea, Sherebia, Hodia, Shebania na Pethahia wakawaambia watu; “Simameni na kumsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Msifuni milele na milele! Na watu walisifu jina lako tukufu, ambalo hutukuka kuliko baraka na sifa zote.”
Mungu Baba tunaomba utuepushe katika majaribu Utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote.. Nguvu za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu na za mpinga Kristo zishindwe katika Jina lililo kuu jina la Yesu.. Baba ukatamalaki na kutuatamia katika maisha yetu... Ututakase Miili yetu na Akili zetu kwa damu ya Mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetuYesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.. Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi.. Ukatufanye chombo chema Baba na tukatumike kama inavyokupendeza wewe...
Basi, wewe mwanangu, uwe na nguvu katika neema tunayopata katika kuungana na Kristo Yesu. Chukua yale mafundisho uliyonisikia nikitangaza mbele ya mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu wanaoaminika, ambao wataweza kuwafundisha wengine pia. Shiriki katika mateso kama askari mwaminifu wa Kristo Yesu. Mwanajeshi vitani hujiepusha na shughuli za maisha ya kawaida, ili aweze kumpendeza mkuu wa jeshi. Mwanariadha yeyote hawezi kushinda na kupata zawadi ya ushindi kama asipozitii sheria za michezo. Mkulima ambaye amefanya kazi ngumu anastahili kupata sehemu ya kwanza ya mavuno. Fikiria hayo ninayosema, kwani Bwana atakuwezesha uelewe kila kitu. Mkumbuke Yesu Kristo aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, aliyekuwa wa ukoo wa Daudi, kama isemavyo Habari Njema ninayoihubiri, na ambayo kwa sababu yake mimi nateseka na nimefungwa minyororo kama mhalifu. Lakini neno la Mungu haliwezi kufungwa minyororo. Kwa hiyo navumilia kila kitu kwa ajili ya wateule wa Mungu, ili wao pia wapate ukombozi upatikanao kwa njia ya Yesu Kristo, na ambao huleta utukufu wa milele. Usemi huu ni wa kweli: “Ikiwa tulikufa pamoja naye, tutaishi pia pamoja naye. Tukiendelea kuvumilia, tutatawala pia pamoja naye. Tukimkana, naye pia atatukana. Tukikosa kuwa waaminifu, yeye hubaki mwaminifu daima, maana yeye hawezi kujikana mwenyewe.”
Ukatupe neema ya kusimamia Neno lako Amri na Sheria zako.. Baba wa Mbiguni ukatubariki na kubariki yote tunayoenda kufanya/kutenda nasi tukatende kama itakavyokupendeza wewe.. Tunayaweka maisha yetu mikononi mwako.. Nyumba zetu/ndoa,watoto/familia ndugu na wote wanaotuzenguka Baba tunawaweka mikononi mwako na vyote tunavyovimiliki vilivyo ndani/nje Baba wa Mbinguni tunaviweka mikononi mwako.. Ukatulinde/kuvilinda na ukawe msimamizi na kiongozi mkuu katika yote..
Mwenyezi-Mungu asipoijenga nyumba, waijengao wanajisumbua bure. Mwenyezi-Mungu asipoulinda mji, waulindao wanakesha bure. Mnajisumbua bure kuamka mapema asubuhi na kuchelewa kwenda kupumzika jioni, mjipatie chakula kwa jasho lenu. Mungu huwaruzuku walio wake hata walalapo. Watoto ni riziki kutoka kwa Mwenyezi-Mungu; watoto ni tuzo lake kwetu sisi.
Asante Mungu Baba sifa na utukufu ni wako.. Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele.. Amina..! Asanteni sana wapendwa.. Mungu akaonekane katika maisha yenu.. Nanyi msipungukiwe katika mahitaji yenu.. Baba wa Mbinguni akawape sawasawa na mapenzi yake.. Nawapenda.
|
No comments:
Post a Comment