Natazama juu milimani; msaada wangu utatoka wapi? Msaada wangu watoka kwa Mwenyezi-Mungu, aliyeumba mbingu na dunia. Hatakuacha uanguke; mlinzi wako hasinzii. Kweli mlinzi wa Israeli hasinzii wala halali. Mwenyezi-Mungu ni mlinzi wako; yuko upande wako wa kulia kukukinga. Mchana jua halitakuumiza, wala mwezi wakati wa usiku. Mwenyezi-Mungu atakukinga na baya lolote; atayalinda salama maisha yako. Mwenyezi-Mungu atakulinda katika shughuli zako zote tangu sasa na hata milele.
Shalom,Habari za Jumapili,Nimatumaini yangu wote mnaendelea vyema.. Huku kwetu hatujambo Mungu yu mwema sana.. Sina La zaidi nawatakia siku njema na Mungu awe nanyi... |
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment