Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 24 November 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;Waamuzi 10...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Mfalme wa Amani,Kimbilio
letu,Mponyaji wetu,Mungu wa upendo,Baba wa faraja,Mungu mwenye
huruma,Mungu mwenye kusamehe,Hakuna kama wewe..!

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari katika majukumu yetu
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwa nguvu zetu wala utashi wetu,si kwa akili zetu wala si kwa uwezo wetu,si kwamba sisi tumetenda mema sana si kwamba sisi ni wazuri mno
hapana ni kwa neema/rehema zako,Ni kwa mapenzi yako Mungu wetu
sisi kuwa hivi tulivyo leo hii..
Unastahili sifa Baba wa Mbinguni,Unastahili kuabudiwa Mungu wetu
Unastahili kuhimidiwa Yahweh,Unastahili kutukuzwa Jehovah..
Unatosha Baba wa Mbinguni....!



Baada ya siku ya Sabato, Maria Magdalene, Salome na Maria mama yake Yakobo walinunua manukato ili wakaupake mwili wa Yesu. Basi, alfajiri na mapema siku ya Jumapili, walifika kaburini, jua lilipoanza kuchomoza. Nao wakawa wanaambiana, “Nani atakayetuondolea lile jiwe mlangoni mwa kaburi?” Lakini walipotazama, waliona jiwe limekwisha ondolewa. (Nalo lilikuwa kubwa mno.) Walipoingia kaburini, walimwona kijana mmoja aliyevaa vazi jeupe, ameketi upande wa kulia; wakashangaa sana. Lakini huyo kijana akawaambia, “Msishangae. Mnamtafuta Yesu wa Nazareti aliyesulubiwa. Amefufuka, hayumo hapa. Tazameni mahali walipokuwa wamemlaza. Nendeni mkawaambie wanafunzi wake pamoja na Petro ya kwamba anawatangulieni kule Galilaya. Huko mtamwona kama alivyowaambieni.” Basi, wakatoka pale kaburini mbio, maana walitetemeka kwa hofu na kushangaa. Hawakumwambia mtu yeyote kitu, kwa sababu waliogopa mno. 

Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia
mikononi mwako Mungu wetu..
Baba wa Mbinguni tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyoyafanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Baba tunaomba utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote...
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Yahweh tunaomba
utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa 
Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..



Yesu alipofufuka mapema Jumapili, alijionesha kwanza kwa Maria Magdalene, ambaye Yesu alikuwa amemtoa pepo wabaya saba. Maria Magdalene akaenda, akawajulisha wale waliokuwa pamoja na Yesu, na wakati huo walikuwa wanaomboleza na kulia. Lakini waliposikia ya kwamba Yesu yu hai na kwamba Maria Magdalene amemwona, hawakuamini.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu,Baba wa Mbinguni
ukatupe ubunifu na maarifa katika ufanyaji/utendaji Yahweh nasi
Tutakatende sawasawa na mapenzi yako,Yahweh tunaomba ukabariki
ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba utupe
neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji,Mungu wetu tunaomba
tusipungukiwe katika mahitaji yetu Yahweh ukatupe kama inavyokupendeza wewe..




Baadaye Yesu aliwatokea wanafunzi wawili akiwa na sura nyingine. Wanafunzi hao walikuwa wanakwenda shambani. Nao pia wakaenda, wakawaambia wenzao. Hata hivyo hawakuamini.
Mfalme wa Amani tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba amani yako ikatawale katika nyumba/ndoa
zetu,watoto,wazazi wetu,Familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Baba wa Mbinguni ukatawale na kutuatamia,Mungu wetu ukatupe
neema ya kufuata njia zako,tukasimamie Neno lako amri na sheria 
zako siku zote za maisha yetu,Tukanene yaliyoyako,Mungu wetu ukaonekane popote tupitapo,utu wema,fadhili,nidhamu,upendo,amani,
unyenyekevu ,huruma na vyote vikupendezavyo visipungue..
Ukatuokoe na kiburi,majivuno,kujitapa,kujiona,makwazo,unafiki na
yote yanayokwenda kinyume nawe..
Ukatufanye Barua njema Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...



Mwishowe Yesu aliwatokea wanafunzi kumi na mmoja walipokuwa pamoja mezani. Akawakemea sana kwa sababu ya kutoamini kwao na ukaidi wao, maana hawakuwaamini wale waliokuwa wamemwona baada ya kufufuka. Basi, akawaambia, “Nendeni ulimwenguni kote mkahubiri Habari Njema kwa kila mtu. Anayeamini na kubatizwa ataokolewa. Asiyeamini atahukumiwa. Na ishara hizi zitaandamana na wale wanaoamini: Kwa jina langu watatoa pepo na watasema kwa lugha mpya. Wakishika nyoka au wakinywa kitu chochote chenye sumu, hakitawadhuru. Watawawekea wagonjwa mikono, nao watapona.”

Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye
nguvu na ukawaponye wagonjwa,wenye njaa ukawapatie chakula,
waliokatika magumu/majaribu Baba wa Mbinguni ukawe msaada wao
walio katika vifungo vya yule mwovu Yahweh ukawaweke huru,
waliokata tamaa Mungu wetu wakapate tumaini lako,Nguvu za giza,
za mizimu,za mapepo na za mpinga Kristo zishindwe katika jina la
Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti...
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako..
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao..
Baba wa Mbinguni tunaomba ukapokee sala/maombi yetu..
Kwa imani tunayaweka haya yote mikononi mwako
Tukiamini na kushukuru daima..


Basi, Bwana Yesu alipokwisha sema nao, akachukuliwa mbinguni, akaketi upande wa kulia wa Mungu. Wanafunzi wakaenda wakihubiri kila mahali. Bwana akafanya kazi pamoja nao na kuimarisha ujumbe huo kwa ishara zilizoandamana nao. 
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwa nami
Mungu aendelee kuwabariki na kuwalinda muingiapo/mtokapo
popote mpitapo Bwana awe nanyi Daima..
Nawapenda.

Tola
1Baada ya kifo cha Abimeleki, Tola mwana wa Pua mwana wa Dodo, wa kabila la Isakari, akatokea kuwakomboa Waisraeli. Tola aliishi Shamiri katika nchi ya milima ya Efraimu. 2Alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini na mitatu, kisha akafariki na kuzikwa huko Shamiri.

Yairi

3Baada ya Tola, alitokea Yairi wa Gileadi, akawa mwamuzi wa Waisraeli kwa miaka ishirini na miwili. 4Yairi alikuwa na watoto wa kiume thelathini ambao walipanda punda thelathini na walikuwa na miji thelathini katika nchi ya Gileadi, ambayo mpaka leo inaitwa Hawoth-yairi.10:4 Hawoth-yairi: Maana yake ni vijiji vya Yairi. 5Yairi alifariki na kuzikwa huko Kamoni.

Yeftha

6Waisraeli walitenda tena uovu mbele ya Mwenyezi-Mungu wakatumikia Mabaali, Maashtarothi, na miungu ya Shamu, ya Sidoni, ya Moabu, ya Amoni na ya Wafilisti. Walimwacha Mwenyezi-Mungu na wala hawakumwabudu tena. 7Hasira ya Mwenyezi-Mungu ikawaka dhidi ya Israeli, naye akawatia mikononi mwa Wafilisti na Waamoni. 8Kwa miaka kumi na minane hao waliwatesa na kuwakandamiza Waisraeli walioishi huko Gileadi katika eneo la Waamori mashariki ya mto Yordani. 9Waamoni nao walivuka mto Yordani kupigana na makabila ya Yuda, Benyamini na Efraimu. Nao Waisraeli wakapata taabu sana.
10Basi wakamlilia Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Tumetenda dhambi dhidi yako, maana tumekuacha wewe Mungu wetu, tukatumikia Mabaali.” 11Naye Mwenyezi-Mungu akawaambia, “Je, mimi sikuwakomboa kutoka kwa Wamisri, Waamoni, Waamori, Wafilisti? 12Wasidoni, Waamaleki na Wamidiani waliwakandamiza nanyi mkanililia, nami nikawakomboa mikononi mwao. 13Hata hivyo nyinyi mmeniacha, mkatumikia miungu mingine. Kwa hiyo sitawakomboeni tena. 14Nendeni mkaililie hiyo miungu mliyoichagua. Iacheni hiyo iwakomboe katika taabu zenu!”
15Lakini Waisraeli wakamwambia Mwenyezi-Mungu, “Tumetenda dhambi. Tufanye upendavyo, lakini tunakuomba utuokoe leo.” 16Kisha wakaitupilia mbali miungu ya kigeni, wakamtumikia tena Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu hakuweza kuvumilia zaidi kuona taabu za Waisraeli.
17Waamoni wakajikusanya wakapiga kambi yao huko Gileadi. Waisraeli nao wakakusanyika na kupiga kambi yao huko Mizpa. 18Waisraeli na viongozi wao wakaulizana, “Ni nani atakayeanza kupigana na Waamoni? Atakayefanya hivyo ndiye atakayekuwa kiongozi wa wakazi wote wa Gileadi.”

Waamuzi 10;1-18

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.


No comments: