Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumashukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu..
Mungu wetu Baba yetu, Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Baba wa Mbinguni,Muweza wa yote,Mungu wa walio hai,Mponyaji wetu..
Alfa na Omega,Baba wa baraka,Baba wa upendo,Baba wa huruma,Baba wa Yatima,Mungu mwenye nguvu,hakuna kama wewe,Emanueli-Mungu pamoja nasi..
Utukuzwe ee Mungu wetu,Uhimidiwe Baba wa Mbinguni,Usifiwe Yahweh,Uabudiwe daima Mfalme wa amani,wewe ukisema ndiyo hakuna wakupinga..
Sifa na utukufu tunakurudishia wewe Mungu wetu..
Asante kwa ulinzi wako wakati wote Mungu wetu..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuiona leo hii..
si kwa uwezo wetu wala si kwa nguvu/utashi wetu,si kwamba sis ni wema sana
si kwa akili zetu Mungu wetu ni kwa neema/rehema zako sisi kuwa hivi ni kwa mapenzi yako Baba wa Mbinguni sisi kuwa hivi tulivyo..
Utukufu una wewe Baba wa Mbinguni..
Ndugu, nataka mjue kwamba babu zetu wote walikuwa chini ya ulinzi wa lile wingu, na kwamba wote walivuka salama ile bahari. Wote walibatizwa katika umoja na Mose katika lile wingu na katika ile bahari. Wote walikula chakula kilekile cha kiroho, wakanywa pia kinywaji kilekile cha kiroho, maana walikunywa kutoka ule mwamba wa kiroho uliowafuata; mwamba huo ulikuwa Kristo mwenyewe. Hata hivyo, wengi wao hawakumpendeza Mungu, na maiti zao zilisambazwa jangwani. Sasa, mambo hayo yote ni mfano tu kwetu; yanatuonya sisi tusitamani ubaya kama wao walivyotamani. Msiwe waabudu sanamu kama baadhi yao walivyokuwa; kama yasemavyo Maandiko: “Watu waliketi kula na kunywa, wakasimama kucheza.” Wala tusizini kama baadhi yao walivyozini, wakaangamia siku moja watu 23,000. Tusimjaribu Bwana kama baadhi yao walivyomjaribu, wakauawa na nyoka. Wala msinungunike kama baadhi yao walivyonungunika, wakaangamizwa na Mwangamizi! Basi, mambo hayo yaliyowapata wao ni kielelezo kwa wengine, na yaliandikwa ili kutuonya sisi ambao mwisho wa nyakati unatukabili.
Tazama jana imepita Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine
Yahweh..!!Mfalme wa amani tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Jehovah..
Baba wa Mbinguni tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwa,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Yahweh nasi tunaomba utupe neuma ya kuweza kuwasamehe wale wote
waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh utuokoe na yule mwovu na Kazi zake zote..
Nguvu za giza,nguvu za mizimu,nguvu za mapepo,Nguvu za mpinga Kristo zishindwe katika jina lililo kuu kuliko majina yote jina la Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akilli zetu Yahweh tunaomba
utufunike kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo..
Anayedhani amesimama imara ajihadhari asianguke. Majaribu mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama. Kwa hiyo, wapenzi wangu, epeni ibada za sanamu. Naongea nanyi, watu wenye busara; jiamulieni wenyewe hayo nisemayo. Tunapomshukuru Mungu kwa kikombe kile cha baraka, je, huwa hatushiriki damu ya Kristo? Na tunapoumega mkate, je, huwa hatushiriki mwili wa Kristo? Kwa kuwa mkate huo ni mmoja, sisi, ingawa ni wengi, tu mwili mmoja; maana sote twashiriki mkate huohuo. Angalieni kwa mfano Wayahudi wenyewe: Wale wanaokula tambiko wanaungana na hiyo madhabahu. Nataka kusema nini, basi? Kwamba chakula kilichotambikiwa sanamu ni kitu zaidi ya chakula? Na hizo sanamu, je, ni kitu kweli zaidi ya sanamu? Hata kidogo! Ninachosema ni kwamba tambiko wanazotoa watu wasiomjua Mungu wanawatolea pepo, sio Mungu. Sipendi kamwe nyinyi muwe na ushirika na pepo. Hamwezi kunywa kikombe cha Bwana na kikombe cha pepo; hamwezi kushiriki katika Karamu ya Bwana na katika meza ya pepo. Au je, tunataka kumfanya Bwana awe na wivu? Mnadhani tuna nguvu zaidi kuliko yeye?
Jehovah tunaomba ukabariki Kazi za mikono yetu Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika ufanyaji/utendaji Baba wa Mbinguni tukafanye sawasawa na mapenzi yako..
Mungu wetu tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Mfalme wa Amani tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Jehovah tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..
Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki..
Jehovah tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu..
Mungu wetu ukaonekane popote tupitapo Yahweh na ijulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni,tuka nene yaliyo yako ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii,tukapate kujitambua/kutambua..
Mungu Baba ukatufanye chombo Chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Vitu vyote ni halali, lakini si vyote vinafaa. Vitu vyote ni halali lakini si vyote vinajenga. Mtu asitafute faida yake mwenyewe, ila faida ya mwenzake. Kuleni chochote kile kiuzwacho sokoni bila ya kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu; maana Maandiko yasema: “Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.” Kama mtu ambaye si mwaamini akiwaalikeni nanyi mkakubali kwenda, basi, kuleni vyote atakavyowaandalieni bila kuulizauliza kwa sababu ya dhamiri zenu. Lakini mtu akiwaambieni: “Chakula hiki kimetambikiwa sanamu,” basi, kwa ajili ya huyo aliyewaambieni hivyo na kwa ajili ya dhamiri, msile. Nasema, “kwa ajili ya dhamiri,” si dhamiri yenu, bali dhamiri yake huyo aliyewaambieni. Mtaniuliza: “Kwa nini uhuru wangu utegemee dhamiri ya mtu mwingine? Ikiwa mimi nashiriki chakula hicho huku namshukuru Mungu, kwa nini nilaumiwe kwa chakula ambacho kwa ajili yake nimemshukuru Mungu?” Basi, chochote mfanyacho iwe ni kula au kunywa, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. Msiwe kikwazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki au kwa kanisa la Mungu. Muwe kama mimi; najaribu kuwapendeza wote kwa kila njia, bila kutafuta faida yangu mwenyewe ila faida ya wote, wapate kuokolewa.
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mono wako wenye nguvu wenye shida/tabu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaponye wagonjwa na ukawape uvumili wale wanao uguza,Yahweh ukawavushe salama wale wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,Mungu wetu ukawe tumaini kwa wale waliokata tamaa,waliokataliwa,wenye hofu na mashaka..
Yahweh tunaomba ukawaweke huru wale wailio Katika vifungo vya yule mwovu
Mungu wetu ukawatete walio magerezani pasipo na hatia Mungu wetu haki ikatendeke..Jeohovah ukawasamehe wale wote waliokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yao,Nuru ikaangane,wakawe salama moyoni na ukawape neema ya kujiombea kufuata njia zako nazo zikawaweke huru..
Baba wa Mbinguni tunaomba ukasikie kulia kwao na ukafute machozi ya watoto wako wanaokutafuta,kukuomba kwa bidii na imani..
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami..
Mungu Baba aendelee kuwabariki,Roho Mtakatifu akawaongoze
mkawe salama moyoni na mkono wa Mungu ukawaguse katika yote mfanyayo,Mungu wetu akawatendee sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.
|
No comments:
Post a Comment