Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu.. Asante Baba wa Mbinguni kwa ulinzi wako kwetu wakati wote.. Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii... Si kwa nguvu zetu wala si kwa utashi wetu,si kwamba tumetenda mema sana wala si kwamba sisi si wakosefu ,wala si kwa uwezo wetu.. Mungu wetu ni kwa neema/rehema zako,ni kwa mapenzi yako Mungu wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii... Mungu wetu utuangalie kwa wema na utufadhili,Wema na uadilifu vituhifadhi,maana tunakutumainia wewe Mungu wetu, Tusikubali kushindwa kwa ubaya,bali tushinde ubaya kwa wema, Mwenyezi-Mungu atuonyeshe wema wake na kutupa amani, Tusipende uovu kuliko wema,tusipende uongo kuliko wema. Utuonee huruma, ee Mungu utubariki,tuelekeze uso wako kwa wema. Utukuzwe ee Mungu wetu,Uabudiwe Baba wa Mbinguni,Usifiwe ee Mungu wetu,Uhimidiwe Jehovah,Matendo yako ni makuu sana.. Unatosha Mungu wetu..!!
Yesu aliwaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama isingekuwa hivyo, ningalikwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieni nafasi. Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi, nitarudi na kuwachukueni kwangu, ili nanyi muwe pale nilipo mimi. Mnajua njia ya kwenda huko ninakokwenda.” Thoma akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda, tutawezaje basi, kuijua hiyo njia?” Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na ukweli na uhai. Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu. Ikiwa mnanijua mimi, mnamjua na Baba yangu pia. Na tangu sasa, mnamjua, tena mmekwisha mwona.” Filipo akamwambia, “Bwana, tuoneshe Baba, nasi tutatosheka.” Yesu akamwambia, “Nimekaa nanyi muda wote huu, nawe Filipo hujanijua? Aliyekwisha niona mimi amemwona Baba. Unawezaje basi, kusema: ‘Tuoneshe Baba?’ Je, huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambieni siyasemi kwa mamlaka yangu; Baba aliye ndani yangu anafanya kazi yake. Mnapaswa kuniamini ninaposema kwamba mimi niko ndani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu. Ama sivyo, aminini kwa sababu ya mambo ninayofanya. Kweli nawaambieni, anayeniamini atafanya mambo ninayofanya mimi; naam, atafanya hata makuu zaidi, kwani ninakwenda kwa Baba. Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba chochote kwa jina langu, nitawafanyieni.
Mungu wetu Baba yetu,Tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza, tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Yahweh.. Baba wa Mbinguni tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Ee Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea.. Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Baba utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote.. Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Baba tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Baada ya hayo, Yesu akatoka nje, akamwona mtozaushuru mmoja aitwaye Lawi, ameketi ofisini. Yesu akamwambia, “Nifuate!” Naye akaacha yote akamfuata. Lawi akamwandalia Yesu karamu kubwa nyumbani mwake. Na kundi kubwa la watozaushuru na watu wengine walikuwa wameketi pamoja nao. Mafarisayo na waalimu wa sheria wakawanungunikia wanafunzi wake wakisema: “Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?” Yesu akawajibu, “Wenye afya hawamhitaji daktari; wanaomhitaji ni wale walio wagonjwa. Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi, wapate kutubu.”
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Yahweh ukatupe ubunifu/maarifa katika ufanyaji/utendeji Mungu wetu tukatende kama inavyokupendeza wewe.. Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji.. Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba utupe sawasawa na mapenzi yako..
Mfalme wa Amani tunaomba amani yako ikatawale katika nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka.. Mungu wetu tunaomba ulinzi wako Yahweh ukatulinde sisi na vyote tunavyovimiliki.. Jehovah tunaomba baraka zako,upendo wetu ukadumu,Amani moyoni,utuwema,unyenyekevu, busara.hekima na vyote vinavyokupendeza wewe, Baba wa Mbinguni ukatamalaki na kutuatamia, Yahweh ukatupe neema ya kusimamia neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu.. Baba ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe.. Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
“Mkinipenda mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi mwingine, atakayekaa nanyi milele. Yeye ni Roho wa ukweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini nyinyi mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu. “Sitawaacha nyinyi yatima; nitakuja tena kwenu. Bado kidogo nao ulimwengu hautaniona tena, lakini nyinyi mtaniona; na kwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa hai. Siku ile itakapofika mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, nanyi mko ndani yangu, nami ndani yenu. Azipokeaye amri zangu na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” Yuda (si yule Iskarioti) akamwambia, “Bwana, itawezekanaje wewe kujidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?” Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika neno langu, na Baba yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kukaa naye. Asiyenipenda hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba aliyenituma. “Nimewaambieni mambo haya nikiwa bado pamoja nanyi, lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowaambieni. “Nawaachieni amani; nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike. Mlikwisha sikia nikiwaambieni: ‘Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu.’ Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye ni mkuu kuliko mimi. Nimewaambieni haya sasa kabla hayajatokea, ili yatakapotokea mpate kuamini. Sitasema nanyi tena mambo mengi, maana mtawala wa ulimwengu huu anakuja. Kwangu mimi hawezi kitu; lakini ulimwengu unapaswa kujua kwamba nampenda Baba, na ndiyo maana nafanya kila kitu kama Baba alivyoniamuru. Simameni, tutoke hapa!
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,walio magerezani pasipo na hatia Mungu wetu ukawatendee,waliokatika vifungo vya yule mwovu Yahweh tunaomba ukawafungue na wakawe huru.. Wangojwa ukawaponye kimwili na kiroho pia,wenye njaa ukawape chakula na ukabariki mashamba/kazi,biashara zao wakapate chakula cha kutosha na kuweka akiba..Jehovah ukawape neema ya kuweza kujiombea na kufuata njia zako,Nuru ikaangaze katika maisha yao na amani ikatawale katika nyumba zao.. Ee Baba usikie na kupokea maombi/sala zetu.. Sifa na utukufu tunakurudishia Mungu wetu.. Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele.. Amina..! Asanteni sana wapendwa katika Bwana kwa kuwa nami Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea katika yote yampendezayo,Roho Mtakatifu akawaongoze na Amani ikawe nanyi daima.. Nawapenda. |
No comments:
Post a Comment