Hamjambo wapendwa/waungwana? Mimi nipo vyema Mungu yu mwema.... Pichani; ni da'Rose wa Mbeyela mimi nimezoea kumuita [Dogo] ni mke wa mtu na ni mama pia.... Kwenye "dawati langu leo" nimeguswa kumuweka na kumtambulisha kwako wewe usiyemfahamu Na wanaomfahamu haijalishi umemjulia wapi,kwenye mitandao,umekuwa naye,umesoma naye vyovyote.. jee nini kinakufanya umsome/umfuatilie? 1.Kwangu mimi da'Rose ni mwandishi mzuri na mchambuzi mzuri wa anavyoviandika hasa kwenye mambo ya kiimani... Akiamua kuandika anaandika [Magazeti]kirefu ... Ninavutiwa sana na magazeti yake hasa ya kiimani huwa ananibariki sana anavyolichambua Neno hata kama ni mvivu wa kusoma lakini utatamani ujue mwisho wake ilikuwajee? Hapo ndipo itabidi umalize kusoma tuu... kwa hili nampongeza sana na namuombea sana. Mungu aendelee kumpa kibali cha kuendelea.. Siku hizi amekuwa mvivu,sijui ametingwa,sijui majukumu ,muda hautoshi au laa... Ushauri wangu dada usijisahaulishe tunaomba urudi kwa Blog au unaweza kurudi kama VLOGGER Kwanini jamani umepewa bure njoo utoe bure japo muda ni gharama pia.... Blog;http://beyou-rose.blogspot.co.uk/ facebook;https://www.facebook.com/rose.w.mbeyela Instagram;https://www.instagram.com/rose_wa_mbeyela/ 2.kwenye majukumu yake kama mke na mama pia ananivutia yeah anauzungu kidogo na uswahili kidogo yupo makini na anavijimisimamo vyake anavyoamini yeye mwenyewe na anaweza kusimama kama mke na kama mama pia hasa wamama/wake wa ughaibuni nako kuna changamoto zake... [Hapa ndani kunakitu tumemuiga/jifunza pia,-alisema wao wakienda kwenye sherehe za Wazungu huwa wanaandaa mboga kabisaa nyumbani wakirudi huko wanaangusha Nguna/Ugali hahahahhahahh...!!! hiki kitendo hapa ndani Baba watoto amekizingatia sana tangu amejua hivyo....hahahaha"swahili na waswahili"] 3.Uchapakazi;Nifamnyaji wa kazi na hachagui saana kazi za kibishoo na ni mtu wa kujivunia anachokifanya Mbunifu[Mtundu]hupenda kujaribu na kujishughulisha.. Anajua kuzitafuta na anajua kuzitumia..... oohh nami nikianza kuongea sitamaliza leo kwa leo ngoja niishie hapa... Nakutakia maisha mema dadake ,yenye baraka,amani,upendo ukadumu kati yetu furaha pamoja na mume wako na watoto pia... Mungu akakupe maisha marefu yenye kumpendeza yeye ukatimize ndoto zako na kazi uliyotumwa hapa duniani.... Migimingilove...... |
Picha na da'Rose[shukrani] |
Asanteni kwa kunisoma,tukutane kwenye dawati langu lijalo sijui atakuwa nani labda ni wewe unayesoma hapa...
Mungu akitubariki tutakuwa na mahojiano/maongezi/video[sauti]si kuandika tuu...
Muwe na wakati mwema..
wenu; Da'Rachel siwa..
"Swahili Na Waswahili"Pamoja daima.
No comments:
Post a Comment