Wapendwa/waungwana natumaini hamjambo na mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku,Pamoja na hayo siku haipiti na wala mambo hayatoenda sawa kama ukiwa na njaa.. ni "Jikoni Leo"mimi leo nimeandaa/pika KUNDE je wewe leo unapika/umepika nini? Kunde hizi nimepewa zawadi kutoka Nyumbani Tanzania [Bongo] Nimezichagua na nikaziacha/loweka kwenye maji usiku mzima,Asubuhi nikaziweka/bandika/tereka..... ok jikoni kwa kuzichemsha mpaka zilivyoiva,nikakatia/weka Kitunguu maji na chumvu zikachemka kidogo nikaongezea/unga nazi tuu sikuweka viuongo vingi...
Mimi hupenda kula na maandazi[zege kibongobongo/kiswazi] pia wali/ubwabwa...! jee wewe unapenda kunde na je unapikaje? na unapenda kula na nini? Karibuni sana... |
No comments:
Post a Comment