Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana tumshukuru katika yote..
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi..
Muumba wa vyote vinavyoonekana na visivyoonekana..
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Mungu wa Wajane,Baba wa Yatima
Baba wa Upendo,Baba wa Baraka,Baba wa Uzima,Mungu mwenye nguvu
Mungu wa wote walio hai....
Utukuzwe Mungu wetu,Usifiwe Jehovah,Uhimidiwe Baba wa Mbinguni,Uabudiwe daima,Matendo yako ji makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu,Hkuna kama wewe ee Mungu wetu...
Unatosha Baba wa Mbinguni...!
Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba yetu na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Asante kwa wema na fadhili zako Mungu wetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe Baba wa Mbinguni...!!
Mfalme wa Amani tazama jana imepita Mungu wetu Leo ni siku mpya Baba wa Mbinguni Kesho ni siku nyingine...
Jehova tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Ee Mungu wetu..
Baba tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyoyafanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea..
Yahweh tunaomba utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu Baba wa Mbinguni utufunike
kwa Damu ya mwanao mpendwa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo
wa Nazareti yeye aliseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Ndugu, tunapaswa kumshukuru Mungu daima kwa ajili yenu. Inafaa kwetu kufanya hivyo kwani imani yenu inakua sana na kupendana kwenu kunaongezeka sana. Ndio maana sisi tunajivunia nyinyi katika makanisa ya Mungu. Tunaona fahari juu ya jinsi mnavyoendelea kuamini na kustahimili katika udhalimu wote na mateso mnayopata. Hayo yote yanathibitisha kwamba hukumu ya Mungu ni ya haki, na matokeo yake, nyinyi mtastahili ufalme wake ambao kwa ajili yake mnateseka. Mungu atafanya jambo la haki: Atawalipa mateso wale wanaowatesa nyinyi na kuwapeni nafuu nyinyi mnaoteseka, na sisi pia. Atafanya jambo hilo wakati Bwana atakapotokea kutoka mbinguni pamoja na malaika wake wenye nguvu na miali ya moto, kuwaadhibu wale wanaomkataa Mungu na wale wasiotii Habari Njema ya Bwana wetu Yesu. Adhabu yao itakuwa kuangamizwa milele na kutengwa mbali na utukufu wake mkuu, wakati atakapokuja siku ile kupokea utukufu kutoka kwa watu wake na heshima kutoka kwa wote wanaoamini. Nyinyi pia mtakuwa miongoni mwao, kwani mmeuamini ule ujumbe tuliowaletea.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Yahweh tunaomba
utupe ubunifu,maarifa katika ufanyaji/utendaji Baba wa Mbinguni
nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako..
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu Yahweh tunaomba ukatupe sawasawa na mapenzi yako..
Mfalme wa Amani tunayaweka maisha yetu mikononi mwako ...
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu
familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Baba wa Mbinguni tunaomba
amani yako ikatawale maishani mwetu,Baba wa Mbinguni ukatuguse
kwa mkono wako wenye nguvu Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu
na kwa vyote tunavyovimiliki,Mungu wetu tunaomba ukatamalaki,
utuatamie na ukaonekane popote tulipo/tupitapo na ijulikane
kwamba upo Baba wa Mbinguni,tukanene yaliyo yako,tupate kujitambua/kutambua,ukatupe neema ya kufuata njia zako,
tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii.
ukatuepushe na yote yanayokwenda kinyume nawe Ee Baba
tunaomba Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu..
Ukatufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza
wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ndiyo maana tunawaombeeni daima. Tunamwomba Mungu wetu awawezesheni kustahili maisha aliyowaitia muyaishi. Tunamwomba, kwa uwezo wake, atimize nia yenu ya kutenda mema na kukamilisha kazi yenu ya imani. Kwa namna hiyo, jina la Bwana wetu Yesu litapata utukufu kutoka kwenu, nanyi mtapata utukufu kutoka kwake kwa neema ya Mungu wetu na ya Bwana Yesu Kristo.
Tazama wenye shida/tabu Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu,Yahweh tunaomba ukawaponye wagonjwa Jehovah
ukawape amani,uvumilivu,nguvu na moyo wote wanaouguza,Mungu wetu
tunaomba ukawape chakula wenye njaa Baba wa Mbinguni tunaomba ukawavushe salama wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Yahweh tunaomba ukawaokoe na kuwaweka huru walio katika vifungo
vya yule mwovu Mungu wetu ukawatendee walio magerezani pasipo
na hatia na haki ikatendeke,Baba wa Mbinguni ukawasamehe na kuwakumbatia tena wale waliokwenda kinyume nawe na wakatubu..
Baba wa Mbinguni ukawaongoze na ukawape ufahamu wale wote
wasio amini Mungu wetu ukawape tumaini wale walio kata tamaa,
wenye hofu na mashaka,walio kataliwa,Baba wa Mbinguni ukawafariji wafiwa,Mungu wetu tunaomba ukasikie,ukapokee na ukajibu sala/maombi yetu...
Jehovah ukaonekane na ukawatendee sawasawa na mapenzi yako wote wanaokuomba/kukutafuta kwa bidii na imani...
Ee Mungu wetu utusikie...!
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina...!
Asante sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami..
Mungu Baba akawabariki na kuwapa kile kilicho chema
Msipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni akawape
sawasawa na mapenzi yake,Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na
utukufu wa Mungu Baba ukawe nanyi daima..
Nawapenda. |
No comments:
Post a Comment