Mwaka 1989 shirika maarufu la muziki Uingereza , WOMAD, lilimtunuku Mtanzania Saidi Kanda tuzo la Mpiga Ngoma wa Kimataifa wa Mwaka duniani. Kuanzia hapo mzawa huyu wa Bagamoyo aliyezaliwa 1962, anahesabika mpiga ngoma wa nne kiufundi ulimwenguni chini ya magwiji hatari kama Airto Morreira (Brazil) na Changuito (Cuba) ...
Baada ya kusakata vituz na wanamuziki mbalimbali akiwemo marehemu Remmy Ongala, Kofi Olomide na msanii maarufu wa kimataifa, Grace Jones; leo Kanda anaongoza kikosi chake kikali cha "Mvula Mandondo" kutangaza albam yake ya kwanza, "Ambush"....
KWA SIMU TOKA LONDON inawaletea sehemu ya kwanza ya Sura Tano za mahojiano kumtathmini mtunzi huyu anayetetea (na kuhusudisha ), sana muziki wa kiasili wa Kitanzania nje na ndani ya Afrika Mashariki.
Zaidi;
No comments:
Post a Comment