Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana.. Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa mamjukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni Uhimidiwe Jehovah,Uabudiwe Yahweh Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu Matendo yako yanatisha...!! Hakuna kama wewe ee Mungu wetu.. Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni...!!
Mtu na atuone sisi kuwa ni watumishi wa Kristo tuliokabidhiwa siri za Mungu. Kinachotakiwa kwa yeyote yule aliyekabidhiwa kazi ni kuwa mwaminifu. Kwangu mimi si kitu nikihukumiwa na nyinyi, au na mahakama ya kibinadamu; wala sijihukumu mimi mwenyewe. Dhamiri yangu hainishtaki kwa jambo lolote, lakini hiyo haionyeshi kwamba sina lawama. Bwana ndiye anayenihukumu. Basi, msihukumu kabla ya wakati wake; acheni mpaka Bwana atakapokuja. Yeye atayafichua mambo ya giza yaliyofichika, na kuonesha wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mmoja atapata sifa anayostahili kutoka kwa Mungu. Ndugu, hayo yote niliyosema juu ya Apolo na juu yangu, ni kielelezo kwenu: Kutokana na mfano wangu mimi na Apolo nataka mwelewe maana ya msemo huu: “Zingatieni yaliyoandikwa.” Kati yenu pasiwe na mtu yeyote anayejivunia mtu mmoja na kumdharau mwingine. Nani amekupendelea wewe? Una kitu gani wewe ambacho hukupewa? Na ikiwa umepewa, ya nini kujivunia kana kwamba hukukipewa? Haya! Mmekwisha shiba! Mmekwisha kuwa matajiri! Mmekuwa wafalme bila ya sisi! Naam, laiti mngekuwa kweli watawala, ili nasi pia tutawale pamoja nanyi. Nafikiri Mungu ametufanya sisi mitume tuwe watu wa mwisho kabisa, kama watu waliohukumiwa kuuawa, maana tumekuwa tamasha mbele ya ulimwengu wote, mbele ya malaika na watu.
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe makosa yetu yote tuliyoyafanya Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote Ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...
Sisi ni wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini nyinyi ni wenye busara katika kuungana na Kristo! Sisi ni dhaifu, nyinyi ni wenye nguvu. Nyinyi mnaheshimika, sisi tunadharauliwa. Mpaka dakika hii, sisi tuna njaa na kiu, hatuna nguo, twapigwa makofi, hatuna malazi. Tena twataabika na kufanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa, tunawatakia baraka; tukidhulumiwa, tunavumilia; tukisingiziwa, tunajibu kwa adabu. Mpaka sasa tumetendewa kama uchafu wa dunia; na kwa kila mtu sisi ni takataka!
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe maarifa na ubunifu katika utendaji Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Baba wa Mbinguni tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba utubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Jehovah ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Mungu wetu tunaomba ukatupe neema ya kufuta njia zako Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mkono wako wenye nguvu ukatuguse Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Baba wa Mbinguni ukatupe hekima,busara,uvumilivu,utuwema,fadhili na upendo ukadumu kati yetu Tuka nene yaliyoyako ee Mungu wetu Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu Ukatufanye chombo chema Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho matakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Siandiki mambo haya kwa ajili ya kuwaaibisha nyinyi, bali kwa ajili ya kuwafundisheni watoto wangu wapenzi. Maana hata kama mnao maelfu ya walezi katika maisha yenu ya Kikristo, baba yenu ni mmoja tu, kwani katika kuungana na Kristo mimi ndiye niliyewazaeni kwa kuihubiri Habari Njema. Kwa hiyo, nawasihi: Fuateni mfano wangu. Ndiyo maana nimemtuma Timotheo kwenu. Yeye ni mtoto wangu mpenzi na mwaminifu katika kuungana na Bwana. Atawakumbusheni njia ninayofuata katika kuungana na Kristo; njia ninayofundisha kila mahali katika makanisa yote. Baadhi yenu wameanza kuwa na majivuno wakidhani kwamba sitakuja tena kwenu. Lakini, Bwana akipenda, nitakuja kwenu upesi; na hapo ndipo nitakapojionea mwenyewe, sio tu kile wanachoweza kusema hao wenye majivuno, bali pia kile wanachoweza kufanya. Maana ufalme wa Mungu si shauri la maneno matupu, bali ni nguvu. Mnapendelea lipi? Nije kwenu na fimbo, ama nije na moyo wa upendo na upole?
Mungu wetu tunawaweka mikonioni mwako watoto wetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaongoze katika hatua zao Jehovah tunaomba ukawape ufahamu,akili,maarifa, wakatambue mema na mabaya Ukafungue masikio yao ee Mungu wetu na wakapate kusikia sauti yako na wakawe watiifu kwako Mungu,wazazi/walezi, walimu,wakubwa/wadogo Mungu wetu wasipate kusikia yanayokwenda kinyume nawe wasisikilize taarifa potofu zinazo jenga hofu na zisizokupendeza Mungu wetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukawape macho ya rohoni Mungu wetu ukayatawale macho yao wakapate kuangalia yaliyo mema na sikuona yasioyo faa.. Baba wa Mbinguni tunaomba ukalinde vinywa vyao Mungu wetu wakanene yaliyo yako,ukawaokoe na Uongo,matusi na yote yasiyokupendeza Mungu Maneno yao yakapate kibali mbele zako Mungu na yakawanufaishe wale wote watakao yasikiliza na kuwajengea kiimani na utii.. Ukawape Moyo wa furaha,amani,uchangamfu na kukujua wewe Mungu mapema katika makuzi yao ee Baba wa Mbinguni ukatawale maisha yao Ubariki mikono yao Mungu wetu wakafanye kazi zilizo zao kwa bidii na imani na ukazibariki kazi za mikono yao Mungu wetu tunaomba ukabariki miguu yao watembeapo wakatembee njia zilizo zako,wasiambatane na walio waovu,wakaambatane na wenye hekima na njia zao zikawe salama Mungu wetu ukawalinde katika ujana wao na ukawaokoe na hatari zote katika ujana wao wakawe watoto wema,wawe kaka/dada wema na ili waje kuwa mama/baba wazuri mbele zako Mungu na mbele ya jamii yote... Ee Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukapokee sala/maombi yetu Jehovah ukatende sawasawa na mapenzi yako kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina...!!
Asanteni sana wapendwa/waungwana kwakuwa nami Mungu Baba aendelee kuwabariki na kwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima. Nawapenda.
|
No comments:
Post a Comment