Ni matumaini yangu hamjambo na manaendelea vyema na majukumu yenu.. Wapendwa/Waungwana "Jikono Leo" ni Boga/Maboga,nafikiri wengi mnayajua hata kama hujawahi kula.. Jee wewe ni mpenzi wa Maboga? Unapikaje?hapo ulipo yanapatikana?watoto wako wanayapenda? Mimi ni mpenzi sana wa Boga mama yangu alikuwa analima sana, Nyumbani kwa mama tulikuwa tunapika -kuchemsha wakati mwingine tunachanganya na mihogo na tunaunga/tia Nazi,lakini wakati wa kula kona zilikuwa nyingi wengi tulikuwa tunaacha mihogo na tunakula maboga hasa ile rojo yake maana huwa yanarainika sana kwenye mchanganyo[Futari].. Hapa nilipo yapo lakini ni ghali kidogo.. watu wengi niliowauliza kama wanayapenda/wanakula? wengi hawali,wengine wanasema huwa wanatengeneza supu,wengine hawajui kabisa kama haya yanaliwa.. Wao wanajua ni kwasababu ya siku kuu ya Halloween huwa yanafanya mapambo ya hiyo kitu yao huwa wanachonga/kutengeneza mapambo ya Halloween.. Hayyahh halloween na Maboga... Kwanza sikuwahi kuisikia hii siku kuu nilipokuwa nyumbani haya mambo nimekutana nayo huku ya kuvaa vitu vya kutisha na watoto usiku wanaenda kila nyumba wanapewa pipi,chocolate [trick or treat]maana zaidi ya halloween unaweza kuipata Google.. Tena hiki ndiyo kipindi chake inakuja hiyo siku.. Eeeh nasikia Bongo-Tanzania nako kuna hiyo siku kwa watoto wa doti comu,wanaoenda na wakati na mitandao..[sina hakika na hili]
Tuendelee na mapishi katika picha... |
No comments:
Post a Comment