Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 27 December 2017

Kikombe Cha Asubuhi ;1Samueli8...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Mungu wetu yu mwema sana tumshukuru kwa kila jambo..
Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako  kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu..
Asante kwakutuchagua tena na kutupa kibali cha kuiona leo hii...
Utukuzwe Mungu wetu,Wewe ni Alfa na Omega,hakuna kama wewe
Mungu mwenye nguvu,Baba wa upendo,Mungu mwenye huruma,
Mponyaji wetu,kimbilio letu,Baba wa Baraka,Mungu wa wajane..
Mungu wa Yatima,Mungu wa walio hai,Mfalme wa amani..
Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Unatosha Baba wa Mbinguni..!!


Nilimngojea Mwenyezi-Mungu kwa uvumilivu, akanielekea na kukisikia kilio changu. Aliniondoa katika shimo la hatari, alinitoa katika matope ya dimbwi, akanisimamisha salama juu ya mwamba, na kuziimarisha hatua zangu. Alinifundisha wimbo mpya, wimbo wa sifa kwa Mungu wetu. Wengi wataona na kuogopa, na kumtumainia Mwenyezi-Mungu. Heri mtu anayemtumainia Mwenyezi-Mungu; mtu asiyejiunga na watu wenye majivuno, watu waliopotoka kwa kuabudu miungu ya uongo. Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umetufanyia mengi ya ajabu, na mipango yako juu yetu haihesabiki; hakuna yeyote aliye kama wewe. Kama ningeweza kusimulia hayo yote, idadi yake ingenishinda. Wewe hutaki tambiko wala sadaka, tambiko za kuteketeza wala za kuondoa dhambi; lakini umenipa masikio nikusikie. Ndipo niliposema: “Niko tayari; ninayotakiwa kufanya yameandikwa katika kitabu cha sheria; kutimiza matakwa yako, ee Mungu wangu ni furaha yangu, sheria yako naishika kwa moyo wangu wote!” Nimesimulia habari njema za ukombozi, mbele ya kusanyiko kubwa la watu. Kama ujuavyo ee Mwenyezi-Mungu, mimi sikujizuia kuitangaza. Sikuuficha moyoni mwangu ukombozi ulionijalia, nimetangaza daima kuwa wewe ni mwokozi mwaminifu; sikulificha kusanyiko kubwa la watu fadhili zako na uaminifu wako. Ee Mwenyezi-Mungu, usininyime huruma yako! Fadhili zako na uaminifu wako vinihifadhi daima.
Tunakuja mbele zako Mungu wetu tukijinyenyekeza,tukishusha na 
kujiachilia mikononi mwako Jehovah..
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote
waliotukosea..
Baba wa Mbinguni tunaomba utuepushe katika majaribu
Yahweh tunaomba utuokoe na yule mwovu na Kazi zake zote..
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na kili zetu Baba wa Mbinguni
utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..


Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, ninaotamani sana kuwaoneni, nyinyi mlio furaha yangu na taji ya ushindi wangu, ndivyo basi mnavyopaswa kukaa imara katika kuungana na Bwana, enyi wapenzi wangu. Euodia na Suntike, nawaombeni na kuwasihi mpatane kama ndugu katika Bwana. Nawe ndugu yangu mwaminifu, nakutaka uwasaidie akina mama hao, kwani wamefanya kazi ya kueneza Injili kwa bidii pamoja nami na Klementi na wafanyakazi wenzangu wengine wote ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uhai. Basi, furahini daima katika kuungana na Bwana! Nasema tena: Furahini! Upole wenu ujulikane kwa watu wote. Bwana yu karibu.

Jehovah tunaomba ukabariki Kazi za mikono yetu Yahweh ukatupe 
ubunifu na maarifa Katika ufanyaji/utendaji Mungu wetu nasi
tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe Katika mahitaji yetu Mungu Baba ukatupe kama inavyokupendeza wewe..

Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu
familia/ndugu na wote wanaotuzunguka..
Yahweh tunaomba ulinzi wake kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki..
Baba wa Mbinguni ukatamalaki na kutuatamia,Mungu wetu ukatupe
neema ya kufuata njia zako Baba wa Mbinguni tukasimamei Neno lako
amri na Sheria zoko siKu zote za maisha yetu..
Mungu wetu neema yako yatutosha,upendo una wewe,amani iko nawe,
baraka zina wewe,Baba wa Mbunguni Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukaonekane popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Baba wa Mbinguni
Ukatufanye combo Chema Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..



Katika kuungana na Bwana nimepata furaha kubwa kwamba mwishoni mlipata tena fursa ya kuonesha kwamba mnanikumbuka. Kusema kweli mmekuwa mkinikumbuka daima ila tu hamkupata nafasi ya kuonesha jambo hilo. Sisemi hivyo sasa kwa sababu nahitaji kitu; maana nimejifunza kuridhika na vitu nilivyo navyo. Najua hali ya kutokuwa na vitu na hali ya kuwa na vingi. Nimejizoeza kuridhika katika kila hali na mahali; niwe nina cha kutosha au nina njaa; iwe nina ziada au nimepungukiwa. Naweza kuikabili kila hali kwani Kristo hunipa nguvu. Hata hivyo, nyinyi mlifanya vema kwa kushirikiana nami katika taabu zangu. Nyinyi Wafilipi mwafahamu wenyewe kwamba mwanzoni mwa kuhubiri Habari Njema, nilipokuwa naondoka Makedonia, nyinyi peke yenu ndio kanisa lililonisaidia; nyinyi peke yenu ndio mlioshirikiana nami katika kupokea na kuwapa wengine mahitaji. Nilipokuwa nahitaji msaada kule Thesalonike mliniletea, tena zaidi ya mara moja. Sio kwamba napenda tu kupokea zawadi; ninachotaka ni faida iongezwe katika hazina yenu. Basi, nimekwisha pokea vitu vyote mlivyonipa, tena ni zaidi kuliko nilivyohitaji. Nina kila kitu kwa vile sasa Epafrodito amekwisha niletea zawadi zenu. Zawadi hizi ni kama tambiko yenye harufu nzuri, sadaka inayokubaliwa na kumpendeza Mungu. Basi, Mungu wangu, kwa utajiri wake mkuu kwa njia ya Kristo, atawapeni mahitaji yenu yote.

Mungu wetu tunarudisha shukrani kwa uponyaji wako,Yahweh umekuwa msaada
kwetu Katika Mapito yetu,Mungu wetu umetutendea na kutubariki,Yahweh umeonekana katika shida/tabu zetu Baba wa Mbinguni utukuzwe milele na milele

Yahweh usiwapite na wengine wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Yahweh ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu,Mungu wetu ukawaponye
wagonjwa na wanaowauguza unawape uvumilivu na nguvu..
Jehovah ukawe tumaini kwa wote waliokata tamaa,waliokataliwa,wenye hofu na mashaka,Yahweh ukawape chakula wenye njaa,Mungu wetu ukawatendee
wajane na Yatima,Mungu wetu ukawafungue walio katika vifungo vya yule mwovu
Mungu wetu ukawaweke huru na haki ikatendeke kwa walio magerezani pasipo na hatia,Jehovah ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako,amani ikae nao
wakawe salama moyoni,ukawasamehe wale wote waliokwenda kinyume nawe
Baba wa mbinguni ukaonekane kwenye shida zao,Mungu wetu ukasikie kuomba kwetu,Mungu Baba ukapokee sala/maombi yetu,Yahweh ukajibu na ukawatendee
sawasawa na mapezni yako..
Sifa na Utukufu una wewe Baba wa mbinguni..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na utukufu hata Milele..
Amina..!

Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami..
Upendo wenu si bure,pendo lenu likadumu,Mungu aendelee kuwatendea
na kuwabariki,Baba wa mbinguni akawape sawasawa na mapenzi yake..
Amani ya kristo Yesu ukase nanyi Daima..
Nawapenda.




Waisraeli wanaomba wawe na mfalme

1Samueli alipokuwa mzee, aliwafanya watoto wake wa kiume kuwa waamuzi wa Israeli. 2Mtoto wake wa kwanza wa kiume aliitwa Yoeli, na wa pili aliitwa Abiya. Wote wawili walikuwa waamuzi huko Beer-sheba. 3Lakini watoto hao hawakufuata mwenendo wa baba yao. Bali walianza kujitafutia faida. Wakapokea rushwa na kupotosha haki.
4Basi, viongozi wote wa Israeli walikusanyika pamoja, na kumwendea Samueli mjini Rama, 5wakamwambia, “Tazama, wewe sasa ni mzee na watoto wako hawafuati mwenendo wako. Hivyo, tuteulie mfalme wa kututawala kama yalivyo mataifa mengine.” 6Lakini jambo la Waisraeli kutaka wapewe mfalme wa kuwatawala, halikumpendeza Samueli. Naye akamwomba Mwenyezi-Mungu. 7Mwenyezi-Mungu akamwambia, “Sikiliza kila kitu ambacho watu wanakuambia; maana hawajakukataa wewe, bali wamenikataa mimi kuwa mfalme juu yao. 8Tangu nilipowatoa Misri, wameniacha mimi, wamekuwa wakiitumikia miungu mingine mpaka leo. Sasa hayo matendo ambayo wamekuwa wakinitendea mimi,8:8 wakinitendea mimi: Haya hayapo katika makala ya Kiebrania. ndiyo wanayokutendea na wewe. 9Basi, wasikilize, lakini, waonye vikali, na waeleze waziwazi jinsi mfalme atakayewatawala atakavyowatendea.”
10Kwa hiyo, Samueli akawaambia wale watu waliokuwa wanaomba wapewe mfalme maneno yote ya Mwenyezi-Mungu. 11Samueli aliwaambia, “Hivi ndivyo mfalme wenu atakayewatawala atakavyowatendea: Watoto wenu wa kiume atawafanya wawe waendeshaji wa magari yake, na wengine kuwa wapandafarasi wake, na wengine watapiga mbio mbele ya magari yake. 12Atajichagulia wengine wawe makamanda wa vikosi vyake vya maelfu na wengine wawe makamanda wa vikosi vya watu hamsinihamsini. Atawafanya wengine wamlimie mashamba yake na kuvuna mazao yake. Atawafanya wengine pia wamtengenezee zana za vita, na wengine wamtengenezee vipuli vya magari yake. 13Binti zenu atawachukua kuwa watengenezaji marashi, wengine wapishi na wengine waokaji mikate. 14Atayachukua mashamba yenu mazuri, mashamba ya mizeituni, na mashamba ya mizabibu na kuwapa watumishi wake. 15Atachukua sehemu ya kumi ya nafaka zenu na ya zabibu zenu na kuwapa maofisa wake na watumishi wake. 16Atachukua watumishi wenu wa kiume na wa kike na ng'ombe wenu8:16 ng'ombe wenu: Makala ya Kiebrania: Vijana wa kiume. wazuri na punda wenu wazuri kabisa na kuwafanya wamfanyie kazi zake. 17Atachukua sehemu ya kumi ya kondoo wenu. Na nyinyi wenyewe mtakuwa watumwa wake. 18Wakati huo, nyinyi mtalalamika kwa sababu ya mfalme wenu ambaye mmejichagulia nyinyi wenyewe. Lakini Mwenyezi-Mungu hatawajibu.”
19Hata hivyo watu walikataa kumsikiliza Samueli, wakasema, “La! Sisi tutakuwa na mfalme juu yetu, 20ili nasi pia tuwe kama mataifa mengine. Mfalme wetu, atatuhukumu, atatuongoza na kutupigania vita vyetu.”
21Samueli alipokwisha sikiliza kila kitu walichosema, akaenda na kumweleza Mwenyezi-Mungu. 22Mwenyezi-Mungu akamwambia Samueli, “Wasikilize na wapatie mfalme.” Kisha Samueli akawaambia Waisraeli warudi nyumbani, kila mtu mjini kwake.


1Samweli8;1-22

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

2 comments:

Anonymous said...

Awesome post.

Anonymous said...

Hi colleagues, its fantastic post regarding cultureand fully explained,
keep it up all the time.