Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote..
Mtakatifu Baba wa Mbinguni,Mungu wetu,Muumba wetu,
Muumba wa nchi na Mbingu,Mungu wa Abarahamu,Isaka na Yakobo
Baba wa Upendo,Mungu mwenye nguvu,Baba wa Yatima,Mume wa
wajane,Baba wa baraka,Muweza wa yote,Alfa na Omega,Hakuna
kama wewe,unatosha Mungu wetu...
Unastahili sifa,unasthahili kuabudiwa,unasthahili kuhimidiwa
Utukufu ni wako Mungu wetu..!!
Mfalme wa amani tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,
tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Yahweh..
Baba wa Mbinguni tunaomba utusamehe makosa yetu yote
tuliyoyafanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale
wote waliotukosea..
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu Yahweh tunaomba
utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote..
Jehovah tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Yahweh utufunike
kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu,maarifa katika
ufanyaji/utendaji Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Yahweh
nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Mungu wetu tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba ukatupe
kama inavyokupendeza wewe..
Mfalme wa Amani tuyaweka maisha yetu mikononi mwako
Yahweh tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi
wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka...
Mungu wetu tunaomba ulinzi wako kwetu na kwavyote tunavyo
vimiliki,Baba wa Mbinguni tunaomba ukatamalaki na kutuatamia..Yahweh ukatupe neema ya kufuata njia zako,kusimamia Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu..
Baba ukatupe neema ya kusaidiana,kuchukuliana,kusameheana,utu wema
fadhili,upendo wa kweli,kuhurumiana na yote yanayokupendeza wewe..
Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu,Amani ikatawale,furaha na
shangwe zisipungue,Mungu wetu ukaonekane popote tupitapo na tukanene
yaliyo yako..
Kwa hiyo, ndugu zangu, maadamu Mungu ni mwenye huruma nyingi, nawasihi kwa moyo wote: Mtoleeni Mungu miili yenu kama tambiko iliyo hai, takatifu na yenye kupendeza. Hii ndiyo njia yenu halisi ya kumwabudu. Msiige mitindo ya ulimwengu huu, bali Mungu afanye mabadiliko ndani yenu kwa kuzigeuza fikira zenu. Hapo ndipo mtakapoweza kuyajua mapenzi ya Mungu na kutambua jambo lililo jema, linalompendeza na kamilifu. Kutokana na neema aliyonijalia Mungu, nawaambieni nyinyi nyote: Msijione kuwa ni kitu zaidi kuliko mnavyopaswa kuwa. Fikira zenu na ziwe na kiasi kadiri ya kipimo cha imani Mungu aliyomgawia kila mmoja. Mwili una viungo vingi, kila kimoja na kazi yake. Hali kadhalika ingawa sisi ni wengi, tu mwili mmoja kwa kuungana na Kristo, na kila mmoja ni kiungo cha mwenzake. Basi, tunavyo vipaji mbalimbali kadiri ya neema tuliyopewa. Mwenye kipaji cha unabii na akitumie kadiri ya imani yake. Mwenye kipaji cha utumishi na atumikie. Mwenye kipaji cha kufundisha na afundishe. Mwenye kipaji cha kuwafariji wengine na afanye hivyo. Mwenye kumgawia mwenzake alicho nacho na afanye hivyo kwa ukarimu. Msimamizi na asimamie kwa bidii; naye mwenye kutenda jambo la huruma na afanye hivyo kwa furaha.
Ukatufanye chombo chema Yahweh nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Mungu wetu tazama watoto wadodo walio yatima,wanao lelewa na mzazi mmoja[single parent]sababu ya Ndoa kuvunjika/kutoelewana kwa wazazi,watoto walioterekezwa wazazi wao
wapo lakini hawawajali,watoto wanaopenda kusoma lakini hawana uwezo,watoto walio wagonjwa,wasiojiweza,wenye njaa,wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali,waliokatika vifungo vya yule mwovu,
waliokata tamaa,wenye shida/tabu..Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu,
Yahweh tunaomba ukawaokoe na ukawaponye kimwilina kiroho pia,
Mungu wetu tunaomba ukaguse maisha ya hawa watoto,
Baba ukaguse hizi ndoa,Baba ukawaguse na walezi wao..
Mungu wetu tunaomba ukaonekane katika maisha ya watoto hawa
Baba wa Mbinguni ukawatendee sawasawa na mapenzi yako..
Furaha ikawe nao,Amani isipotee,Baba wakapate tumaini,Yahweh
ukawafariji,ukawape ubunifu/maarifa walezi wao,
Jehovah tunaomba upokee sala/maombi yetu Baba wa Mbinguni
usikie kilio chetu na ukafute machozi ya hawa watoto,wazazi,walezi
na wote wanaowaangalia/walea..
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasaidia
kwa chochote kitakacho kupendeza wewe,iwe sala/maombi,ikawe
kulipia ada,chakula,mavazi,sabuni,kuwatia moyo,kufurahi pamoja nao,
Ee Mungu wetu tunaomba ukatuongoze katika yote...!!
Mapendo yenu na yawe bila unafiki wowote. Chukieni jambo lolote ovu, zingatieni jema. Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima. Msilegee katika bidii, ila muwe wachangamfu rohoni katika kumtumikia Bwana. Tumaini lenu liwaweke daima wenye furaha; muwe na saburi katika shida, na kusali daima. Wasaidieni watu wa Mungu katika mahitaji yao; wapokeeni wageni kwa ukarimu. Watakieni baraka wote wanaowadhulumu nyinyi; naam, watakieni baraka na wala msiwalaani. Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wenye kulia. Ishini kwa kupatana vema nyinyi kwa nyinyi. Msijitakie makuu, bali jishughulisheni na madogo. Msijione kuwa wenye hekima sana. Msilipe ovu kwa ovu. Zingatieni mambo mema mbele ya wote. Kadiri inavyowezekana kwa upande wenu, muwe na amani na watu wote. Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.” Zaidi ya hayo, Maandiko yasema: “Adui yako akiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kinywaji. Maana kwa kufanya hivyo utamfanya apate aibu kali kama makaa ya moto juu ya kichwa chake.” Usikubali kushindwa na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu..
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele..
Amina..!
Asanteni sana wapendwa katika Bwana kwa kuwa nami
Baba wa Mbinguni awe nanyi daima..
Nawapenda.
|
No comments:
Post a Comment