Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 17 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 6...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Mungu mwenye nguvu,Mungu mwenye huruma,Mungu mwenye kuponya
Mungu wa walio hai,Mungu mwenye kusamehe,Mungu mwenye Upendo
Baba wa Faraja,Baba wa Yatima,Mume wa Wajane,muweza wa yote
Alafa na Omega...!!

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhikli zako kwetu

Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha
kuendelea kuina leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudishia ee  Mungu wetu...!!


Hapo mwanzo, Neno alikuwako; naye alikuwa na Mungu, naye alikuwa Mungu. Tangu mwanzo Neno alikuwa na Mungu. Kwa njia yake vitu vyote viliumbwa; hakuna hata kiumbe kimoja kilichoumbwa pasipo yeye. Yeye alikuwa chanzo cha uhai na uhai huo ulikuwa mwanga wa watu. Na mwanga huo huangaza gizani, nalo giza halikuweza kuushinda. Mungu alimtuma mtu mmoja jina lake Yohane, ambaye alikuja kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Alikuja ili kwa ujumbe wake watu wote wapate kuamini. Yeye hakuwa huo mwanga, ila alikuja tu kuwaambia watu juu ya huo mwanga. Huu ndio mwanga halisi, mwanga unaokuja ulimwenguni, na kuwaangazia watu wote.



Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha

na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea
Mungu wetu utuepushe katika majaribu Jehovah tunaomba
utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Jehovah utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu
Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona



Basi, Neno alikuwako ulimwenguni, na kwa njia yake ulimwengu uliumbwa, lakini ulimwengu haukumtambua. Alikuja katika nchi yake mwenyewe, nao walio wake hawakumpokea. Lakini wale waliompokea, wale waliomwamini, aliwapa uwezo wa kuwa watoto wa Mungu, ambao walizaliwa si kwa maumbile ya kibinadamu, wala kwa nguvu za kimwili, wala mapenzi ya mtu, bali kutokana na Mungu mwenyewe.



Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki 
wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba
ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako

Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Yahweh tunaomba utubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu
tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Jehovah ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama moyoni
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusika sauti yako
na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Mungu wetu tukasimamie Neno lako amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu
Mfalme wa Amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Upendo ukadumu kati yetu,Ukatupe hekima na busara,utu wema
na fadhili
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako ziwe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu  nasi tukatumike
kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi



Naye Neno akawa mwanadamu, akakaa kwetu. Nasi tumeuona utukufu wake, utukufu wake yeye aliye Mwana wa pekee wa Baba; amejaa neema na ukweli. Yohane aliwaambia watu habari zake, akasema kwa sauti, “Huyu ndiye niliyemtaja wakati niliposema: ‘Anakuja mtu mmoja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, maana alikuwako kabla mimi sijazaliwa.’” Kutokana na ukamilifu wake sisi sote tumepokea neema kupita neema. Maana Mungu alitoa sheria kwa njia ya Mose, nayo neema na kweli vimetujia kwa njia ya Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu kamwe. Mwana wa pekee aliye sawa na Mungu ambaye ameungana na Baba, ndiye aliyetujulisha habari za Mungu.


Yahweh tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu
wote wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na Imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mko wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Jehovah tunaomba 
ukawafute machozi yao
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Jehovah tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuta njia zako
na wakasimamie Neno lako nalo likawaweke huru
Ukawape macho ya rohoni Mungu wetu ukawape na masikio
ya kusikia sauti yako
Ukawainue na kuwaokoa katika mapito/majaribu yao
Ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Jehovah
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu 

kwakuwanami/kunisoma
Mungu wetu akawaguse kwa makono wake wenye nguvu
Mfalme wa Amani akatawale na Amani ikawe nanyi daima
Nawapenda.

Nasaba ya makuhani wakuu

1Lawi alikuwa na wana watatu: Gershomu, Kohathi na Merari. 2Kohathi alikuwa na wana wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. 3Amramu alikuwa na wana wawili: Aroni na Mose, na binti mmoja jina lake Miriamu.
Aroni alikuwa na wana wanne: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
4Eleazari alimzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua, 5Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, 6Uzi akamzaa Zerahia, Zerahia akamzaa Merayothi, 7Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, 8Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi, 9Ahimaasi akamzaa Azaria, Azaria akamzaa Yohanani, 10na Yohanani akamzaa Azaria. (Azaria ndiye aliyefanya kazi ya ukuhani katika hekalu alilojenga mfalme Solomoni huko Yerusalemu). 11Azaria alimzaa Amaria, Amaria alimzaa Ahitubu, 12Ahitubu alimzaa Sadoki, Sadoki alimzaa Meshulamu, 13Meshulamu alimzaa Hilkia, Hilkia alimzaa Azaria, 14Azaria alimzaa Seraya, Seraya alimzaa Yehosadaki; 15Yehosadaki alikwenda uhamishoni wakati Mwenyezi-Mungu alipowapeleka uhamishoni watu wa Yuda na Yerusalemu kwa kuutumia mkono wa mfalme Nebukadneza.

Wazawa wengine wa Lawi

16Lawi alikuwa na wana watatu: Gershomu, Kohathi na Merari. 17Kila mmoja wao pia alikuwa na wana. Gershomu aliwazaa Libni na Shimei; 18Kohathi aliwazaa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli; 19naye Merari aliwazaa Mahli na Mushi. Hizi ndizo jamaa za Walawi kulingana na koo zao. 20Wafuatao ndio wazawa wa Gershomu kutoka kizazi hadi kizazi: Gershomu alimzaa Libni, Libni akamzaa Yahathi, Yahathi akamzaa Zima, 21Zima akamzaa Yoa, Yoa akamzaa Ido, Ido akamzaa Zera, Zera akamzaa Yeatherai.
22Hawa ndio wazawa wa Kohathi kutoka kizazi hadi kizazi: Kohathi alimzaa Aminadabu, Aminadabu akamzaa Kora, Kora akamzaa Asiri, 23Asiri akamzaa Elkana, Elkana akamzaa Ebiasafu, Ebiasafu akamzaa Asiri, 24Asiri akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Urieli, Urieli akamzaa Usia, Usia akamzaa Shauli. 25Wana wa Elkana walikuwa wawili: Amasai na Ahimothi.
26Na hawa ndio wazawa wa Ahimothi: Ahimothi alimzaa Elkana, Elkana akamzaa Sofai, Sofai akamzaa Nahathi, 27Nahathi akamzaa Eliabu, Eliabu akamzaa Yerohamu, Yerohamu akamzaa Elkana. 28Wana wa Samueli walikuwa wawili: Yoeli,6:28 Yoeli: Kiebrania hakina jina hili. mzaliwa wake wa kwanza, na Abiya, mdogo wake.
29Na hawa ndio wazawa wa Merari kutoka kizazi hadi kizazi: Merari alimzaa Mali, Mali akamzaa Libni, Libni akamzaa Shimei, Shimei akamzaa Uza, 30Uza akamzaa Shimea, Shimea akamzaa Hagia, Hagia akamzaa Asaya.

Waimbaji hekaluni

31Hawa ndio watu ambao mfalme Daudi aliwaweka wahudumu kama waimbaji katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu, baada ya sanduku la agano kuwekwa ndani. 32Walifanya kazi yao ya kuimba mbele ya hema takatifu la mkutano hadi wakati mfalme Solomoni alipojenga hekalu la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu. Waliutekeleza wajibu wao barabara, kwa zamu. 33Zifuatazo ni koo za wale ambao walitoa huduma hizo: Ukoo wa Kohathi: Hemani, kiongozi wa kundi la kwanza la waimbaji, alikuwa mwana wa Yoeli. Ukoo wake kutokana na Israeli ni kama ifuatavyo: Hemani, mwana wa Yoeli, mwana wa Samueli, 34mwana wa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elieli, mwana wa Toa, 35mwana wa Zufu, mwana wa Elkana, mwana wa Mahathi, mwana wa Amasai, 36mwana wa Elkana, mwana wa Yoeli, mwana wa Azaria, mwana wa Sefania, 37mwana wa Tahathi, mwana wa Asiri, mwana wa Ebiasafu, mwana wa Kora, 38mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, mwana wa Israeli.
39Asafu, ndugu yake alikuwa upande wake wa kulia. Ukoo wake kutokana na Lawi: Asafu, mwana wa Berekia, mwana wa Shimea, 40mwana wa Mikaeli, mwana wa Baaseya, mwana wa Malkiya, 41mwana wa Ethni, mwana wa Zera, mwana wa Adaya, 42mwana wa Ethani, mwana wa Zima, mwana wa Shimei, 43mwana wa Yahathi, mwana wa Gershomu, mwana wa Lawi.
44Ethani wa ukoo wa Merari, alikuwa kiongozi wa kundi la tatu la waimbaji. Ukoo wake kutokana na Lawi ni kama ifuatavyo: Ethani, mwana wa Kishi, mwana wa Abdi, mwana wa Maluki, 45mwana wa Hashabia, mwana wa Amazia, mwana wa Hilkia, 46mwana wa Amsi, mwana wa Bani, mwana wa Shemeri, 47mwana wa Mahli, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.
48Ndugu zao wengine walipewa wajibu wa kuhudumia hema takatifu la nyumba ya Mungu.

Wazawa wa Aroni

49Aroni na wazawa wake ndio waliokuwa wakitoa tambiko juu ya madhabahu ya tambiko za kuteketezwa na pia juu ya madhabahu ya kufukizia ubani. Walifanya kazi zote zilizohusika na mahali patakatifu sana ili kuifanyia Israeli upatanisho. Haya yote waliyafanya kulingana na maagizo aliyotoa Mose, mtumishi wa Mungu. 50Wafuatao ndio wazawa wa Aroni: Aroni alimzaa Eleazari, Eleazari akamzaa Finehasi, Finehasi akamzaa Abishua, 51Abishua akamzaa Buki, Buki akamzaa Uzi, Uzi akamzaa Serahia, 52Serahia akamzaa Merayothi, Merayothi akamzaa Amaria, Amaria akamzaa Ahitubu, 53Ahitubu akamzaa Sadoki, Sadoki akamzaa Ahimaasi.
54Yafuatayo ndiyo makazi yao kulingana na mipaka yake: Wazawa wa Aroni katika jamaa ya Wakohathi kulingana na kura yao, 55hao walipewa mji wa Hebroni katika nchi ya Yuda na malisho kandokando yake. 56Lakini mashamba ya mjini pamoja na malisho yake alipewa Kalebu mwana wa Yefune. 57Wazawa wa Aroni walipewa miji ya makimbilio: Hebroni, Libna pamoja na malisho yake, Yatiri na Eshtemoa pamoja na malisho yake, 58Hileni na Debiri pamoja na malisho yake, 59Ashani na Beth-shemeshi pamoja na malisho yake. 60Katika eneo la kabila la Benyamini walipewa miji ya Geba, Alemethi na Anathothi pamoja na malisho ya miji hiyo. Miji yote waliyopewa kulingana na jamaa zao ilikuwa kumi na mitatu. 61Miji kumi ya eneo la nusu ya kabila la Manase ilitolewa kwa sehemu iliyobaki ya ukoo wa Kohathi kwa kura kulingana na jamaa zao.
62Ukoo wa Gershomu, kulingana na jamaa zake ulipewa miji kumi na mitatu katika kabila la Isakari, na katika kabila la Naftali na katika kabila la Manase katika Bashani. 63Vivyo hivyo, miji kumi na miwili katika kabila la Reubeni, na katika kabila la Gadi na katika kabila la Zebuluni ilipewa ukoo wa Merari kulingana na jamaa zao. 64Kwa njia hii watu wa Israeli waliwapa Walawi miji ili waishi humo pamoja na malisho ya miji hiyo. 65(Miji iliyotajwa majina hapa juu katika kabila la Yuda, na katika kabila la Simeoni na katika kabila la Benyamini iligawiwa kabila la Lawi kwa kura.)
66Jamaa nyingine za ukoo wa Kohathi zilipewa miji pamoja na malisho yake katika kabila la Efraimu: 67Shekemu, mji wa makimbilio katika nchi ya milima ya Efraimu pamoja na malisho yake, Gezeri pamoja na malisho yake, 68Yokmeamu pamoja na malisho yake, Beth-horoni pamoja na malisho yake; 69Aiyaloni pamoja na malisho yake, na Gath-rimoni pamoja na malisho yake. 70Katika nusu ya kabila la Manase walipewa miji ya Aneri pamoja na malisho yake, na Bileamu pamoja na malisho yake. Hii ndiyo miji iliyopewa jamaa za ukoo wa Kohathi.
71Jamaa za ukoo wa Gershomu walipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake: Katika nusu ya kabila la Manase walipewa: Golani katika Bashani pamoja na malisho yake, Ashtarothi pamoja na malisho yake. 72Katika kabila la Isakari walipewa: Kedeshi pamoja na malisho yake, Deberathi pamoja na malisho yake, 73Ramothi pamoja na malisho yake na Anemu pamoja na malisho yake.
74Katika kabila la Asheri walipewa: Mashali pamoja na malisho yake, Abdoni pamoja na malisho yake, 75Hukoki pamoja na malisho yake, na Rehobu na malisho yake. 76Katika kabila la Naftali: Kedeshi katika Galilaya pamoja na malisho yake, Hamoni pamoja na malisho yake na Kiriathaimu pamoja na malisho yake. 77Jamaa za Merari zilizosalia, zilipewa miji ifuatayo pamoja na malisho yake kandokando ya miji hiyo: Katika kabila la Zebuluni walipewa Rimono pamoja na malisho yake na Tabori pamoja na malisho yake. 78Katika kabila la Reubeni, mashariki ya mto Yordani karibu na mji wa Yeriko walipewa Bezeri ulioko katika nyanda za juu pamoja na malisho yake, Yahasa pamoja na malisho yake, 79Kedemothi pamoja na malisho yake na Mefaathi pamoja na malisho yake. 80Katika kabila la Gadi walipewa Ramothi katika Gileadi pamoja na malisho yake, Mahanaimu pamoja na malisho yake, 81Heshboni pamoja na malisho yake na Yazeri pamoja na malisho yake.


1Mambo ya Nyakati6;1-81


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.


No comments: