Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 21 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 8...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua
na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
si kwa kuwa sisi ni wema sana,wala si kwakuwa ni wazuri mno
Si kwa nguvu zetu wala akili zetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa Neema/Rehema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu
Tumshukuru Mungu wetu katika yote....

Asante Baba wa Mbinguni kwa wema na fadhili zako
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudishia ee Mungu wetu




“Kama ulimwengu ukiwachukia nyinyi, kumbukeni kwamba umenichukia mimi kabla ya kuwachukia nyinyi. Kama mngalikuwa watu wa ulimwengu, ulimwengu ungaliwapenda nyinyi kama watu wake. Lakini kwa vile nyinyi si wa ulimwengu, ila mimi nimewachagueni kutoka ulimwenguni, kwa sababu hiyo ulimwengu unawachukieni. Kumbukeni niliyowaambieni: Mtumishi si mkuu kuliko bwana wake. Ikiwa wamenitesa mimi, watawatesa na nyinyi pia; kama wameshika neno langu, watalishika na lenu pia.

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu  zote tulizozitenda
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Jehovah nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote walio tukosea
Mungu wetu tunaomba utuepushe katika majaribu
Baba wa Mbinguni  utuokoe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Jehovah utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo
wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.....





Lakini hayo yote watawatendeeni nyinyi kwa sababu ya jina langu, kwani hawamjui yeye aliyenituma. Kama nisingalikuja na kusema nao wasingalikuwa na hatia; lakini sasa hawawezi kujitetea kwamba hawana dhambi. Anayenichukia mimi, anamchukia na Baba yangu pia. Kama nisingalifanya kwao mambo ambayo hakuna mtu mwingine amekwisha yafanya wasingalikuwa na hatia; lakini sasa wameona niliyoyafanya wakanichukia mimi, wakamchukia na Baba yangu pia. Ndiyo maana yale yaliyoandikwa katika sheria yao ni kweli: ‘Wamenichukia bure!’ “Atakapokuja huyo Msaidizi nitakayemtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyo Roho wa ukweli, atokaye kwa Baba, yeye atanishuhudia mimi. Nanyi pia mtanishuhudia kwa kuwa mmekuwa nami tangu mwanzo.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji
Baba wa Mbinguni tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,
wazazi wetu,Familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo
vimiliki
Mungu wetu tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki vyote tunavyoenda
kugusa/kutumia
Yahweh tunaomba ukavitakase na kuvifunika kwa Damu
ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Jehovah ukaonekane katika maisha yetu
Baba wa Mbinguni ukatupe macho ya kuona na masikio
ya kusikia sauti yako na kuitii
Mungu wetu tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Baba wa Mbinguni tukasimamie Neno lako amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu
Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Yahweh ukatupe hekima,busara na upendo ukadumu kati yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike
kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi



“Nimewaambieni hayo kusudi msiiache imani yenu. Watu watawafukuza nyinyi katika masunagogi yao. Tena, wakati unakuja ambapo kila atakayewaua nyinyi atadhani anamhudumia Mungu. Watawatendeeni mambo hayo kwa sababu hawamjui Baba, wala hawanijui mimi. Basi, nimewaambieni mambo haya ili saa yake itakapofika mkumbuke kwamba niliwaambieni. “Sikuwaambieni mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.

Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawaguse kwa mkono wako
wenye nguvu wote wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani
Jehovah tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Yahweh tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Mungu wetu tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
waka simamie Neno lako nalo likawaweke huru
Jehovah tunaomba ukawape macho ya rohoni na masikio ya kusika
Baba wa Mbinguni tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu tunaomba ukapokee sala/maombi yetu
Baba wa Mbinguni ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utufuku hata Milele
Amina....!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyo
mpendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nayi daima
Nawapenda.


Wazawa wa Benyamini

1Benyamini alikuwa na wana watano: Bela, mzaliwa wake wa kwanza, Ashbeli wa pili, Ahara wa tatu, 2Noha wa nne na Rafa wa tano.
3Bela naye alikuwa na wana: Adari, Gera, Abihudi, 4Abishua, Naamani, Ahoa, 5Gera, Shufamu na Huramu. 6Hawa ndio wazawa wa Ehudi. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa za wale waliokuwa wakiishi Geba, lakini wakachukuliwa mateka uhamishoni Manahathi; 7Naamani, Ahiya na Gera. Gera, baba yake Uza na Ahihudi, ndiye aliyewaongoza kuchukua hatua hiyo. 8Shaharaimu aliwapa talaka wake zake wawili, Hushimu na Baara na baadaye alipata watoto wa kiume nchini Moabu. 9Alimwoa Hodeshi, naye akamzalia wana saba: Yoabu, Sibia, Mesha, Malkamu, 10Yeuzi, Sakia, na Mirma. Hawa wanawe wote walikuja kuwa wakuu wa koo. 11Shaharaimu na mkewe Hushimu alipata wana wengine wawili: Abitubu na Elpaali. 12Wana wa Elpaali walikuwa watatu: Eberi, Mishamu na Shemedi ambaye aliijenga miji ya Ono na Lodi, pamoja na vijiji kandokando yake.

Wabenyamini walioishi Gathi na Aiyaloni

13Beria na Shema walikuwa miongoni mwa jamaa ambazo zilikuwa zinaishi katika mji wa Aiyaloni, na kuwafukuza wenyeji wa Gathi. 14Nao Ahio, Shashaki, Yeremothi, 15Zebadia, Aradi, Ederi, 16Mikaeli, Ishpa na Yoha ni wazawa wengine wa Beria. 17Zebadia, Meshulamu, Hizki, Heberi, 18Ishnerai, Izlia na Yobabu walikuwa wazawa wa Epaali. 19Yakimu, Zikri, Zabdi, 20Elienai, Zilethai, Elieli, 21Adaya, Beraya na Shimrathi walikuwa wazawa wa Shimei. 22Ishpani, Eberi, Elieli, 23Abdoni, Zikri, Hanani, 24Hanania, Elamu, Anthothiya, 25Ifdeya na Penueli walikuwa wazawa wa Shashaki. 26Shamsherai, Sheharia, Athalia, 27Yaareshia, Elia na Zikri walikuwa baadhi ya wazawa wa Yerohamu. 28Hao ndio waliokuwa wakuu wa koo zao kulingana na vizazi vyao. Walikuwa wakuu na waliishi Yerusalemu.

Wabenyamini walioishi Gibeoni na Yerusalemu

29Yeieli,8:29 Yeieli: Linganisha 9:35, Kiebrania hakina jina hili. alikuwa mwanzilishi wa mji wa Gibeoni. Mkewe alikuwa Maaka. 30Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Abdoni. Wanawe wengine ni Zuri, Kishi, Baali, Nadabu, 31Gedori, Ahio, Zekeri, 32na Miklothi baba yake Shimea. Hawa pia waliishi Yerusalemu karibu na watu wengine wa ukoo wao.

Ukoo wa mfalme Shauli

33Neri alimzaa Kishi, Kishi akamzaa Shauli. Shauli alikuwa na wana wanne: Yonathani, Malki-shua, Abinadabu na Eshbaali. 34Yonathani alimzaa Merib-baali, na Merib-baali akamzaa Mika. 35Mika alikuwa na wana wanne: Pithoni, Meleki, Terea na Ahazi. 36Ahazi alimzaa Yehoada. Naye Yehoada aliwazaa Alemethi, Azmawethi na Zimri. Zimri alimzaa Mosa. 37Mosa alimzaa Binea, aliyemzaa Rafa, aliyemzaa Eleasa, naye Eleasa akamzaa Aseli. 38Wana wa Aseli walikuwa sita: Majina yao ni Azrikamu, Bokeru, Ishmaeli, Shearia, Obadia na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Aseli. 39Nao wana wa Esheki, nduguye Aseli, walikuwa watatu. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Ulamu, wa pili Yeushi na wa tatu Elifeleti. 40Wana wa Ulamu walikuwa watu mashujaa sana wa vita, na wapiga upinde hodari. Alikuwa na wana na wajukuu wengi, jumla150. Hao wote waliotajwa hapo juu walikuwa wa ukoo wa Benyamini.



1Mambo ya Nyakati8;1-50


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.


No comments: