Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah..!Haleluyah..!Haleluyah..!Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mtakatifu..!Mtakatifu..!Mtakatifu..!Baba wa Mbinguni..
Mungu wetu,Muumba wetu,Muumba wa Mbingu na Nchi na vyote vinavyoonekana na visivyo onekana..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..!
Muweza wa yote,Hakuna kama wewe,Unastahili sifa,
Unastahili kuabudiwa,Unasthahili kutukuzwa,unastahili ee Mungu..!
Uhimidiwe Jehovah,Unatosha Baba wa Mbinguni,
Matendo yako ni makuu sana,matendo yako ni
ya ajabu,wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Alfa na Omega..!
“Sikiliza!” Asema Yesu, “Naja upesi pamoja na tuzo nitakalompa kila mmoja kufuatana na matendo yake. Mimi ni Alfa na Omega, wa kwanza na wa mwisho, mwanzo na mwisho.” Heri yao wale wanaoosha mavazi yao, wapate kuwa na haki ya kula tunda la mti wa uhai, na haki ya kuingia mjini kwa kupitia milango yake. Lakini mbwa, wachawi, wazinzi, wauaji, waabudu sanamu na wote wanaopenda kusema uongo, watakaa nje ya mji. “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!” Roho na Bibi arusi waseme, “Njoo!” Kila mtu asikiaye hili, na aseme, “Njoo!” Aliye na kiu na aje; anayependa, na achukue maji ya uhai bila malipo.
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa kutuchagua na kutupa kibali cha kuendelea
kuiona leo hii Mungu wetu..
Asante kwa pumzi/uzima na ukatufanye tayari kwa majukumu yetu na kujiandaa kwa yajayo..
“Lakini, juu ya siku au saa hiyo, hakuna mtu ajuaye itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye. Kwa maana kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu. Maana nyakati hizo, kabla ya gharika kuu, watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, mpaka Noa alipoingia ndani ya ile safina. Hawakujua kuna nini mpaka ile gharika ilipotokea, ikawakumba wote. Ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Mtu atakapokuja. Wakati huo watu wawili watakuwa shambani; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Kina mama wawili watakuwa wanasaga nafaka, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa. Basi, kesheni, kwa maana hamjui siku atakayokuja Bwana wenu. Lakini kumbukeni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua siku mwizi atakapofika, angekesha, wala hangeiacha nyumba yake ivunjwe. Kwa hiyo, nanyi pia muwe tayari, kwa maana Mwana wa Mtu atakuja saa msiyoitazamia.”
Si kwamba sisi ni wema sana,si kwa nguvu zetu wala utashi wetu
sisi kuwa hivi tulivyo leo hii Yahweh ni kwa mapenzi yako
ni kwa neema/rehema zako Mungu wetu sisi kuwa hivi tulivyo
Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Mungu wetu..
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na tukijiachilia mikononi mwako Mungu wetu..
Tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya..
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Baba
utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba utufunike kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana
na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti...
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
“Kweli nawaambieni, yeyote yule asiyeingia katika zizi la kondoo kwa kupitia mlangoni, bali hupenya na kuingia kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyanganyi. Lakini anayeingia kwa kupitia mlangoni, huyo ndiye mchungaji wa kondoo. Mngojamlango wa zizi humfungulia, na kondoo husikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kila mmoja kwa jina lake, na kuwaongoza nje. Akisha watoa nje huwatangulia mbele, nao kondoo humfuata, kwani wanaijua sauti yake. Kondoo hao hawawezi kumfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti yake.” Yesu aliwaambia mfano huo, lakini wao hawakuelewa alichotaka kuwaambia.
Jehovah tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu,Biashara,Masomo na vyote tunavyenda kugusa kutumia Mungu wetu tunaomba ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Mungu wetu vyote tunavyoenda kufanya/kutenda tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji,Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbingu tunaomba utupe sawasawana mapenzi yako..
Mfalme wa Amani tunaomba Amani na Upendo vikatawale katika Nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,famila/ndugu na wote wanaotuzunguka,Mungu wetu tunaomba ulinzi wako wakati wote
Baba wa Mbimnguni tunaomba utamalaki na kutuatamia..
Yahweh tunaomba uwe nasi katika yote,Mungu wetu tunaomba mkono wako wenye nguvu ukatuguse ,ukatutakase na kutufunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo,Mungu wetu ukatupe neema ya kuweza kusimamia Neno lako Amri na Sheria zako siku zote za maisha yetu ,Ukatufanye chombo chema Baba nasi
tukatumike kama inavyokupendeza wewe...
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe
na kiasi..
Basi, akasema tena, “Kweli nawaambieni, mimi ni mlango wa kondoo. Wale wengine wote waliokuja kabla yangu ni wezi na wanyanganyi, nao kondoo hawakuwasikiliza. Mimi ni mlango. Anayeingia kwa kupitia kwangu ataokolewa; ataingia na kutoka, na kupata malisho. Mwizi huja kwa shabaha ya kuiba, kuua na kuharibu. Mimi nimekuja mpate kuwa na uhai – uhai kamili. “Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo wake. Mtu wa kuajiriwa ambaye si mchungaji, na wala kondoo si mali yake, anapoona mbwamwitu anakuja, huwaacha kondoo na kukimbia, kisha mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya. Yeye hajali kitu juu ya kondoo kwa sababu yeye ni mtu wa mshahara tu. Mimi ni mchungaji mwema. Nawajua walio wangu, nao walio wangu wananijua mimi, kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Mimi nayatoa maisha yangu kwa ajili yao.
Baba wa Mbinguni tazama wenye shida/tabu,wagonjwa,wenye njaa waliokata tamaa,waliokatawaliwa,walioumizwa,walio katika
vifungo vya yule mwovu,wote wataabikao,
wanaopitia magumu/majaribu mbali mbali,Mungu wetu tunaomba ukawaguse na mkono wako wenye nguvu,Baba ukawape uponyajiwa mwili na roho pia, Mungu wetu ukawasimamishe wote walioanguka,
Mungu wetu ukasikie kulia kwao Baba ukawafute
machozi ya watoto wako,Mungu wetu ukawape neema ya kuweza kujiombea na kufuata njia zako nazo ziwaweke huru..
Baba wa Mbinguni ukawape msamaha wale wote waliokwenda kinyume nawe,Mungu wetu wakuombapo kwa imani Baba ukawape Amani na kupokea sala/maombi yao..
Tena ninao kondoo wengine ambao hawamo zizini humu. Inanibidi kuwaleta hao pia, nao wataisikia sauti yangu, na kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. “Baba ananipenda kwani nautoa uhai wangu ili nipate kuupokea tena. Hakuna mtu anayeninyanganya uhai wangu; mimi nautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa na uwezo wa kuuchukua tena. Hivi ndivyo Baba alivyoniamuru nifanye.” Kukawa tena na mafarakano kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya. Wengi wao wakasema, “Ana pepo; tena ni mwendawazimu! Ya nini kumsikiliza?” Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mwenye pepo. Je, pepo anaweza kuyafumbua macho ya vipofu?”
Asante Mungu wetu yote tunayaweka mikononi mwako..
Tukiamini na kushukuru daima..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!!
Asanteni sana wapendwa katika Bwana..
Mungu wetu aendelee kuonekana kwa kila jambo
mfanyalo,naye akawape Baraka na kuwaongezea zaidi
ya mnapojitoa,msipungukiwe katika mahitaji yenu
Baba wa Mbinguni akawape kama inavyompendeza yeye..
Nawapenda.
|
No comments:
Post a Comment