Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 26 December 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;1Samueli7...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote..

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuiona leo hii..

Utukuzwe Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Jehovah,
Uabudiwe Yahweh,Unatosha Mungu wetu,Hakuna kama wewe..!



Nitamtukuza Mwenyezi-Mungu nyakati zote, sitaacha kamwe kuzitamka sifa zake. Mimi nitaona fahari juu ya Mwenyezi-Mungu, wanyonge wasikie na kufurahi. Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu pamoja nami, sote pamoja tulisifu jina lake. Nilimwomba Mwenyezi-Mungu naye akanijibu, na kuniondoa katika hofu zangu zote. Mgeukieni Mungu mpate kufurahi; nanyi hamtaaibishwa kamwe. Maskini alimlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamsikia, na kumwokoa katika taabu zake zote. Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao, na kuwaokoa katika hatari. Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema. Heri mtu anayekimbilia usalama kwake. Mcheni Mwenyezi-Mungu enyi watakatifu wake; maana wenye kumcha hawatindikiwi na kitu. Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa; lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema. Njoni enyi vijana mkanisikilize, nami nitawafundisha kumcha Mwenyezi-Mungu. Je, watamani kufurahia maisha, kuishi maisha marefu na kufurahia mema? Basi, acha kusema mabaya, na kuepa kusema uongo. Jiepushe na uovu, utende mema; utafute amani na kuizingatia.


Tazama jana imepita Baba wa Mbinguni leo ni siku mpya na kesho ni  situ nyingine..
Mfalme wa amani tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako..
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya 
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
 wale wote waliotukosea..
Yahweh tunaomba utuepushe katika majaribu Mungu Baba utuokoe na yule mwovu na Kazi zake zote..
Nguvu za giza,nguvu za mapepo,nguvu za mizimu,nguvu za mpinga Kristo zishindwe katika jina lililokuu  jina la Bwana wetu Yesu Kristo wa Nazareti..
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni
utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo..
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..


Nitalihifadhi agizo hilo na kulifunga fundisho hilo miongoni mwa wafuasi wangu. Nitamngojea Mwenyezi-Mungu ambaye amejificha mbali na wazawa wa Yakobo; nitamtumainia. Mimi pamoja na watoto alionipa Mwenyezi-Mungu ni ishara na alama katika Israeli kwa jina la Mwenyezi-Mungu wa majeshi akaaye mlimani Siyoni. Baadhi watawaambieni: “Nendeni mkatake shauri kwa mizimu na mizuka iliayo kama ndege; kwani ni kawaida watu kutaka shauri kwa miungu yao, na kutaka shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai.” Hakika anayesema hivyo hajapata kuona mwanga. Lakini nyinyi shikilieni lile agizo na fundisho la Mungu.

Mungu baba tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa Katika ufanyaji/utendaji
Mungu wetu tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye
kuhitaji..

Mfalme wa Amani tunaomba amani yako ikatawale katika nyumba/ndoa zetu,Mungu wetu tunaomba ukabariki watoto,wazazi wetu,familia/ndugu
na wote wanaotuzunguka..
yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Jehovah ukatamalaki na kutuatamia,Mungu Baba tukawe salama moyoni
ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Mungu wetu ukatupe neema ya kufuata njia zako,Yahweh kusimamia
Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu..
Baba wa Mbinguni ukatuoke na kiburi,chuki,majivuno,makwazo,
unafiki na nyote vinavyokwenda kinyume nawe..
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu,Nuru yako
ikaangaze,Upendo ukadumu kati yetu, ukaonekane popote tupitapo 
na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni..
Ukatufanye chombo Chema Yahweh  nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..



Nitamtukuza Mwenyezi-Mungu nyakati zote, sitaacha kamwe kuzitamka sifa zake. Mimi nitaona fahari juu ya Mwenyezi-Mungu, wanyonge wasikie na kufurahi. Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu pamoja nami, sote pamoja tulisifu jina lake. Nilimwomba Mwenyezi-Mungu naye akanijibu, na kuniondoa katika hofu zangu zote. Mgeukieni Mungu mpate kufurahi; nanyi hamtaaibishwa kamwe. Maskini alimlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamsikia, na kumwokoa katika taabu zake zote. Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao, na kuwaokoa katika hatari. Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema. Heri mtu anayekimbilia usalama kwake. Mcheni Mwenyezi-Mungu enyi watakatifu wake; maana wenye kumcha hawatindikiwi na kitu. Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa; lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema. Njoni enyi vijana mkanisikilize, nami nitawafundisha kumcha Mwenyezi-Mungu. Je, watamani kufurahia maisha, kuishi maisha marefu na kufurahia mema? Basi, acha kusema mabaya, na kuepa kusema uongo. Jiepushe na uovu, utende mema; utafute amani na kuizingatia.
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
wenye shida/tabu,Mungu wetu ukawavushe salama wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,Mfalme wa amani amani yako ikatawale
kwa walio na uchungu moyoni,walioumizwa,walio na hasira na wenye kusononeka..
Yahweh tunaomba ukawaponye wagonjwa na unawape uvumili/nguvu wanaowauguza..
Jehovah ukabariki mashamba/kazi zoo na ukawape chakula cha kutosha wenye njaa na wapate kuweka akiba..
Mungu Baba ukawatue na kuwapumzisha wale waliolemewa na mizigo
Yahweh ukawe tumaini kwa wote waliokata tamaa,waliokataliwa,wenye
hofu na mashaka..
Mungu wetu ukawasamehe wale wote waliokwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yao..
Baba wa mbinguni ukaguse matumbo ya wanaotafuta watoto,Mungu wetu ukawape watoto walio wako,Yahweh ukasikie kilio cha watoto wako
Mungu wetu uwafute machozi na ukawape sawasawa na mapenzi yako wote wanaokuomba kwa bidii na imani..
Ee Baba ukasikie,ukapokee,ukajibu maombi/sala zetu..
Kwakuwa ufalne ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni Sana wapendwa katika kristo Yesu kwakuwa nami
Baba wa upendo akawatendee sawasawa na mapenzi yake
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo ikawe nanyi Daima..
Nawapenda.




