Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu kwa wema na fadhili zake kwetu...
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu,Muumba Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyopo vinavyoonekana na visivyo onekana Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Baba wa Upendo,Baba wa Baraka Mungu wenye nguvu,Mungu wa walio hai,Muweza wa yote,Alfa na Omega Unastahili sifa Baba wa Mbinguni,Unastahili kuabudiwa Jehovah,Unastahili kuhimidiwa Yahweh..Unatosha Baba wa Mbinguni...!!
Unijulishe njia zako, ee Mwenyezi-Mungu; unifundishe nifuate unayotaka. Uniongoze katika ukweli wako na kunifundisha, kwani wewe ni Mungu, mwokozi wangu; ninakutegemea wewe kila siku. Uikumbuke huruma yako ee Mwenyezi-Mungu; uzikumbuke na fadhili zako kuu, ambazo zimekuwako tangu kale. Usikumbuke dhambi na makosa ya ujana wangu; unikumbuke kadiri ya fadhili zako, kwa ajili ya wema wako, ee Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu ni mwema na mnyofu, kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia. Huwaongoza wanyenyekevu katika uadilifu; naam, huwafundisha hao njia yake. Mwenyezi-Mungu hutenda kwa fadhili na uaminifu, kwa wale wanaoshika agano lake na maamuzi yake.
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote.. Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu.. Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Mungu Baba..!!
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote walio tukosea.. Mfalme wa amani tunaomba utuepushe katika majaribu Baba wa Mbinguni tunaomba utuokoe na yule mwovu na Kazi zake zote.. Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Yahweh tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti.. yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Basi, Myahudi ana nini zaidi kuliko watu wengine? Au kutahiriwa kuna faida gani? Naam, iko faida kwa kila upande. Kwanza, Mungu aliwakabidhi Wayahudi ujumbe wake. Lakini itakuwaje iwapo baadhi yao hawakuwa waaminifu? Je, jambo hilo litaondoa uaminifu wa Mungu? Hata kidogo! Mungu hubaki mwaminifu daima, ingawaje kila binadamu ni mwongo. Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Kila usemapo, maneno yako ni ya kweli; na katika hukumu, wewe hushinda.” Lakini, ikiwa uovu wetu unathibitisha kwamba Mungu anatenda kwa haki, tutasema nini? Je, tutasema kwamba anakosa haki akituadhibu? (Hapa naongea kibinadamu). Hata kidogo! Ingekuwa hivyo, Mungu angewezaje kuuhukumu ulimwengu? Labda utasema: “Ikiwa ukosefu wa uaminifu kwa upande wangu unamdhihirisha Mungu kuwa mwaminifu zaidi na hivyo kumpatia utukufu, basi singepaswa kuhukumiwa kuwa mwenye dhambi!” Ni sawa na kusema: Tufanye maovu ili tupate mema! Ndivyo wengine walivyotukashifu kwa kutushtaki kwamba tumefundisha hivyo. Watahukumiwa wanavyostahili!
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa Katika ufanyaji/utendaji Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika nyumba/ndoa zetu watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Baba wa Mbinguni ukatubariki na mkono wako wenye nguvu ukatuguse... Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki.. Mungu Baba tunaomba ukatupe macho ya rohoni,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii,tukawe salama moyoni na ukatupe neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako,Yahweh tuka nene yaliyo yako.. Mungu wetu ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe.. Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Tuseme nini, basi? Je, sisi Wayahudi ni bora kuliko wengine? Hata kidogo! Kwa maana nimekwisha bainisha hapo mwanzoni kwamba Wayahudi na watu wa mataifa mengine wote wako chini ya utawala wa dhambi. Kama Maandiko Matakatifu yasemavyo: “Hakuna hata mmoja aliye mwadilifu! Hakuna mtu anayeelewa, wala anayemtafuta Mungu. Wote wamepotoka wote wamekosa; hakuna atendaye mema, hakuna hata mmoja. Makoo yao ni kama kaburi wazi, ndimi zao zimejaa udanganyifu, midomoni mwao mwatoka maneno yenye sumu kama ya nyoka. Vinywa vyao vimejaa laana chungu. Miguu yao iko mbioni kumwaga damu, popote waendapo husababisha maafa na mateso; njia ya amani hawaijui. Hawajali kabisa kumcha Mungu.” Tunajua kwamba sheria huwahusu walio chini ya sheria hiyo, hata hawawezi kuwa na kisingizio chochote, na ulimwengu wote uko chini ya hukumu ya Mungu. Maana hakuna binadamu yeyote anayekubaliwa kuwa mwadilifu mbele yake Mungu kwa kushika sheria; kazi ya sheria ni kumwonesha tu mtu kwamba ametenda dhambi.
Yahweh tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu wenye shida/tabu Mungu wetu tunaomba ukawavushe salama wale wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali... Mungu wetu tunaomba ukawaponye wagonjwa Yahweh ukawape uvumilivu na nguvu wale wanaowauguza.. Jehovah tunaomba ukawape chakula wenye njaa Yahweh ukawe tumaini kwa walio kata tamaa,waliokataliwa,wenye hofu na mashaka Baba wa Mbinguni ukawasamehe wale wote walikwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawe faraja kwa waliofiwa Yahweh ukawape neema ya kujiombea kufuata njia zako na Nuru yako ikaangaze katika maisha yao.. Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako.. Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na utukufu hata Milele.. Amina..!
Asanteni sana Wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami.. Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea sawasawa na mapenzi yake Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo ikatawale katika maisha yenu.. Nawapenda.
|
No comments:
Post a Comment