Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 10 May 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; Tumemaliza Kitabu cha -2 Wafalme ,Leo tunaanza kitabu Cha 1Mambo ya Nyakati 1...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana...
Tunamshukuru Mungu wetu kwa kutupa neema ya kuweza
kupitia kitabu cha "Wafalme" Asante sana Mungu wetu kwa nafasi hii
Kwa imani yote tuliyojifunza kupitia kitabu hiki yatakuwa ndani yetu
pia na faida kwetu na kwa wengine....

 Leo tunaanza Kitabu cha "1Mambo ya Nyakati"Mungu wetu tunaomba
tunapoanza kusoma Neno lako kupitia kitabu hiki,ukatupe macho
ya rohoni,masikio,uelewa na kutambua..
Mungu wetu tukasome na kuhifadhi pia elimu hii ikawafae na wengine
Ee Baba tunaomba ukatuongoze...!!

Siku zile, tangazo rasmi lilitolewa na Kaisari Augusto kuwataka watu wote nchini kote wahesabiwe. Sensa hiyo ilikuwa mara ya kwanza, wakati Kurenio alipokuwa mkuu wa mkoa wa Siria. Basi, wote waliohusika walikwenda kuhesabiwa kila mtu katika mji wake. Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya, na kwa vile alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi, alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yudea, alikozaliwa mfalme Daudi. Alikwenda kuhesabiwa pamoja na mchumba wake Maria ambaye alikuwa mjamzito. Walipokuwa huko, siku yake ya kujifungua ikawadia, akajifungua mtoto wake wa kwanza wa kiume, akamvika nguo za kitoto, akamlaza horini kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

Tunakushukuru Mungu wetu kwa siku hii pia
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali
cha kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana,wala si kwamba sisi 
ni wazuri mno,si kwa nguvu zetu wala utashi wetu
Si kwa uwezo wala akili zetu sisi kuwa hivi tulivyo
Ni kwa neema/rehema zako ni kwa mapenzi yako Mungu wetu
Sifa na Utukufu tunakurudishia Baba wa Mbinguni...!!

Katika sehemu hizo, walikuwako wachungaji wakikesha usiku mbugani kulinda mifugo yao. Malaika wa Bwana akawatokea ghafla, na utukufu wa Bwana ukawaangazia pande zote. Wakaogopa sana. Malaika akawaambia, “Msiogope! Nimewaleteeni habari njema ya furaha kubwa itakayowapata watu wote. Kwa maana, leo hii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi kwa ajili yenu, ndiye Kristo Bwana. Na hiki kitakuwa kitambulisho kwenu: Mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini.” Mara kundi kubwa la jeshi la mbinguni likajiunga na huyo malaika, wakamsifu Mungu wakisema: “Utukufu kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu anaowafadhili!”


Tazama jana imepita Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho
ni siku nyingine Jehovah
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Yahweh nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe
wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuokoe na yule mwovu
na kazi zake zote
Baba wa Mbinguni tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Mungu wetu utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu
Yesu Kristo wa Nazareti,yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate
kupona...

Baada ya hao malaika kuondoka na kurudi mbinguni, wachungaji wakaambiana: “Twendeni moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukalione tukio hili Bwana alilotujulisha.” Basi, wakaenda mbio, wakamkuta Maria na Yosefu na yule mtoto mchanga amelazwa horini. Hao wachungaji walipomwona mtoto huyo wakawajulisha wote habari waliyokuwa wamesikia juu yake. Wote waliosikia hayo walishangaa juu ya habari walizoambiwa na wachungaji. Lakini Maria aliyaweka na kuyatafakari mambo hayo yote moyoni mwake. Wale wachungaji walirudi makwao huku wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa yote waliyokuwa wamesikia na kuona; yote yalikuwa kama walivyokuwa wameambiwa.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Yahweh nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Jehovah tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki
wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Mfalme wa amani tunaomba amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,watoto,wazazi wetu
familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Baba wa Mbinguni tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote
tunavyovimiliki
Jehovah tunaomba  ukatamalaki na kutuatamia
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase na kuvifunika kwa Damu ya Bwana 
wetu Yesu Kristo..
Mungu wetu tukawe salama rohoni
Baba wa Mbinguni ukatupe macho ya kuona na masikio ya 
kusikia sauti yako na kuitii
Jehovah ukatupe neema ya kufuata njia zako Mungu wetu tukasimamie
Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Yahweh ukatupe akili ya kutamnbua mema na mabaya
Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu
Neema yako na Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
mkono wako wenye nguvu ukatuguse ee Mungu wetu
Ukatufanye chombo chema Baba wa Mbinguni nasi tukatumike
kama inavyokupendeza wewe..
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi


Siku nane baadaye, wakati wa kumtahiri mtoto ulipofika, walimpa jina Yesu, jina ambalo alikuwa amepewa na malaika kabla hajachukuliwa mimba.
Tazama wenye shida/tabu Mungu wetu
Tazama watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba ukamguse kila mmoja na mahitaji yake
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Baba wa Mbinguni ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Mungu wetu tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia
zako Mungu wetu ukawape macho ya rohoni
Yahweh tunaomba ukasikie kulia kwao Mungu wetu tunaomba
 ukawafute machozi yao
Baba wa Mbinguni tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Mungu wetu ukapokee sala/maombi yetu Jehovah ukawatendee
sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwa kuwanami/kunisoma
Baba wa Mbinguni akawabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye..
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukawe nanyi Daima...
Nawapenda.

Toka Adamu hadi Abrahamu

(Mwa 5:1-32; 10:1-32; 11:10-26)

1Adamu alimzaa Sethi, Sethi akamzaa Enoshi, Enoshi akamzaa Kenani, 2Kenani akamzaa Mahalaleli, Mahalaleli akamzaa Yaredi, 3Yaredi akamzaa Henoki, Henoki akamzaa Methusela. Methusela alimzaa Lameki, 4Lameki akamzaa Noa. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi.
5Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. 6Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Difathi na Togama. 7Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. 8Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. 9Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. 10Kushi alimzaa Nimrodi, aliyekuwa mtu shujaa wa kwanza duniani.
11Wazawa wa Misri ni Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi, 12Wapathrusi Wakaftori na Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti). 13Wana wa Kanaani walikuwa Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi. 14Kanaani pia ndiye babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, 15Wahivi, Waarki, Wasini, 16Waarvadi, Wasemari na Wahamathi.
17Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuri, Arpaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri na Mesheki. 18Arpaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. 19Eberi alikuwa na wana wawili; mmoja wao aliitwa Pelegi, (kwa maana wakati wake watu walikuwa wametawanyika duniani), na ndugu yake aliitwa Yoktani. 20Wana wa Yoktani walikuwa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, 21Hadoramu, Uzali, Dikla, 22Obali, Abimaeli, Sheba, 23Ofiri, Havila na Yobabu. Hao watu ni wana wa Yoktani.
24Ukoo wa Abrahamu kutokea Shemu ni kama ifuatavyo: Shemu alimzaa Arpaksadi, naye Arpaksadi akamzaa Shela. 25Shela akamzaa Eberi, Eberi akamzaa Pelegi, Pelegi akamzaa Reu; 26Reu akamzaa Serugi, Serugi akamzaa Nahori, Nahori akamzaa Tera, 27na Tera akamzaa Abramu, ambaye ndiye Abrahamu.

Wazawa wa Ishmaeli

(Mwa 25:12-16)

28Abrahamu alikuwa na watoto wawili wa kiume: Isaka na Ishmaeli. 29Hivi ndivyo vizazi vyao: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli alikuwa Nebayothi na wengine ni Kedari, Adbeeli, Mibsamu, 30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, 31Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli.
32Abrahamu alikuwa na suria aliyeitwa Ketura. Ketura alimzalia Abrahamu: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani. 33Wana wa Midiani walikuwa: Efa, Eferi, Henoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wazawa wa Ketura.

Wazawa wa Esau

(Mwa 25:12-16)

34Isaka, mwana wa Abrahamu, alikuwa na wana wawili: Esau na Israeli. 35Wana wa Esau walikuwa Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora. 36Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna na Amaleki. 37Wana wa Reueli walikuwa Nahathi, Zera, Shama na Miza.

Wazawa wa asili wa Edomu

(Mwa 36:20-30)

38Wana wa Seiri walikuwa Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani. 39Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna. 40Wana wa Shobali walikuwa Alvani, Manahathi, Ebali, Shefi1:40 Shefi: Mwa 36:23: Shefo. na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa Aya na Ana. 41Mwana wa Ana alikuwa Dishoni; na wana wa Dishoni walikuwa Hamrani,1:41 Hamrani: Mwa 36:26: Hemdani. Eshbani, Ithrani na Kerani. 42Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani na Akani; na wana wa Dishoni1:42 Dishoni: Mwa 36:26: Dishani. walikuwa Usi na Arani.

Wafalme wa Edomu

(Mwa 36:31-39)

43Wafuatao ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu, akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba. 44Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra alitawala badala yake. 45Yobabu alipofariki, Hushamu wa nchi ya Watemi alitawala badala yake. 46Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi alitawala badala yake, makao yake makuu yakiwa katika mji wa Avithi. Huyu ndiye aliyewapiga na kuwashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu. 47Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka alitawala badala yake. 48Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ulio karibu na mto Eufrate, alitawala badala yake. 49Shauli alipofariki, Baal-hanani mwana wa Akbori alitawala badala yake. 50Baal-hanani alipofariki, Hadadi kutoka Pai alitawala badala yake na jina la mkewe Akbori lilikuwa Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. 51Naye Hadadi akafariki.
Wakuu wa makabila ya Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi, 52Oholibama, Ela, Pinoni, 53Kenazi, Temani, Mibsari, 54Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.





1Mambo ya Nyakati1;1-54


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: