Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday 7 August 2017

Kikombe Cha Asubuhi;kitabu cha Hesabu..25

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah..!Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru na kumsifu daima..
Mungu wetu,Baba yetu Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwa nguvu zetu wala uelewa wetu Baba wa Mbinguni sisi kuwa hivi tulivyo ni kwa Neema/Rehema zako Mungu wetu..


Tunakuja mbele zako tukijinyeyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mfalme wa Amani..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Jehovah tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale waliotukosea..



Mfano wa mtumishi asiyesamehe
21Kisha Petro akamwendea Yesu, akamwuliza, “Je, ndugu yangu akinikosea, nimsamehe mara ngapi? Mara saba?” 22Yesu akamjibu, “Sisemi mara saba tu, bali sabini mara saba. 23Ndiyo maana ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake. 24Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta 10,000. 25Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru auzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe. 26Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, ‘Unisubiri nami nitakulipa deni lote’. 27Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake.
28“Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha dinari 100. Akamkamata, akamkaba koo akisema, ‘Lipa deni lako!’ 29Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, ‘Unisubiri nami nitakulipa’. 30Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni.
31“Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia. 32Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, ‘Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote. 33Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?’
34“Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote. 35Na baba yangu aliye mbinguni atawafanyieni vivyo hivyo kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kwa moyo wake wote.”

Yahweh tunaomba utuepushe katika majaribu na utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Jehovah tuyaweka maisha yetu mikononi mwako..
tunaomba utubariki na ukabariki kazi za mikono yetu na yote tunayoenda kufanya/kutenda tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo nasi utupe neema ya kuwabariki wenye kuhitaji..

tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mfalme wa Amani ukatupe kama inavyokupendeza wewe..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike sawasawa na mapenzi yako..

Mungu wetu tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu na ukawaponye wote wataabikao,wenye shida/tabu,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,wagonjwa na wafiwa ukawe mfariji wao 
na ukawape neema ya kusimamia Neno lako Amri na sheria zako ...

wakapate kuwa huru rohoni na mwilini..

Roho Mtakatifu akatuongoze vyema,tusiwe watu wa kuhukumu wengine,tusiwe watu wa kudharau wengine na kukatisha tamaa..
tukawe na upendo wa kweli na kiasi katikayote..


Usimhukumu ndugu yako
1Mkaribisheni kwenu mtu aliye dhaifu, lakini msibishane naye juu ya mawazo yake binafsi. 2Watu hutofautiana: Mmoja imani yake inamruhusu kula kila kitu; lakini mwingine ambaye imani yake ni dhaifu, hula tu mboga za majani. 3Mtu ambaye hula kila kitu asimdharau yule ambaye hawezi kula kila kitu; naye ambaye hula tu mboga za majani asimhukumu anayekula kila kitu, maana Mungu amemkubali. 4Wewe ni nani hata uthubutu kumhukumu mtumishi wa mwingine? Akisimama au akianguka ni shauri la Bwana wake; naam, atasimama imara, maana Bwana anaweza kumsimamisha.
5Mtu anaweza kufikiria siku fulani kuwa ya maana zaidi kuliko nyingine; mtu mwingine aweza kuzifikiria siku zote kuwa sawa. Kila mmoja na afuate msimamo wa akili yake. 6Anayeadhimisha siku fulani anaadhimisha siku hiyo kwa ajili ya kumtukuza Mungu; naye anayekula chakula fulani anafanya hivyo kwa kumtukuza Bwana maana anamshukuru Mungu. Kadhalika naye anayeacha kula chakula fulani anafanya hivyo kwa ajili ya kumtukuza Bwana, naye pia anamshukuru Mungu. 7Maana hakuna mtu yeyote miongoni mwetu aishiye kwa ajili yake mwenyewe, wala hakuna anayekufa kwa ajili yake mwenyewe 8maana tukiishi twaishi kwa ajili ya Bwana; tukifa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi, kama tukiishi au tukifa, sisi ni mali yake Bwana. 9Maana Kristo alikufa, akafufuka ili apate kuwa Bwana wa walio hai na wafu. 10Kwa nini basi, wewe wamhukumu ndugu yako? Nawe, kwa nini wamdharau ndugu yako? Sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. 11Maana Maandiko yanasema:
“Kama niishivyo, asema Bwana,
kila mtu atanipigia magoti,
na kila mmoja atakiri kwamba mimi ni Mungu.”
12Kwa hiyo, kila mmoja wetu atatoa hoja juu yake mwenyewe mbele ya Mungu.


Asante Mungu Baba ...Sifa na utukufu ni wako..
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa kwakuwa nami/kunisoma..
Mungu aendelee kuwa nayi daima..
Nawapenda.


Waisraeli na Baali wa Peori
1Waisraeli walipokuwa huko Shitimu, wanaume walianza kuzini na wanawake wa Moabu. 2Wanawake hao waliwaalika Waisraeli washiriki matambiko waliyotambikia miungu yao, nao Waisraeli wakala chakula na kuiabudu miungu yao. 3Ndivyo Waisraeli walivyojiunga na mungu Baali wa Peori, nayo hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawaka dhidi yao. 4Basi, Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Wachukue viongozi wote wa Israeli, uwanyonge mbele yangu juani, ili ghadhabu yangu dhidi yenu ipite.” 5Mose akawaambia waamuzi wa Israeli, “Kila mmoja wenu amuue mtu yeyote miongoni mwenu ambaye amejiunga na mungu Baali wa Peori.”
6Wakati huohuo mtu mmoja akamleta mwanamke mmoja Mmidiani nyumbani kwake, Mose na jumuiya yote ya watu wa Israeli wakiwa wanaomboleza penye lango la hema la mkutano. 7Basi, Finehasi mwana wa Eleazari mwana wa kuhani Aroni alipoona hayo, aliinuka akatoka katika hiyo jumuiya, akachukua mkuki 8na kumfuatia yule Mwisraeli mpaka hemani, akawachoma mkuki wote wawili tumboni. Maradhi mabaya yaliyokuwa yamewaangamiza Waisraeli yakakomeshwa. 9Waliokufa kutokana na maradhi yale mabaya walikuwa watu 24,000.
10Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 11“Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, ameizuia hasira yangu dhidi ya Waisraeli; miongoni mwenu ni yeye tu aliyeona wivu kama nilio nao mimi. Ndio maana sikuwaangamiza Waisraeli wote kwa hasira yangu. 12Kwa hiyo mwambie kwamba ninafanya naye agano la amani. 13Naagana naye kwamba yeye na wazawa wake watakuwa makuhani milele kwa sababu aliona wivu kwa ajili yangu, Mungu wake, akawafanyia upatanisho Waisraeli.”
14Huyo Mwisraeli aliyeuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani aliitwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa mojawapo katika kabila la Simeoni. 15Na huyo mwanamke Mmidiani aliyeuawa aliitwa Kozbi binti Suri, aliyekuwa kiongozi wa ukoo fulani huko Midiani.
16Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, 17“Wachokoze Wamidiani na kuwaangamiza, 18kwa sababu waliwachokoza nyinyi kwa hila zao, wakawadanganya kuhusu jambo la Peori, na kwa sababu ya Kozbi, binti yao, aliyeuawa wakati maradhi mabaya yalipozuka kule Peori.


Hesabu25;1-18


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.


No comments: