Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 19 December 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;1Samueli2...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..

Mtakatifu..Mtakatifu..Mtakatifu Baba wa Mbinguni,Mungu wetu
mwenye nguvu,Baba wa upendo,Baba wa Baraka,Mungu wa walio
hai,Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Mfalme wa Amani,
Muweza wa yote,Hakuna kama wewe,Unatosha Baba wa Mbinguni
Matendo yak ni makuu sana,Matendo yako ni ya Ajabu...
Sifa na utukufu tunakurudishia Mungu wetu...
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Utukuzwe Mungu wetu,unastahili sifa,unastahili kuabudiwa,unastahili kuhimidiwa,unastahili ee Baba wa mbinguni..Unatosha Mungu wetu..!





Kutokana na hayo, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu, namwomba Mungu. Bila shaka mmekwisha sikia kwamba Mungu, kwa neema yake, alinikabidhi kazi hii niifanye kwa faida yenu. Mimi nilijulishwa kwa njia ya ufunuo mpango wake uliofichika. (Nimeandika kwa ufupi juu ya jambo hili, nanyi mkiyasoma maneno yangu mtaweza kujua jinsi ninavyoielewa siri hiyo ya Kristo). Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho. Siri yenyewe ni hii: Kwa njia ya Injili watu wa mataifa mengine wanapata sehemu yao pamoja na Wayahudi katika zile baraka za Mungu; wao ni viungo vya mwili uleule, na wanashiriki ahadi ileile aliyofanya Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.Kutokana na hayo, mimi Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu kwa ajili yenu, namwomba Mungu. Bila shaka mmekwisha sikia kwamba Mungu, kwa neema yake, alinikabidhi kazi hii niifanye kwa faida yenu. Mimi nilijulishwa kwa njia ya ufunuo mpango wake uliofichika. (Nimeandika kwa ufupi juu ya jambo hili, nanyi mkiyasoma maneno yangu mtaweza kujua jinsi ninavyoielewa siri hiyo ya Kristo). Zamani watu hawakujulishwa siri hiyo; lakini sasa Mungu amewajulisha mitume na manabii wake watakatifu kwa njia ya Roho. Siri yenyewe ni hii: Kwa njia ya Injili watu wa mataifa mengine wanapata sehemu yao pamoja na Wayahudi katika zile baraka za Mungu; wao ni viungo vya mwili uleule, na wanashiriki ahadi ileile aliyofanya Mungu kwa njia ya Kristo Yesu.




Tazama jana imepita Mungu wetu leo ni siku mpya Yahweh kesho ni siku
nyingine Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na 
kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu...
Baba wa Mbinguni tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyoyafanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Yahweh nasi 
tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah tunaomba utuepushe Katika majaribu Baba wa mbinguni utuokoe
na yule mwovu na Kazi zake zote...
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni
utufunike kwa Damu ya Bwana na mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sis tupate kupona..

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za kimono yetu..
Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa Katika ufanyaji/utendaji
Mungu wetu tukatende kama inavyokupendeza wewe..
Baba wa Mbinguni ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Baba wa Mbinguni tunaomba tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Jehovah ukatupe sawasawa na mapenzi yako...




Mwenyezi-Mungu asema; “Nilikuwa tayari kujionesha kwao wasiouliza habari zangu. Nilikuwa tayari kuwapokea wale wasionitafuta. Nililiambia taifa ambalo halikuomba kwa jina langu: ‘Nipo hapa! Nipo hapa!’ Mchana kutwa niliwanyoshea mikono watu waasi, watu ambao hufuata njia zisizo sawa, watu ambao hufuata fikira zao wenyewe. Ni watu ambao daima hunichokoza waziwazi; hutambikia miungu yao katika bustani, na kuifukizia ubani juu ya matofali. Huketi makaburini na kukaa mafichoni usiku. Hula nyama ya nguruwe na mchuzi wa wanyama haramu. Huwaambia wale wanaokutana nao: ‘Kaeni mbali nami; msinikaribie kwani mimi ni mtakatifu!’ Watu hao wananikasirisha mno, hasira yangu ni kama moto usiozimika. “Jueni kuwa nimelitia jambo hilo moyoni, sitanyamaza bali nitawafanya walipe; nitawafanya walipe kwa wingi. Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yao wayalipie na maovu ya wazee wao. Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani, wakanitukana mimi huko vilimani. Nitawafanya walipe kwa wingi, watayalipia matendo yao ya awali.” Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Mtu akikuta kishada cha zabibu nzuri, watu husema: ‘Tusikiharibu; kina baraka.’ Ndivyo nitakavyofanya kwa ajili ya watumishi wangu; sitawaangamiza wote. Nitawajalia watu wa Yakobo, na Yuda nitamjalia warithi wa milima yangu; watumishi wangu watakaa huko. Nchi tambarare ya Sharoni itakuwa malisho, bonde la Akori litakuwa mapumziko ya mifugo kwa ajili ya watu wangu walionitafuta. “Lakini nitafanya nini na nyinyi mnaoniacha mimi Mwenyezi-Mungu, msioujali Siyoni, mlima wangu mtakatifu, nyinyi mnaoabudu mungu ‘Gadi’, na kumtolea tambiko ya divai mungu ‘Meni’? Nimewapangia kifo kwa upanga, nyote mtaangukia machinjoni! Maana, nilipowaita, hamkuniitikia; niliponena, hamkunisikiliza. Mlitenda yaliyo maovu mbele yangu, mkachagua yale nisiyoyapenda. Basi, mimi Mwenyezi-Mungu nasema, watumishi wangu watakula, lakini nyinyi mtaona njaa; watumishi wangu watakunywa, lakini nyinyi mtaona kiu; watumishi wangu watafurahi, lakini nyinyi mtafedheheka. Watumishi wangu wataimba kwa furaha moyoni, lakini nyinyi mtalia kwa uchungu moyoni na kupiga kelele kwa uchungu mkubwa rohoni. Wale niliowachagua nitawapa jina jipya. Lakini nyinyi jina lenu watalitumia kulaania; ‘Watasema: Bwana Mungu awaue kama hao.’ Basi, mwenye kujitakia baraka nchini, atajitakia baraka kwa Mungu wa kweli. Mwenye kuapa katika nchi hii, ataapa kwa Mungu wa kweli. Maana taabu za zamani zimepita zimetoweka kabisa mbele yangu.

Mfalme wa amani tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Yahweh
tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Mungu wetu ukaonekane popote tupitapo Yahweh na ijulikane kwamba
upo Baba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako Jehovah ukatupe neema ya hekima,busara,utuwema,upendo na amani ikatawale..
Mungu Baba ukatuepushe na kiburi,majivuno,choyo,ubinafsi ,makwazo na yote yanayokwenda kinyume nawe...
Jehovah ukatupe neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu..
Ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Ukatufanye chombo Chema Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..


“Sasa, naumba mbingu mpya na dunia mpya. mambo ya zamani hayatakumbukwa tena. Furahini, mkashangilie milele, kwa ajili ya vitu hivi ninavyoumba. Yerusalemu nitaufanya mji wa shangwe, na watu wake watu wenye furaha. Nami nitaufurahia mji wa Yerusalemu, nitawafurahia watu wangu. Sauti ya kilio haitasikika tena, kilio cha taabu hakitakuwako. Hakutakuwa tena na vifo vya watoto wachanga, wazee nao hawatakufa kabla ya wakati wao. Akifa mtu wa miaka 100 amekufa akiwa kijana; na akifa kabla ya miaka 100 ni balaa. Watu watajenga nyumba na kuishi humo; watalima mizabibu na kula matunda yake. Hawatajenga nyumba zikaliwe na watu wengine, wala kulima chakula kiliwe na watu wengine. Maana watu wangu niliowachagua wataishi maisha marefu kama miti; wateule wangu watafurahia matunda ya jasho lao. Kazi zao hazitakuwa bure, wala hawatazaa watoto wa kupata maafa; maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu, wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao. Hata kabla hawajaniita, mimi nitawaitikia; kabla hawajamaliza kusema, nitakuwa nimewajibu. Mbwamwitu na kondoo watakula pamoja, simba watakula nyasi kama ng'ombe, nao nyoka chakula chao kitakuwa vumbi. Katika mlima wangu wote mtakatifu, hakuna atakayeumiza au kuharibu kitu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”



Yahweh tunawaweke mikononi mwako wenye shida/tabu Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaponye wagonjwa na ukawape uvumilivu wanaowauguza,
Mungu wetu tunaomba ukawape chakula wenye njaa..
Baba wa Mbinguni ukawafungue na kuwaweka huru wale walio Katika
vifungo vya yule mwovu Mungu wetu ukawatue na kuwapumzisha wale walio elemewa na mizigo.. Mungu wetu ukawaguse kwa mono wako wenye
nguvu wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Baba wa Mbinguni
ukaonekane na kuwatendea sawasawa na mapenzi yako watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani,Yahweh ukaguse matumbo ya wale wanaohitaji watoto Mungu wetu ukawape watoto walio wako,Mungu Baba
tunaomba ukapokee,ukasikie na ukatujibu sala/maombi yetu kama ivyokupendeza wewe..
kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata milele..
Amina..!

Asanteni Sana wapendwa  katika Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti
kwakuwa nami,Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea sawasawa
na mapenzi yake,Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo ikawe nayi daima..
Nawapenda.


Sala ya Hana

1Halafu Hana aliomba na kusema:
“Namshangilia Mwenyezi-Mungu moyoni mwangu.
Namtukuza Mwenyezi-Mungu aliye nguvu yangu.
Nawacheka adui zangu;
maana naufurahia ushindi wangu.
2“Hakuna aliye mtakatifu kama Mwenyezi-Mungu;
hakuna yeyote aliye kama yeye;
hakuna aliye mwamba kama Mungu wetu.
3Acheni kujisifu,
acheni kusema ufidhuli.
Maana ajuaye ni Mwenyezi-Mungu.
Yeye huyapima matendo yote.
4Pinde za wenye nguvu zimevunjika.
Lakini wadhaifu wanaendelea kupata nguvu.
5Wale ambao zamani walikuwa na chakula tele,
sasa wanaajiriwa ili wapate chakula.
Lakini waliokuwa na njaa,
sasa hawana njaa tena.
Mwanamke tasa amejifungua watoto saba.
Lakini mama mwenye watoto wengi,
sasa ameachwa bila mtoto.
6Mwenyezi-Mungu huua na hufufua;
yeye huwashusha chini kuzimu
naye huwarudisha tena.
7Mwenyezi-Mungu huwafanya baadhi wawe maskini,
na baadhi wawe matajiri.
Wengine huwashusha,
na wengine huwakweza.
8Huwainua maskini toka mavumbini;
huwanyanyua wahitaji toka majivuni,
akawaketisha pamoja na wakuu,
na kuwarithisha viti vya heshima.
Maana, minara ya dunia ni ya Mwenyezi-Mungu;
yeye ameisimika dunia juu ya minara yake.
9“Maisha ya waaminifu wake huyalinda,
lakini maisha ya waovu huyakatilia mbali gizani.
Maana, binadamu hapati ushindi kwa nguvu zake.
10Maadui wa Mwenyezi-Mungu watavunjwa vipandevipande;
atanguruma dhidi yao kama radi mbinguni.
Mwenyezi-Mungu ataihukumu dunia yote;
atampa nguvu mfalme wake
ataukuza uwezo wa mteule wake.”
11Kisha, Elkana akarudi nyumbani Rama. Lakini mtoto Samueli akabaki Shilo kumtumikia Mwenyezi-Mungu chini ya uongozi wa kuhani Eli.

Watoto wa kiume wa Eli

12Watoto wa kiume wa Eli walikuwa walaghai sana. Hawakumjali Mwenyezi-Mungu 13wala juu ya vitu ambavyo watu walipaswa kuwapa makuhani. Kila mara mtu alipokuwa anatolea tambiko yake, mtumishi wa kuhani alikuja na uma wenye meno matatu; na wakati nyama ikiwa bado inachemka, 14huyo mtumishi aliuchomeka uma huo ndani ya chungu, nyama yoyote iliyotolewa humo na uma huo, ilikuwa mali ya kuhani. Waisraeli wote waliokwenda Shilo kutolea tambiko zao walitendewa hivyo. 15Zaidi ya hayo, hata kabla mafuta hayajachomwa, mtumishi wa kuhani huja na kumwambia yule mtu anayetoa tambiko, “Mtolee kuhani nyama ya kubanika maana yeye hatapokea nyama yako iliyochemshwa, bali iliyo mbichi.” 16Na kama mtu huyo akimjibu, “Ngojea kwanza nichome mafuta halafu utachukua kiasi chochote unachotaka,” hapo huyo mtumishi wa kuhani humjibu, “La, ni lazima unipe sasa hivi. La sivyo, nitaichukua kwa nguvu.” 17Dhambi hii ya vijana hao wa Eli ilikuwa kubwa sana mbele ya Mwenyezi-Mungu. Maana, vijana hao walidharau matoleo ya Mwenyezi-Mungu.

Samueli huko Shilo

18Wakati huo, kijana Samueli aliendelea kumtumikia Mwenyezi-Mungu, akiwa amevaa kizibao cha kitani. 19Kila mwaka mama yake alimfumia vazi dogo, na kumpelekea alipokuwa akienda na mumewe kutolea tambiko ya kila mwaka. 20Eli aliwabariki Elkana na mkewe, akisema, “Mwenyezi-Mungu na akupe wewe Elkana watoto wengine kwa mwanamke huyu ili wachukue mahali pa yule uliyempa Mwenyezi-Mungu.” Kisha wao hurudi nyumbani.
21Mwenyezi-Mungu alimhurumia Hana naye akajaliwa kupata watoto wa kiume watatu na mabinti wawili. Mtoto Samueli akaendelea kukua mbele ya Mwenyezi-Mungu.

Eli na wanawe

22Wakati huo Eli alikuwa mzee sana. Aliposikia yote ambayo watoto wake wa kiume walikuwa wanawatendea Waisraeli, jinsi walivyokuwa wanalala na wanawake waliokuwa wanahudumu kwenye mlango wa hema la mkutano, 23aliwauliza, “Kwa nini mnafanya mambo haya? Nasikia kutoka kwa watu wote juu ya maovu mnayoyafanya. 24Msifanye hivyo wanangu kwa sababu mambo hayo ninayoyasikia kutoka kwa watu wa Mwenyezi-Mungu ni mabaya. 25Mtu akimkosea mwenzake, anaweza kuombewa kwa Mungu, ili Mungu amsamehe. Lakini mtu akimkosea Mwenyezi-Mungu nani awezaye kumwombea msamaha?” Lakini watoto hao hawakumsikiliza baba yao, kwani Mwenyezi-Mungu alikwisha kata shauri kuwaua.
26Mtoto Samueli aliendelea kukua, akazidi kupendwa na Mwenyezi-Mungu na watu.

Unabii dhidi ya jamaa ya Eli

27Siku moja, mtu wa Mungu alimwendea Eli, akamwambia, “Mwenyezi-Mungu amesema hivi: ‘Nilijijulisha kwa jamaa ya Aroni, wazee wako, walipokuwa watumwa wa Farao nchini Misri. 28Kati ya makabila yote ya Israeli nilimchagua Aroni na jamaa yake kuwa makuhani wangu, wanitumikie madhabahuni, wafukize ubani na kuvaa kizibao mbele yangu. Nikaipatia jamaa ya mzee wako tambiko zangu ambazo Waisraeli walinitolea kwa moto. 29Kwa nini basi, umezionea wivu tambiko na sadaka nilizowaamuru watu waniletee? Wewe umewastahi watoto wako kuliko mimi kwa kujinenepesha nyinyi wenyewe kwa kula sehemu nzurinzuri za sadaka ambazo watu wangu wa Israeli hunitolea!’ 30Kwa hiyo, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, anatamka hivi, ‘Niliahidi kwamba jamaa yako na jamaa ya wazee wako mtakuja mbele yangu kunitumikia milele;’ lakini sasa Mwenyezi-Mungu anakutangazia hivi, ‘Jambo hilo liwe mbali nami.’ Nitawaheshimu wale wanaoniheshimu, na wale wanaonidharau, nitawadharau. 31Angalia siku zaja ambapo nitawaua vijana wote wa kiume katika jamaa yako na katika ukoo wako, hata hakutakuwa na mwanamume yeyote atakayeishi awe mzee. 32Utakuwa na wasiwasi na utawaonea wenzio kijicho kwa zile baraka zote ambazo nitawapa watu wengine wa Israeli, lakini hakuna mtu katika jamaa yako atakayeishi na kuwa mzee. 33Mtu wako ambaye sitamkatilia mbali kutoka madhabahu yangu atakuwa amenusurika ili nimpofushe macho yake, naye atakufa moyo na wazawa wako watauawa kikatili.2:33 Makala ya Kiebrania si dhahiri; aya hii yaweza kusomeka: Hivyo nitabakiza mzawa wako mmoja hai, naye atanitumikia kama kuhani. Lakini atakuwa kipofu na hatakuwa na tumaini lolote; na wazawa wako wengine wote watauawa kikatili. 34Na litakalowapata watoto wako wawili wa kiume, Hofni na Finehasi, ni hili: Wote wawili watakufa siku moja. Hii itakuwa ni ishara kwako. 35Kisha, nitajiinulia kuhani mwingine mwaminifu atakayefanya kulingana na yale yaliyomo moyoni na akilini mwangu. Nitamjengea ukoo imara, naye atahudumu daima mbele ya mfalme wangu. 36Yeyote atakayebakia katika jamaa yako atamwendea kuhani huyo na kumwomba kipande cha fedha au mkate, na kumwambia, ‘Niweke, nakuomba, kwenye nafasi mojawapo ya kuhani ili niweze, angalau, kupata kipande cha mkate.’”

1Samweli2;1-36

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.


No comments: