Jumuiya ya wasanii Watanzania Uingereza (WASATU) ilichemsha supu, ukumbi wa Heartlands , Birmigham, Uingereza Jumamosi iliyopita. Makutano haya yalikuwa pia sehemu ya mchango mahususi kusaidia wasichana wanaopewa mimba kabla ya kuwa watu wazima, kitongoji cha Tengeru, Arusha. Fedha zilikusanywa na mjasiria mali mkazi wa Birmingham, Mtanzania Sia Travel. Sia alijaa mlangoni akihakikisha kila senti iiliyolipwa na wahudhuriaji watashiba chakula , sanaa usiku kucha na kuwafariji vigoli wetu.
WASATU iliyoundwa mwaka 2016 chini ya udhamini wa Balozi wetu Uingereza, Mhe Asha Rose Migiro, inakutanisha wasanii wa ala mbalimbali chini ya viongozi- mwanamuziki na mcheza sarakasi mwenye nidhamu ya hali yajuu, Fab Moses na mtangaza mapishi ya Kitanzania, Uingereza, Bi Neema Kitilya, aliyetulizana kama shingo ya twiga.
Mwaka jana, 2017, shughuli hii ilifanywa Northampton na asilimia 20 ya kipato iliwafikia Watanzania waliofikwa na maafa ya mafuriko ya maji.
Viongozi wa WASATU – Neema Kitilya na Fab Moses wakijadiliana huku shughuli zikikwea minazi na kuta |
Fahari ya Tanzania – imesambazwa meza ya bidhaa mseto na “All Things African” |
Mcheza ngoma aliyepitia mitihani mikali na vikundi maarufu vya mila zetu- Kibisa na Muungano - Likiwa Ismail- akionesha SINDIMBA – bila aibu, staha wala wasiwasi.
|
Rama Sax akipuliza vitu. Zamani alipiga na Simba Wanyika akashiriki kurekodi wimbo wa “Sina Makosa”. Rama Sax ni pia mwimbaji mahiri |
Baadhi ya vyakula vya Kitanzania |
Msanii wa mapishi Neema John aliyechangia kazi njema na Neema Kitilya. |
Wageni toka Tanzania na Uganda. Huyo Mganda (kushoto) ni mwanafunzi wa lugha ya Kiswahili |
Mpiga Gitaa mkuu wetu, Jioni Ticha na kipande cha kuku baada ya kazi jukwaani. Alisafiri toka Leeds. Mbali sana na hapa |
Watanzania wakichangamkia shughuli |
Sia Travel akihamasika. Hakupitwa |
Mwanamuziki Saidi Kanda,(aliyesimama) mbabe na mtukuzaji wa vyombo asilia vya muziki wa Kitanzania, akijumuika na Wabongo nadhif, waliokuwemo |
Mwandishi na mwanamuziki, F Macha pamoja na wasanii Likiwa Ismail (ngoma) na Rama Sax. |
Shukrani...
kwa habari na Matukio nitumie kupitia Email;rasca@hotmail.co.uk
"Swahili Na Waswahili"Pamoja Daima.
No comments:
Post a Comment