1Kisha, watu wa Kiriath-yearimu wakaenda na kulichukua sanduku la Mwenyezi-Mungu, wakalipeleka nyumbani kwa Abinadabu, aliyeishi milimani. Wakamweka wakfu mtoto wake wa kiume aliyeitwa Eleazari ili alitunze sanduku hilo.
Samueli anatawala Israeli
2Tangu sanduku la Mwenyezi-Mungu lipelekwe mjini Kiriath-yearimu muda mrefu ulipita, miaka ishirini hivi. Wakati huo Waisraeli wote walimlilia Mwenyezi-Mungu.
3Samueli akawaambia Waisraeli, “Kama mnamrudia Mwenyezi-Mungu kwa moyo wenu wote, ni lazima mwondoe kati yenu miungu ya kigeni na sanamu za Ashtarothi. Mwelekeeni Mwenyezi-Mungu kwa moyo wote, na kumtumikia yeye peke yake; naye atawaokoa kutoka mikononi mwa Wafilisti.” 4Hivyo, Waisraeli wakatupilia mbali sanamu za Mabaali na Maashtarothi, wakamtumikia Mwenyezi-Mungu peke yake.
5Kisha, Samueli akawaita Waisraeli wote wakutane huko Mizpa, akawaambia, “Huko nitamwomba Mwenyezi-Mungu kwa ajili yenu.” 6Hivyo, Waisraeli wote wakakusanyika huko Mizpa. Walichota maji na kuyamimina mbele ya Mwenyezi-Mungu, wakafunga siku ile yote na kusema, “Tumetenda dhambi mbele ya Mwenyezi-Mungu.” (Samueli alikuwa mwamuzi wa Waisraeli huko Mizpa).
7Wafilisti waliposikia kuwa Waisraeli wamekusanyika huko Mizpa, wakuu watano wa Wafilisti wakaenda kuwashambulia. Waisraeli waliposikia juu ya jambo hilo waliwaogopa Wafilisti. 8Basi, wakamwambia Samueli, “Usiache kumlilia Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, kwa ajili yetu. Endelea kumlilia atuokoe kutoka kwa Wafilisti.” 9Kwa hiyo Samueli alichukua mwanakondoo anayenyonya akamtolea Mwenyezi-Mungu kama sadaka ya kuteketezwa nzima. Kisha Samueli akamlilia Mwenyezi-Mungu kwa ajili ya Israeli, naye akajibu kilio chake. 10Samueli alipokuwa anatoa ile sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti walikaribia kuwashambulia Waisraeli. Lakini Mwenyezi-Mungu akatoa sauti kubwa ya ngurumo dhidi ya Wafilisti, na kuwavuruga Wafilisti, nao wakatimuliwa mbele ya Waisraeli. 11Waisraeli walitoka Mizpa na kuwafuatilia Wafilisti mpaka karibu na mji wa Beth-kari, wakawaangamiza.
12Kisha, Samueli alichukua jiwe na kulisimamisha kati ya Mizpa na Sheni, akaliita jiwe hilo Ebenezeri7:12 Ebenezeri: Maana yake: Jiwe la msaada. akisema, “Mwenyezi-Mungu ametusaidia mpaka sasa.” 13Siku hiyo Wafilisti walishindwa; na Mwenyezi-Mungu aliwazuia Wafilisti kuivamia nchi ya Israeli wakati wote Samueli alipokuwa hai. 14Miji yote ya Waisraeli ambayo Wafilisti waliiteka kati ya Ekroni na Gathi ilirudishiwa Waisraeli, nao walikomboa nchi yao kutoka kwa Wafilisti. Tena kulikuwa na amani kati ya Waisraeli na Waamori.
15Samueli alikuwa mwamuzi wa Israeli maisha yake yote. 16Kila mwaka Samueli alitembelea Betheli, Gilgali na Mizpa, na kuwaamua Waisraeli katika miji hiyo yote.
17Kisha, alikuwa akirudi Rama, maana huko kulikuwa nyumbani kwake; aliwaamulia Waisraeli haki zao huko, na kumjengea Mwenyezi-Mungu madhabahu huko.



1Samweli7;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: