Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 18 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 7...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana
Tumshukuru Mungu katika yote
Mungu wetu Baba  yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa Vyote Vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu mwenye nguvu,Mungu mwenye huruma,Mungu wa walio hai
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Mungu anayejibu,Mungu anayetenda,Mungu wa upendo,
Mungu anayeponya,Mungu wetu si mtu hata aseme uongo...

Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize? Tazama, nimepewa amri ya kubariki, naye amebariki wala siwezi kuitangua. Mwenyezi-Mungu hajaona ubaya kwa wana wa Yakobo, wala udhia kwa hao wana wa Israeli. Mwenyezi-Mungu Mungu wao yuko pamoja nao, Yeye husifiwa kwa vifijo miongoni mwao, yeye huzipokea sifa zao za kifalme. Mungu aliyewachukua kutoka Misri, huwapigania kwa nguvu kama za nyati. Hakika ulozi hauwezi kuwapinga watu wa Yakobo, wala uchawi dhidi ya watu wa Israeli. Sasa kuhusu Israeli, watu watasema, ‘Tazameni maajabu aliyotenda Mungu!’ Tazama! Waisraeli wameinuka kama simba jike, wanasimama kama simba dume. Ni kama simba asiyelala mpaka amalize mawindo yake, na kunywa damu ya mawindo.”

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha
kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudishi Mungu wetu...!!

Mungu wetu tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Yahweh tunaomba nasi utupe neema ya kuweza kuwasamehe
 wale wote waliotukosea
Mungu wetu utuepushe katika majaribu Jehovah tunaomba utuoke
na yule mwovu na kazi zake zote
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Jehovah utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu
Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona


“Mimi ni mzabibu wa kweli, na Baba yangu ndiye mkulima. Kila tawi ndani yangu lisilozaa matunda yeye huliondoa, na kila tawi lizaalo hulisafisha lipate kuzaa zaidi. Nyinyi mmekwisha kuwa safi kwa sababu ya ule ujumbe niliowaambieni. Kaeni ndani yangu, nami nikae ndani yenu. Kama vile tawi haliwezi peke yake kuzaa matunda lisipobaki katika mzabibu, hali kadhalika nanyi hamwezi kuzaa matunda msipokaa ndani yangu. “Mimi ni mzabibu, nanyi ni matawi. Akaaye ndani yangu, nami nikiwa ndani yake, huyo huzaa matunda mengi, maana bila mimi hamwezi kufanya chochote.


Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Mungu wetu tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwanbariki
wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu
ukatupe kama inavyokupendeza wewe......

Mungu wetu tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzuka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Mungu wetu tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Baba wa Mbinguni tunaoma ukavibariki vyote tunavyoenda
kugusa/kutumia
Yahweh tunaomba ukavitakase  na kuvifunika kwa Damu ya Bwana
wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahweh tunaomba ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia
sauti yako na kuitii
Jehovah tunaomba ukatupe neema ya kufuta njia zako
Mungu wetu tukasimamie Neno lako amri na sheria zako
 siku zote za maisha yetu
Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika
maisha yetu,upendo ukadumu kati yetu
Yahweh ukaonekane katika maisha yetu
Mungu wetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi.....

Mtu yeyote asipokaa ndani yangu hutupwa nje kama tawi litupwalo nje hata likakauka. Watu huliokota tawi la namna hiyo na kulitupa motoni liungue. Mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, basi, ombeni chochote mtakacho nanyi mtapewa. Baba yangu hutukuzwa kama mkizaa matunda mengi na kuwa wanafunzi wangu. Mimi nimewapenda nyinyi kama vile Baba alivyonipenda mimi. Kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu mtakaa katika pendo langu, kama vile nami nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Nimewaambieni mambo haya ili furaha yangu ikae ndani yenu, na furaha yenu ikamilike. Hii ndiyo amri yangu: Pendaneni; pendaneni kama nilivyowapenda nyinyi. Hakuna upendo mkuu zaidi kuliko upendo wa mtu atoaye uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Nyinyi ni rafiki zangu mkifanya ninayowaamuru. Nyinyi siwaiti tena watumishi, maana mtumishi hajui anachofanya bwana wake. Lakini mimi nimewaita nyinyi rafiki, kwa sababu nimewajulisha yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba yangu. Nyinyi hamkunichagua mimi; mimi niliwachagueni na kuwatuma mwende mkazae matunda, matunda yadumuyo, naye Baba apate kuwapeni chochote mnachomwomba kwa jina langu. Basi, amri yangu kwenu ndiyo hii: Pendaneni.

Baba wa Mbinguni tazama watoto wako wenye shida/tabu
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
wote wanaokutafuta/kukuomba,kukulilia,kukuhitaji kwa namna
moja au nyingine wewe Mungu ujua haja zao na mioyo yao
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea na kufuata njia zako
nazo zikawaweke huru
Jehovah ukawape macho ya rohoni na masikio ya kusikia sauti yako
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukawe nanyi daima..
Nwapenda.




Wazawa wa Isakari


1Wana wa Isakari walikuwa wanne: Tala, Pua, Yashubu na Shimroni.
2Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibsamu na Shemueli. Hao walikuwa wakuu wa jamaa za koo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Idadi ya wazawa wao siku za mfalme Daudi ilikuwa 22,600.
3Uzi alikuwa na mwana mmoja, jina lake Izrahia. Na wana wa Izrahia walikuwa Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia, jumla wanne,7:3 wanne: Kiebrania: Watano. na wote walikuwa wakuu wa jamaa. 4Kwa vile ambavyo wake na watoto wao walikuwa wengi sana, mliweza kupatikana vikosi vya wanajeshi 36,000 kutokana na wazawa wao.
5Ndugu zao katika jamaa zote za kabila la Isakari walioandikishwa kwa kufuata koo, walikuwa 87,000, na wote walikuwa mashujaa wa vita.

Wazawa wa Benyamini na Dani

6Benyamini alikuwa na wana watatu: Bela, Bekeri na Yediaeli. 7Bela alikuwa na wana watano: Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa zao, na wanajeshi mashujaa. Walioandikishwa kwa kufuata koo, idadi ya wazawa wao ilikuwa 22,034.
8Bekeri alikuwa na wana tisa: Zemira, Yoashi, Eliezeri, Eliehonai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Wote hawa ni wazawa wa Bekeri. 9Waliandikishwa kwa koo kulingana na vizazi vyao kama viongozi wa jamaa zao, na idadi ya wazawa wao ilikuwa 20,200, wote wakiwa mashujaa wa vita.
10Yediaeli alikuwa na mwana mmoja, jina lake Bilhani. Bilhani alikuwa na wana: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. 11Wote hawa walikuwa wakuu wa jamaa katika koo zao na askari mashujaa wa vita. Kutokana na wazawa wao, kulipatikana wanaume 178,200, wanajeshi hodari tayari kabisa kwa vita. 12Shupimu na Hupimu pia walikuwa wa kabila hili. Dani alikuwa na mwana mmoja, jina lake Hushimu.

Wazawa wa Naftali

13Naftali alikuwa na wana wanne: Yaasieli, Guni, Yereri na Shalumu. Hao walikuwa wazawa wa Bilha.7:13 Bilha: Suria wa Yakobo aliyemzalia Dani na Naftali.

Wazawa wa Manase

14Manase alikuwa na wana wawili kutokana na suria wake Mwaramu: Asrieli na Makiri. Makiri alikuwa baba yake Gileadi. 15Makiri aliwazaa Hupimu na Shupimu. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri alikuwa Selofehadi. Selofehadi alikuwa na mabinti peke yake.
16Maaka mkewe Makiri, alizaa mwana jina lake Pereshi. Jina la nduguye Pereshi lilikuwa Shereshi. Wanawe Shereshi walikuwa Ulamu na Rakemu. 17Rakemu alimzaa Bedani. Hawa wote ni wazawa wa Gileadi, mwana wa Makiri, mjukuu wa Manase. 18Hamo-lekethi, dada yake Gileadi, aliwazaa Ishhodi, Abiezeri na Mala. 19Wana wa Shemida walikuwa Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu.

Wazawa wa Efraimu

20Hawa ndio wazawa wa Efraimu kutoka kizazi hadi kizazi: Shuthela, Beredi, Tahathi, Eleada, Tahathi, 21Zabadi na Shuthela. Mbali na Shuthela, Efraimu alikuwa na wana wengine wawili, Ezeri, na Eleadi, ambao waliuawa na wenyeji wa asili wa nchi ya Gathi kwa sababu walikwenda huko kuwanyanganya mifugo yao. 22Efraimu baba yao aliomboleza vifo vyao kwa siku nyingi sana, na ndugu zake wakaja kumfariji. 23Ndipo Efraimu akalala na mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana. Efraimu akampa jina Beria, kwa sababu ya maafa yaliyoipata jamaa yake.
24Efraimu alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliyeijenga miji ya Beth-horoni ya juu na chini, na Uzen-sheera. 25Efraimu alimzaa pia Refa ambaye alimzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani, 26Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama, 27Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua.
28Milki zao na makao yao yalikuwa: Betheli na vitongoji vyake, Naraani uliokuwa upande wa mashariki, Gezeri uliokuwa upande wa magharibi pamoja na vitongoji vyake, Shekemu na vitongoji vyake, na Aya na vitongoji vyake. 29Na pia mipakani mwa wana wa Manase: Beth-sheani na vitongoji vyake, Taanaki na vitongoji vyake, Megido na vitongoji vyake na Dori na vitongoji vyake. Hiyo ndiyo miji walimoishi wazawa wa Yosefu, mwana wa Israeli.

Wazawa wa Asheri

30Hawa ndio wazawa wa Asheri. Asheri alikuwa na wana wanne: Imna, Ishva, Ishri na Beria, na binti mmoja jina lake Sera. 31Beria alikuwa na wana wawili: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi. 32Heberi alikuwa na wana watatu: Yafleti, Shomeri na Hothamu, na binti mmoja jina lake Shua. 33Yafleti pia alikuwa na wana watatu: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. 34Shemeri, nduguye, alikuwa na wana watatu: Roga, Yehuba na Aramu. 35Na Helemu, ndugu yake mwingine, alikuwa na wana wanne: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali. 36Wana wa Sofa walikuwa Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, 37Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera. 38Wana wa Yetheri walikuwa Yefune, Pispa na Ara. 39Wana wa Ula walikuwa Ara, Hanieli na Risia. 40Hao wote walikuwa wazawa wa Asheri na walikuwa wakuu wa jamaa zao, watu wateule na hodari wa vita. Idadi ya wale walioandikishwa kwa kufuata koo katika jeshi ilikuwa 26,000.



1Mambo ya Nyakati7;1-40


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: