Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 14 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 3...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana...
Ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua
na kutupa kibali cha kuendelea tena kuiona leo hii
Si kwamba sisi ni wema sana,si kwamba sisi ni wazuri mno,
si kwa nguvu zetu wala si kwa akili zetu si kwa uwezo wetu
sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa neema/rehema ni kwa mapenzi yake Mungu wetu..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Hao wazazi walipokwisha fanya yote yaliyoamriwa na sheria ya Bwana, walirudi makwao Nazareti, wilayani Galilaya. Mtoto akakua, akazidi kupata nguvu, akajaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa naye.

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,Usifiwe Baba wa Mbinguni,Uhimidiwe Jehovah
Uabudiwe Yahweh...!
Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho ni Alfa na Omega
Matendo yako ni makuu mno,Matendo yako ni ya ajabu
Neema yako yatutosha Mungu wetu...!

Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na
kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea
Jehovah utuepushe katika majaribu Mungu wetu tunaomba utuokoe
na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba
utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Wazazi wake walikuwa na desturi ya kwenda Yerusalemu kila mwaka wakati wa sikukuu ya Pasaka. Mtoto alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, wote walikwenda kwenye sikukuu hiyo kama ilivyokuwa desturi. Baada ya sikukuu, walianza safari ya kurudi makwao, lakini Yesu alibaki Yerusalemu bila wazazi wake kuwa na habari. Walidhani alikuwa pamoja na kundi la wasafiri, wakaenda mwendo wa kutwa, halafu wakaanza kumtafuta miongoni mwa jamaa na marafiki. Kwa kuwa hawakumwona, walirudi Yerusalemu wakimtafuta.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji
Baba wa Mbinguni tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Jehovah ukatupe kama inavyokupendeza wewe.....

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu
Familia/ndugu na wote wanao tuzunguka
Jehovah tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Yahweh tunaomba ukabariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Mungu wetu ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana wetu
Yesu Kristo
Baba wa Mbinguni ukatamalaki na kutuatamia
Mungu wetu tukawe salama rohoni
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatupe macho ya kuona na masikio ya 
kusikia sauti yako na kuitii
Mungu wetu tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu
Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Jehovah tukanene yaliyo yako
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema yako na Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Mfalme wa amani amani yako ikatawale na upendo ukadumu kati yetu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike
kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi

Siku ya tatu, walimkuta hekaluni kati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Wote waliosikia maneno yake walistaajabia akili yake na majibu yake ya hekima. Wazazi wake walipomwona walishangaa. Maria, mama yake, akamwuliza, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivyo? Baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa huzuni.” Yeye akawajibu, “Kwa nini mlinitafuta? Hamkujua kwamba inanipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?” Lakini wazazi wake hawakuelewa maana ya maneno aliyowaambia. Basi, akarudi pamoja nao hadi Nazareti, akawa anawatii. Mama yake akaweka mambo hayo yote moyoni mwake. Naye Yesu akaendelea kukua katika hekima na kimo; akazidi kupendwa na Mungu na watu.

Baba wa Mbinguni tunawaweka mikononi mwako wote
wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Jehovah tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Yahweh tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Mungu wetu tunaomba ukawape macho ya rohoni na masikio ya kusikia
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukasikie na ukapokee sala/maombi yetu
Baba wa Mbinguni ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kutendea kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Krisro na Upendo wa Mungu Baba
ukawe nanyi daima.....
Nawapenda.





Wana wa mfalme Daudi

1Hawa ndio wana wa mfalme Daudi waliozaliwa wakati alipokuwa huko Hebroni:
Amnoni, mzaliwa wake wa kwanza; mama yake aliitwa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili, Mkarmeli; 2wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, bintiye Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne alikuwa Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi; 3wa tano alikuwa Shefatia, ambaye mama yake alikuwa Abitali; na wa sita alikuwa Ithreamu, ambaye mama yake alikuwa Egla.
4Wote sita, walizaliwa Hebroni ambako Daudi alitawala kwa muda wa miaka saba na nusu. Huko Yerusalemu, alitawala kwa muda wa miaka thelathini na mitatu. 5Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.
6Na mbali na hao alikuwa na wana wengine tisa: Ibhari, Elishua, Elifaleti, 7Noga, Nefegi, Yafia, 8Elishama, Eliada na Elifeleti. 9Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wengine waliozaliwa na masuria wake. Daudi alikuwa na binti pia, aliyeitwa Tamari.

Wazawa wa mfalme Solomoni

10Wazawa wa mfalme Solomoni: Solomoni alimzaa Rehoboamu, aliyemzaa Abiya, aliyemzaa Asa, aliyemzaa Yehoshafati, 11aliyemzaa Yehoramu, aliyemzaa Ahazia, aliyemzaa Yoashi, 12aliyemzaa Amazia, aliyemzaa Uzia, aliyemzaa Yothamu, 13aliyemzaa Ahazi, aliyemzaa Hezekia, aliyemzaa Manase, 14aliyemzaa Amoni, aliyemzaa Yosia. 15Yosia alikuwa na wana wanne: Yohanani, mzaliwa wake wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia na wa nne Shalumu. 16Yehoyakimu alikuwa na wana wawili: Yekonia na Sedekia.
17Wana wa Yekonia aliyechukuliwa mateka na Wababuloni walikuwa saba: Shealtieli, 18Malkiramu, Pedaya, Shenazari, Yekamia, Hoshama na Nedabia. 19Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Zerubabeli alikuwa na wana wawili: Meshulamu na Hanania, na binti mmoja, jina lake Shelomithi. 20Zerubabeli pia alikuwa na wana wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-hesedi. 21Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Yeshaya alimzaa Refaya, aliyemzaa Arnani, aliyemzaa Obadia, aliyemzaa Shekania.3:21 aya hii Kiebrania si dhahiri. 22Shekania alimzaa Shemaya. Wana wa Shemaya walikuwa sita: Hatushi, Igali, Baria, Nearia na Shafati. 23Nearia alikuwa na wana watatu: Eliehonai, Hizkia na Azrikamu. 24Eliehonai alikuwa na wana saba: Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohanani, Delaya na Anani.



1Mambo ya Nyakati3;1-24


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: