Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tusalimiane na kukumbushana wema wa Mungu na fadhili zake..
Jee unamkumbuka Ndugu yako katika Kristo katika lipi? kwa wema wake?kujitoa katika kazi ya Mungu /kanisa? kujitoa kwa wapendwa wengine ndani na nje ya kanisa? Hekima,Busara,uvumilivu,upatanishi,uongozi bora,Upendo,ucheshi, unyenyekevu,amani,ukweli,uimbaji wake? na vingine vingi unaweza kusema ambavyo mimi sikuviweka...
Jee asipokuwepo kunakuwa na pengo,upweke,kupwaya na kuhisi kunaupungufu kidogo?
Au unamkumbuka Ndugu yako katika Kristo kwa baya lipi? Makwazo,ugombanishi,uongo,uzushi,ukorofi,kisirani,unafiki?na vingine vingi unavyoona vibaya ambavyo mimi sikuviweka wewe unaviju..
Jee umechukua hatua gani? Umemsifia kwa mema/mazuri anayoyafanya na kumuombea aendelee kusimamia hayo na Mungu aendelee kumuongoza katika yote yampendezayo?
Jee kwa mabaya pia umechukua hatua gani? Au unaendeleza nawe ubaya na kusengenya pembeni? Umejaribu kumshauri hiyo njia siyo?na kumuonya/kumuelisha kwa upendo,hekima na busara?
Jee unampenda?au unamdanganya na unajidanganya mwenyewe kwa sababu upendo wa kweli ni kumwambia ukweli naye anaweza kujirudi hata kama kwa wakati ule alihamaki lakini atajifikiria na kuchukua hatua....
Ebu tujaribu leo kwa watu 2 wa karibu yako iwe kwa mazuri yao au mabaya yao,unaweza kufikiri kwamba alikuwa anatenda vibaya kwa jambo unaloliona wewe lakini kumbe anasababu na anaweza kukupa sababu ya kufanya hivyo.. Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote tunayoenda kufanya/kutenda, kunena na tukanene yaliyo yake.. Mungu ni pendo apenda watu... Nakupenda.. Tuendelee...
Napenda kumjulisha kwenu dada yetu Foibe ambaye ni mtumishi katika kanisa la Kenkrea. Mpokeeni kwa ajili ya Bwana kama iwapasavyo watu wa Mungu. Mpeni msaada wowote atakaohitaji kutoka kwenu, maana yeye amekuwa mwema sana kwa watu wengi na kwangu pia. Salamu zangu ziwafikie Priska na Akula, wafanyakazi wenzangu katika utumishi wa Kristo Yesu. Wao walihatarisha maisha yao kwa ajili yangu. Wanastahili shukrani; si tu kutoka kwangu, bali pia kutoka kwa makanisa yote ya watu wa mataifa mengine. Salamu zangu pia kwa kanisa linalokutana nyumbani kwao. Salamu zangu zimfikie rafiki yangu Epaineto ambaye ni wa kwanza katika mkoa wa Asia kumwamini Kristo. Nisalimieni Maria ambaye amefanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu. Salamu zangu kwa Androniko na Yunia, wananchi wenzangu waliofungwa gerezani pamoja nami; wao wanajulikana sana kati ya mitume; tena walikuwa Wakristo kabla yangu mimi. Salamu zangu kwa Ampliato, rafiki yangu katika kuungana na Bwana. Salamu zangu zimfikie Urbano, mfanyakazi mwenzangu katika utumishi wa Kristo; salamu zangu pia kwa rafiki yangu Staku. Nisalimieni Apele ambaye uaminifu wake kwa Kristo umethibitishwa. Salamu zangu kwa wote walio nyumbani mwa Aristobulo. Salamu zangu kwa Herodiana, mwananchi mwenzangu; na kwa jamaa yote ya Narkisi iliyojiunga na Bwana. Nisalimieni Trufena na Trufosa wanaofanya kazi katika utumishi wa Bwana, na rafiki yangu Persi ambaye amefanya mengi kwa ajili ya Bwana. Nisalimieni Rufo, mtu hodari sana katika kazi ya Bwana, na mama yake ambaye ni mama yangu pia. Nisalimieni Asunkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma na ndugu wote walio pamoja nao. Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, pamoja na watu wote wa Mungu walio pamoja nao. Salimianeni nyinyi kwa nyinyi kwa ishara ya upendo. Salamu kwenu kutoka kwa makanisa yote ya Kristo.
Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu.. Asante Baba wa Mbinguni kwa ulinzi wako wakati wote.. Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuina leo hii..Si kwamba sisi tumetenda mema sana,wala si kwa nguvu/utashi wetu sisi kuwa hivi tulivyo ni kwa neema/rehema zako Mungu wetu ni kwa mapenzi yako...
Ukuu ni wako, ee Mwenyezi-Mungu, una nguvu, utukufu, ushindi na enzi. Vyote vilivyoko mbinguni na duniani ni vyako. Ee Mwenyezi-Mungu, ufalme ni wako, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote. Utajiri na heshima hutoka kwako, vyote wavitawala. Uwezo na nguvu vimo mkononi mwako, nawe wawakuza uwapendao, na huwaimarisha wote. Sasa ee Mungu wetu, tunakushukuru na kulisifu jina lako tukufu.
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachlia mikononi mwako Baba wa Mbinguni.. Yahweh tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua.. Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea.. Jehovah tunaomba utuepushe katika majaribu Baba utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote.. Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Jehovah utufunikekwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti.. yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Ndugu zangu, nawasihi mwafichue wote wanaosababisha mafarakano na kuwafanya watu wengine waanguke, kinyume cha mafundisho mliyofundishwa. Jiepusheni na watu hao, maana watu wa namna hiyo hawamtumikii Kristo Bwana wetu, bali wanayatumikia matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao matamu na hotuba za kubembeleza hupotosha mioyo ya watu wanyofu. Kila mtu amesikia juu ya utii wenu katika mambo mema, na bila hatia kuhusu mambo mabaya. Naye Mungu aliye chanzo cha amani hatakawia kumponda Shetani chini ya miguu yenu. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi. Timotheo, mfanyakazi mwenzangu, anawasalimu. Hali kadhalika Lukio, Yasoni, na Sosipateri, wananchi wenzangu, wanawasalimu. Nami Tertio, ninayeandika barua hii, nawasalimuni kwa jina la Bwana. Gayo, mwenyeji wangu, pamoja na kanisa lote linalokutana kwake, anawasalimu. Erasto, mweka hazina wa mji huu, pamoja na Kwarto, wanawasalimu. [ Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amina.]
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu vyote tunavyoenda kufanya/kutenda Yahweh tukatende kama inavyo kupendeza wewe.. Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji.. Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Mfalme wa Amani tunaomba amani yako ikatawale katika nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Yahweh tunaomba ulinzi wako, Baba tunaomba ukatamalaki na kutuatamia,ukatubariki, Baba wa Mbinguni tukawe na kiu/shauku ya kujua/kufuata njia zako, kusoma Neno lako na likawe taa na Nuru kwenye maisha yetu Ukatupe neema ya kusimamia Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu.. Tukawe barua njema na tukasomeke kama inavyokupendeza wewe.. Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote tukawe na kiasi... Ee Baba ukasikie kuomba kwetu na ukapokee maombi/sala zetu..
Basi, sasa na tumsifu Mungu! Yeye anaweza kuwaimarisheni katika ile Habari Njema niliyohubiri juu ya Yesu Kristo, na katika ile siri iliyofunuliwa na ambayo ilikuwa imefichika kwa karne nyinyi zilizopita. Lakini, sasa ukweli huo umefunuliwa kwa njia ya maandiko ya manabii; na kwa amri ya Mungu wa milele umedhihirishwa kwa mataifa yote ili wote waweze kuamini na kutii. Kwake Mungu aliye peke yake mwenye hekima, uwe utukufu kwa njia ya Yesu Kristo, milele na milele! Amina.
Tazama wenye shida/tabu,wagonjwa,wenye njaa,walio katika vifungo mbalimbali,wanaopitia magumu/majaribu, waliokata tamaa Baba wa Mbinguni ukawape tumaini Yahweh ukawape neema ya kujiombea,kusimamia njia zako ukawaguse na mkono wako wenye nguvu Yahweh wakapate kupona kimwili na kiroho pia,ukawape ubunifu katika kazi,kilimo, biashara na ukawatendee sawasawa na mapenzi yako.. Sifa na utukufu tunakurudishia Mungu wetu.. Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele.. Amina..!!
Wapendwa katika Bwana asanteni kwakuwa pamoja nami Mungu wa Upendo akadumu katika maisha yenu... aendelee kuwabariki nanyi mkawe baraka kwa wengine.. Nawapenda. |
No comments:
Post a Comment