Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 11 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 2...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana
Tumshukuru Mungu katika yote....

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majuku yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni
Uhimidiwe Jehovah,Uabudiwe Yahweh...
Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu,
Matendo yako yanatisha...
Neema yako yatutosha ee mungu wetu...!!


Siku zilipotimia za Yosefu na Maria kutakaswa kama walivyotakiwa na sheria, wazazi hao walimchukua mtoto, wakaenda naye Yerusalemu ili wamweke mbele za Bwana. Katika sheria ya Bwana imeandikwa: “Kila mzaliwa wa kwanza wa kiume atawekwa wakfu kwa Bwana.” Pia walikwenda ili watoe sadaka: Hua wawili au makinda mawili ya njiwa, kama ilivyotakiwa katika sheria ya Bwana. Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye. Roho Mtakatifu alikuwa amemhakikishia kwamba hatakufa kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Basi, akiongozwa na Roho Mtakatifu, Simeoni aliingia hekaluni; na wazazi wa Yesu walipomleta hekaluni mtoto wao ili wamfanyie kama ilivyotakiwa na sheria, Simeoni alimpokea mtoto Yesu mikononi mwake huku akimtukuza Mungu, akisema: “Sasa Bwana, umetimiza ahadi yako, umruhusu mtumishi wako aende kwa amani. Maana kwa macho yangu nimeuona wokovu ulioleta, ambao umeutayarisha uonekane na watu wote: Mwanga utakaowaangazia watu wa mataifa, na utukufu kwa watu wako Israeli.”


Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe 
wale wote waliotukosea
Mungu wetu utuepushe katika majaribu Yahweh utuokoe na 
yule mwovu na kazi zake zote
Ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni
utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo 
wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona..

Baba yake Yesu na mama yake walikuwa wakistaajabia maneno aliyosema Simeoni juu ya mtoto. Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu; na hivyo mawazo ya watu wengi yataonekana wazi. Nawe mwenyewe, uchungu ulio kama upanga mkali utauchoma moyo wako.”


Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji
Baba wa Mbinguni tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe...


Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu
familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Yahweh tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Jehovah tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukabariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu 
ya Bwana wetu Yesu Kristo
Yahweh ukatamalaki na kutuatamia
Mungu wetu tukawe salama rohoni
Baba wa Mbinguni ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Jehovah ukatupe neema ya kufuata njia zako Mungu wetu
tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Baba wa Mbinguni ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Yahweh tukanene yaliyo yako,ukatupe hekima na busara Mungu wetu
Baba wa Mbinguni ukatufanye chombo chema Mungu wetu
nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi


Palikuwa na nabii mmoja mwanamke, mzee sana, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila la Asheri. Alikuwa ameishi na mumewe kwa miaka saba tangu alipoolewa. Halafu alibaki mjane hadi wakati huo akiwa mzee wa miaka themanini na minne. Wakati huo wote alikaa hekaluni akifunga na kusali usiku na mchana. Saa hiyohiyo, alijitokeza mbele, akamshukuru Mungu, na kueleza habari za huyo mtoto kwa watu wote waliokuwa wanatazamia ukombozi wa Yerusalemu.

Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wote 
wanaokutafuta na kukuomba kwa bidii na imani
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba ukawaponye kimwili na kiroho pia
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea na kufuata njia zako
nazo zikawaweke huru
Ukawape macho ya kuona Mungu wetu na amasikio ya kusikia sauti yako
Ee Baba tunaomba ukasikie na ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukajibu sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Yesu Kristo kwakuwa nami
Mungu aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye
Nawapenda.

Wazawa wa Yuda

1Israeli alikuwa na wana wa kiume kumi na wawili: Reubeni, Simeoni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuluni, 2Dani, Yosefu, Benyamini, Naftali, Gadi na Asheri. 3Wana wa Yuda waliozaliwa na Bethshua, mkewe Mkanaani, walikuwa Eri, Onani na Shela. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu mbele ya Mwenyezi-Mungu, basi Mwenyezi-Mungu akamuua. 4Na Tamari, mkwewe, alimzalia wana wawili: Peresi na Zera. Jumla, wana wa Yuda walikuwa watano.
5Peresi alikuwa na wana wawili: Hesroni na Hamuli. 6Zera nduguye alikuwa na wana watano: Zimri, Etheni, Hemani, Kalkoli na Dara. 7Mwana wa Karmi, alikuwa Akari. Huyu aliwaletea Waisraeli taabu kwa sababu alijiwekea nyara zilizokuwa zimewekwa wakfu. 8Ethani alikuwa na mwana mmoja, jina lake Azaria.

Nasaba ya mfalme Daudi

9Wana wa Hesroni walikuwa Yerameeli, Ramu na Kelubai. 10Ramu alimzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa kabila la Yuda. 11Nashoni alimzaa Salma, Salma akamzaa Boazi, 12Boazi akamzaa Obedi, Obedi akamzaa Yese. 13Yese aliwazaa Eliabu, mwanawe wa kwanza, wa pili Abinadabu, wa tatu Shimea, 14wa nne Nethaneli, wa tano Radai, 15wa sita Osemu na wa saba Daudi. 16Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa watatu: Abishai, Yoabu na Asaheli. 17Abigaili alimzaa Amasa ambaye baba yake alikuwa Yetheri, Mwishmaeli.

Wazawa wa Hesroni

18Kalebu, mwana wa Hesroni, kutokana na wake zake wawili, Azuba na Yeriothi, aliwazaa Yesheri, Shaobabu na Ardoni. 19Azuba alipofariki, Kalebu alimwoa Efratha aliyemzalia Huri. 20Huri alimzaa Uri, naye Uri akamzaa Besaleli.
21Hesroni alipokuwa na umri wa miaka sitini, alimwoa binti Makiri, dada yake Gileadi. Huyo alimzalia mwana jina lake Segubu. 22Segubu alimzaa Yairi ambaye alitawala miji mikubwa ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi. 23Lakini falme za Geshuri na Aramu ziliwashambulia na kuwanyanganya miji ya Haroth-yairi, Kenathi na vijiji vyake, jumla miji sitini. Hao wote walikuwa wazawa wa Makiri, baba yake Gileadi. 24Baada ya Hesroni kufariki, Kalebu alimwoa Efratha,2:24 Kalebu alimwoa Efratha: Kiebrania: Huko Kalebu Efratha. mjane wa Hesroni, baba yake. Efratha alimzalia Kalebu mwana jina lake Ashuri, aliyekuwa mwanzilishi wa mji wa Tekoa.

Wana wa Yerameeli

25Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, alikuwa na wana watano: Ramu, mzaliwa wake wa kwanza, Buna, Oreni, Osemu na Ahiya. 26Yerameeli alikuwa na mke mwingine jina lake Atara. Huyu alimzalia Yerameeli mwana, jina lake Onamu. 27Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini na Ekeri. 28Wana wa Onamu walikuwa Shamai na Yada. Nao wana wa Shamai walikuwa Nadabu na Abishuri.
29Abishuri alioa mke, jina lake Abihaili, naye akamzalia wana wawili: Abani na Molidi. 30Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu; lakini Seledi alifariki bila watoto.
31Apaimu alikuwa na mwana mmoja aliyeitwa Ishi. Ishi alimzaa Sheshani, na Sheshani akamzaa Alai. 32Yada, nduguye Shamai, alikuwa na wana wawili: Yetheri na Yonathani. Lakini Yetheri alifariki bila watoto. 33Yonathani alikuwa na wana wawili: Pelethi na Zaza. Wote hao ni wazawa wa Yerameeli. 34Sheshani hakuwa na watoto wa kiume; alikuwa na binti tu. Hata hivyo, alikuwa na mtumwa wa Kimisri, jina lake Yarha. 35Hivyo, Sheshani akamwoza Yarha mtumwa wake, mmoja wa binti zake, naye akamzalia mwana jina lake Atai. 36Atai alimzaa Nathani, Nathani akamzaa Zabadi. 37Zabadi akamzaa Eflali, Eflali akamzaa Obedi, 38Obedi akamzaa Yehu, Yehu akamzaa Azaria, 39Azaria akamzaa Helesi, Helesi akamzaa Eleasa, 40Eleasa akamzaa Sismai, Sismai akamzaa Shalumu, 41Shalumu akamzaa Yekamia, na Yekamia akamzaa Elishama.

Wazawa wengine wa Kalebu

42Mzaliwa wa kwanza wa Kalebu, nduguye Yerameeli, aliitwa Mesha. Mesha alimzaa Zifu, Zifu akamzaa Maresha, Maresha akamzaa Hebroni.2:42 Hebroni: Kiebrania si dhahiri. 43Hebroni alikuwa na wana wanne: Kora, Tapua, Rekemu na Shema. 44Shema alikuwa baba yake Rahamu na babu yake Rekemu. Rekemu nduguye Shema alimzaa Shamai, 45Shamai akamzaa Maoni, na Maoni akamzaa Beth-suri. 46Kalebu alikuwa na suria, jina lake Efa. Huyu alimzalia wana wengine watatu: Harani, Mosa na Gazezi. Harani alimzaa Gazezi. 47Yadai alikuwa na wana sita: Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa na Shaafu. 48Kalebu alikuwa na suria mwingine jina lake Maaka. Huyu alimzalia wana wawili: Sheberi na Tirhana. 49Maaka alimzalia Kalebu wana; Shaafu mwanzilishi wa mji wa Madmana, na Sheva, mwanzilishi wa mji wa Makbena na Gibea. Kalebu alikuwa pia na binti, jina lake Aksa.
50Kalebu alikuwa na wazawa wengine pia kwa mkewe Efratha. Huri, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa na wana watatu: Shobali, mwanzilishi wa mji wa Kiriath-yearimu, 51wa pili Salma, mwanzilishi wa mji wa Bethlehemu, na wa tatu Herefu, mwanzilishi wa mji wa Bethi-gaderi. 52Shobali, mwanzilishi wa mji wa Kiriath-yearimu, alikuwa pia babu yao watu wa Haroe, na nusu ya wakazi wa mji wa Menuhothi, 53pamoja na koo zifuatazo zilizoishi Kiriath-yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi na Wamishrai. (Wasorathi na Waeshtaoli walitokana na watu hao).
54Salma, mwanzilishi wa mji wa Bethlehemu alikuwa babu ya Wanetofathi, Waatroth-beth-yoabu na nusu ya Wamenahathi yaani Wasori.
55Jamaa zifuatazo za waandishi ziliishi katika mji wa Yabesi: Watirathi, Washimeathi na Wasukathi. Wao ndio Wakeni waliotoka katika uzao wa Hamathi, aliyekuwa babu yao waliokuwa wa ukoo wa Warekabu.




1Mambo ya Nyakati2;1-55


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: