Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
ni Siku/wiki/mwaka mwingine tena Mungu wetu ametupa kibali cha kuendelea
kuiona siku hii...
Wangapi tulianza nao mwaka?nini tumempa Mungu?
ni wema gani tumetenda zaidi ya wengine?ni jambo gani zuri zaidi tumelifanya?
si kwamba sisi ni wazuri mno,si kwa nguvu zetu,wala si kwa utashi wetu,
si kwa akili zetu wala si kwa ujuaji wetu...
Ni kwa mapenzi yake Mungu wetu,ni kwa neema/rehema zake Baba wa Mbinguni
sisi kuwa hivi tulivyo leo hii..
Kutoka kwangu mimi Paulo, mtumishi wa Kristo Yesu, na mtume niliyeteuliwa na kuitwa kwa ajili ya kuhubiri Habari Njema ya Mungu. Hapo kale, Mungu aliwaahidi watu hii Habari Njema kwa njia ya manabii wake katika Maandiko Matakatifu. Hii Habari Njema inamhusu Mwana wa Mungu, Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kuhusu ubinadamu wake, alikuwa mzawa wa Daudi; kuhusu utakatifu wake wa kimungu, alithibitishwa kwa uwezo mkuu kwamba ni Mwana wa Mungu kwa kufufuliwa kutoka kwa wafu. Kwa njia yake, mimi nimepewa neema ya kuwa mtume, ili kwa ajili yake niwaongoze watu wa mataifa yote wapate kuamini na kutii. Nyinyi ni miongoni mwa watu hao; mmeitwa muwe watu wake Yesu Kristo. Basi, nawaandikia nyinyi nyote mlioko Roma ambao Mungu anawapenda, akawateua muwe watu wake. Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Tunakushuru ee Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu..
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote..
Asante kwa kutuchagua na kutupa nafasi ya kuendelea kuiona leo hii..
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari katika majukumu yetu..
Asante kwa mwaka uliopita na asante kwa mwaka huu tunaouanza..
Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni..
Usifiwe Jehovah,Uhimidiwe Yahweh,Unatosha Mungu wetu..
Uabudiwe Mfalme wa amani,hakuna kama wewe Mungu wetu..
Mungu mwenye nguvu,Baba wa Upendo,Baba wa huruma,Mponyaji wetu,
Kimbilio letu,Mungu wa walio hai,Mungu wa Yatima,Mungu wa wajane..
Alfa na Omega,wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho..
Sifa na utukufu tunakurudishia ee Baba wa Mbinguni..!!
Awali ya yote, namshukuru Mungu wangu kwa njia ya Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inasikika duniani kote. Mungu, ambaye ninamtumikia kwa moyo wangu wote katika kuhubiri Habari Njema ya Mwanae, ni shahidi wangu kwamba ninawakumbukeni daima katika sala zangu. Namwomba Mungu akipenda, anipatie nafasi nzuri ya kuja kwenu sasa. Kwa maana ninatamani sana kuwaoneni ili nipate kuwagawieni zawadi ya kiroho na kuwaimarisha. Ndiyo kusema, tutaimarishana: Imani yenu itaniimarisha mimi, na yangu itawaimarisha nyinyi. Ndugu zangu, nataka mjue kwamba mara nyingi nilikusudia kuwatembeleeni, lakini mpaka sasa nimezuiwa. Ningependa kupata mafanikio mema kati yenu kama nilivyopata kati ya watu wa mataifa mengine. Ninalo jukumu kwa watu wote, waliostaarabika na wasiostaarabika, wenye elimu na wasio na elimu. Ndiyo maana ninatamani pia kuihubiri Habari Njema kwenu nyinyi mlioko huko Roma.
Mungu wetu tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia
mikononi mwako Jehovah..
Yahweh tunaomba utusamehe Dhabi zetu zote tulizozifanya
kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua..
Mfalme wa amani nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale
wote waliotukosea..
Baba wa Mbinguni tunaomba utuepushe katika majaribu Mungu wetu utuokoe
na yule mwovu na Kazi zake zote..
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu Mungu wetu utufunike
kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..
Sioni aibu kutangaza Habari Njema; yenyewe ni nguvu ya Mungu inayowaokoa wote wanaoamini: Wayahudi kwanza na wasio Wayahudi pia. Kwa maana Habari Njema inaonesha wazi jinsi Mungu anavyowakubali watu kuwa waadilifu; jambo hili hufanyika kwa imani, tangu mwanzo mpaka mwisho; kama ilivyoandikwa: “Mwadilifu kwa imani ataishi.”
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Yahweh tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika ufanyaji/utendaji
Mungu wetu nasi tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji..
Yahweh tunayaweka Maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu
familia/ndugu na wote wanaotuzunguka...
Yahweh tunaomba Amani yako ikatawale,Upendo wetu ukadumu,tukawe salama moyoni,Baba wa Mbinguni ukatamalaki na kutuatamia,Mungu Baba ukawe mlinzi
wetu kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki,Yahweh ukaseme nasi,Baba wa Mbinguni
ukatupe macho ya rohoni,Jehovah ukatupe masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Mungu wetu neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni ukatupe hekima,busara,
utu wema na utuepushe na kiburi,chuki,makwazo,unafiki na yote yanayokwenda kinyume nawe..
Yahweh tunaomba utupe neema ya kufuata njia zako,Mungu wetu tukasimamie
Neno lako amri na sheia zako siku zote za maisha yetu..
Mungu wetu ukataufanye chombo chema nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi..
Ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa binadamu ambao kwa njia zao mbaya wanaupinga ukweli usijulikane. Kwa maana, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao; maana Mungu mwenyewe ameyadhihirisha. Tangu Mungu alipoumba ulimwengu, uwezo wake wa milele na uungu wake, ingawa havionekani kwa macho, vinafahamika wazi. Watu wanaweza kuyajua mambo hayo kutokana na vitu hivyo alivyoumba Mungu. Kwa hiyo hawana njia yoyote ya kujitetea! Ingawa wanajua kuna Mungu, lakini hawampi heshima anayostahili, wala hawamshukuru. Badala yake, fikira zao zimekuwa batili na akili zao tupu zimejaa giza. Wanajidai kuwa wenye hekima, kumbe ni wapumbavu. Wanaacha kumwabudu Mungu aishiye milele, na badala yake, wanaabudu sanamu zilizo mfano wa binadamu ambaye hufa, mfano wa wanyama, ndege, au wanyama watambaao. Kwa sababu hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya za mioyo yao na kufanyiana mambo ya aibu kwa miili yao. Wanaubadili ukweli juu ya Mungu kwa uongo; wanaheshimu na kuabudu kiumbe badala ya Muumba mwenyewe, ambaye ndiye astahiliye sifa milele! Amina. Kwa hiyo, Mungu amewaacha wafuate tamaa mbaya. Hata wanawake wanabadili matumizi yanayopatana na maumbile. Nao wanaume hali kadhalika, wanaacha kufuata matumizi ya maumbile ya mume na mke, wakawakiana tamaa wao kwa wao. Wanaume wanafanyiana mambo ya aibu, na hivyo wanajiletea wenyewe adhabu wanayostahili kwa vitendo vyao viovu. Kwa vile watu walikataa kumtambua Mungu, Mungu amewaacha katika fikira zao potovu, wakafanya yale ambayo hawangestahili kufanya. Wamejaa kila aina ya uovu, dhuluma, ulafi na ufisadi. Wamejaa wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu na nia mbaya; husengenya, na kusingiziana; ni watu wa kuchukiza kwa Mungu, wafidhuli, wenye kiburi na majivuno; hodari sana katika kutenda mabaya, na hawawatii wazazi wao; hawana dhamiri, hawatimizi ahadi zao, hawana wema wala huruma kwa wengine. Wanajua kwamba sheria ya Mungu yasema kwamba watu wanaoishi mithili hiyo, wanastahili kifo. Zaidi ya hayo, siyo tu kwamba wanafanya mambo hayo wao wenyewe, bali hata huwapongeza wale wanaofanya mambo hayohayo.
Mungu wetu tazama wenye shida/tabu,Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu wote walio katika mahangaiko..
Mungu wetu tunaomba ukawaponye wagonjwa na ukawape uvumilivu/nguvu
wanaowauguza,Yahweh tunaomba ukawavushe salama wale wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu ukaonekane katika maisha yao..
Baba wa Mbinguni ukawe faraja kwa wafiwa Mungu wetu ukawe tumaini
kwa wote waliokata tamaa,waliokataliwa,wenye hofu na mashaka..
Yahweh tunaomba ukawalishe wenye njaa na ukabariki vyanzo vyao..
Jehovah tunaomba ukawasamehe wale wote waliokwenda kinyume nawe
Mungu wetu ukawainue walio anguka Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Yahweh Nuru yako ikaangaze katika maisha Yao..
Baba wa Mbinguni ukasikie kuomba kwetu..Yahweh ukapokee
sala/maombi yetu Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi
yako...
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina..!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami
Baba wa Upendo akawabariki na pendo lenu likadumu
Mungu mwenye nguvu akawaguse kwa mkono wake kila
jambo likatendeke sawasawa na mapenzi yake..
Nawapenda.
|
No comments:
Post a Comment