Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 1 June 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 17...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki/mwezi mwingine tena Mungu wetu 
ametuchagua na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwa nguvu zetu wala si kwa uwezo wetu,si kwa akili zetu
wala si kwa utashi wetu  si kwamba sisi tumetenda mema 
na si kwamba sisi ni wazuri mno ni kwa rehema/neema zake
ni kwa mapenzi yake Mungu wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Sifa na Utukufu tunakurudishia Mungu wetu..!!



Ole wake mji wa Yerusalemu, mji mchafu, najisi na mdhalimu. Hausikilizi onyo lolote, wala haukubali kukosolewa. Haukumtegemea Mwenyezi-Mungu kamwe, wala kumkaribia Mungu wake. Viongozi wake ni simba wangurumao, mahakimu wake ni mbwamwitu wenye njaa jioni wasioacha chochote mpaka asubuhi. Manabii wake ni watu wasiojali na wadanganyifu. Makuhani wake wamevitia unajisi vitu vitakatifu na kuihalifu sheria kwa nguvu. Lakini Mwenyezi-Mungu aliye mjini humo ni mwadilifu, yeye hatendi jambo lolote baya. Kila siku asubuhi hudhihirisha kauli yake, naam, kila kunapopambazuka huitekeleza. Lakini wahalifu hawana aibu hata kidogo.

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Jehovah  Jireh..!Jehovah Nissi..!Jehovah Raah..!
Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shamlom..!
Emanuel-Mungu pamohja nasi..!!
Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni..!


Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...


Mwenyezi-Mungu asema: “Nimeyafutilia mbali mataifa; kuta zao za kujikinga ni magofu. Barabara zao nimeziharibu, na hamna apitaye humo. Miji yao imekuwa mitupu, bila watu, na bila wakazi. Nilisema, ‘Hakika mji huu watanicha na kukubali kukosolewa; hautaacha kukumbuka mara hizo zote nilizowaadhibu.’ Lakini watu wake walizidisha tamaa zao za kufanya matendo yao kuwa upotovu. “Kwa hiyo ningojeni mimi Mwenyezi-Mungu, ngoja siku nitakapoinuka kutoa mashtaka. Nimeamua kuyakusanya mataifa na falme, kuyamwagia ghadhabu yangu, kadhalika na ukali wa hasira yangu. Dunia yote itateketezwa kwa moto wa ghadhabu yangu. “Wakati huo nitaibadili lugha ya watu, nitawawezesha kusema lugha adili ili waniite mimi Mwenyezi-Mungu, na kuniabudu kwa moyo mmoja. Kutoka ng'ambo ya mito ya Kushi watu wangu wanaoniomba ambao wametawanyika, wataniletea sadaka yangu. “Siku hiyo, haitakulazimu kuona aibu, kutokana na matendo yako ya kuniasi, maana nitawaondoa miongoni mwako wale wanaojigamba na kujitukuza nawe hutakuwa na kiburi tena katika mlima wangu mtakatifu. Nitakuachia watu wapole na wanyenyekevu ambao watakimbilia usalama kwangu mimi Mwenyezi-Mungu. Waisraeli watakaobaki, hawatatenda mabaya wala hawatasema uongo; wala kwao hatapatikana mdanganyifu yeyote. Watapata malisho na kulala wala hakuna mtu atakayewatisha.”


Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
ukatupe kama inavyokupendeza wewe....




Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Mungu wetu

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi



Imba kwa sauti, ewe Siyoni, paza sauti ee Israeli. Furahi na kushangilia kwa moyo wote, ewe Yerusalemu! Mwenyezi-Mungu amekuondolea hukumu iliyokukabili, amewageuzia mbali adui zako. Mwenyezi-Mungu, mfalme wa Israeli yuko pamoja nawe hutaogopa tena maafa. Siku hiyo, mji wa Yerusalemu utaambiwa: “Usiogope, ee Siyoni, usilegee mikono. Mwenyezi-Mungu, Mungu wako yu pamoja nawe yeye ni shujaa anayekuletea ushindi. Yeye atakufurahia kwa furaha kuu, kwa upendo wake atakujalia uhai mpya. Atakufurahia kwa wimbo wa sauti kubwa, kama vile katika siku ya sikukuu.” Mwenyezi-Mungu asema: “Nitakuondolea maafa yako, nawe hutahitaji kuona aibu kwa ajili yake. Wakati huo, nitawaadhibu wote wanaokukandamiza. Nitawaokoa vilema na kuwakusanya waliotupwa, na kubadili aibu yao kuwa sifa na fahari duniani kote. Wakati huo nitawakusanya, na kuwafanya mjulikane na kusifiwa, miongoni mwa watu wote duniani nitakapowarudishia hali yenu njema nanyi muone kwa macho yenu wenyewe. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”


Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba  ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu  unajua haja za mioyo ya kila mmoja
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!

Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

Ujumbe wa Daudi kutoka kwa Nathani

(2Sam 7:1-17)

1Wakati mfalme Daudi alipokuwa akikaa katika ikulu, siku moja alimwita nabii Nathani, na kumwambia, “Hebu tazama, mimi ninakaa kwenye nyumba nzuri iliyojengwa kwa mwerezi, lakini sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu linakaa hemani.” 2Nathani akamwambia Daudi, “Fanya chochote unachofikiria moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yu pamoja nawe.” 3Lakini usiku uleule, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Nathani, kusema, 4“Nenda ukamwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Mwenyezi-Mungu anasema hivi: Wewe hutanijengea nyumba ya kukaa. 5Tangu wakati ule nilipowaongoza watu wa Israeli kutoka Misri mpaka hivi leo, sijaishi kwenye nyumba. Nimekuwa nikihama toka hema hadi hema, na toka makao hadi makao mengine. 6Je, kila mahali ambako nimekwenda na Waisraeli, nimepata kumwuliza mwamuzi wao yeyote niliyemwamuru awachunge watu wangu, “Kwa nini hukunijengea nyumba ya mierezi?” ’ 7Kwa hiyo basi, mwambie mtumishi wangu Daudi: ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi anasema hivi: Nilikutoa malishoni ulipokuwa unawachunga kondoo, ili uwe mkuu wa watu wangu Israeli. 8Tangu wakati huo nimekuwa pamoja nawe kokote ulikokwenda na nimewaangamiza maadui zako wote mbele yako. Nitakufanya kuwa maarufu kama wakuu wengine wa dunia. 9Nami nitawachagulia watu wangu wa Israeli mahali pa kuishi niwapandikize, ili waishi mahali pao wenyewe, wasisumbuliwe tena. Nao watu wakatili wanaotumia nguvu hawatawatesa tena kama hapo awali, 10tangu wakati nilipowateua waamuzi juu ya watu wangu Israeli; mimi nitawashinda maadui zako wote. Zaidi ya yote, mimi Mwenyezi-Mungu nakutangazia kuwa nitakujengea nyumba. 11Siku zako zitakapotimia za kujiunga na babu zako, nitamfanya mmoja wa watoto wako, wewe mwenyewe awe mfalme; nami nitauimarisha ufalme wake. 12Yeye ndiye atakayenijengea nyumba; nami nitahakikisha kwamba ufalme wake unadumu milele. 13Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; lakini sitamwondolea fadhili zangu kama vile nilivyomwondolea Shauli aliyekutangulia. 14Bali nitamwimarisha katika nyumba yangu na katika ufalme wangu milele, na kiti chake cha enzi kitakuwa imara daima.’”
15Nathani alimwelezea Daudi mambo yote haya kulingana na maono yote.

Sala ya Daudi ya shukrani

(2Sam 7:18-29)

16Kisha mfalme Daudi akaingia ndani ya hema na kuketi mbele ya Mwenyezi-Mungu, halafu akaomba, “Mimi ni nani, ee Mwenyezi-Mungu, na nyumba yangu ni nini hata unitukuze hivi? 17Isitoshe, umenifanyia mengine zaidi: Umenitolea ahadi juu ya vizazi vyangu vijavyo ee Mwenyezi-Mungu! 18Nikuambie nini zaidi, mimi Daudi mtumishi wako, kwa kunitukuza hivyo? Wewe unanijua mimi mtumishi wako. 19Ee Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya mtumishi wako na kwa kufuatana na moyo wako mwenyewe, umeyatenda hayo makuu yote, ili yajulikane hayo matendo makuu yote. 20Hakuna mwingine kama wewe, ee Mwenyezi-Mungu, na yote tunayoyasikia yanathibitisha kwamba hakuna Mungu mwingine ila wewe. 21Tena ni watu gani duniani ambao wanaweza kulinganishwa na watu wako wa Israeli ambao peke yao Mungu wao alikwenda kuwakomboa ili wawe watu wake? Wewe ulijifanyia jina kwa kutenda mambo makubwa na ya ajabu hapo ulipoyafukuza mataifa mbele ya watu wako ambao uliwakomboa kutoka Misri. 22Hata umejifanyia watu wako wa Israeli kuwa watu wako milele; nawe ee Mwenyezi-Mungu, umekuwa Mungu wao.
23“Basi sasa, ewe Mwenyezi-Mungu, liimarishe milele neno lako ulilosema kunihusu mimi mtumishi wako na kuhusu jamaa yangu. 24Nalo jina lako litatukuzwa milele, nao watu watasema, ‘Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, ndiye Mungu wa Israeli!’ Na jamaa yangu, mimi Daudi mtumishi wako, itaimarika mbele yako. 25Maana ee Mungu wangu nimepata ujasiri kukuomba kwa sababu wewe, umenifunulia ukisema ya kwamba utanijengea nyumba. 26Sasa ee Mwenyezi-Mungu, wewe ndiwe Mungu, umeniahidi mimi mtumishi wako jambo hili jema; 27kwa hiyo nakuomba uibariki nyumba yangu, mimi mtumishi wako, ili idumu milele mbele yako; kwani unachobariki wewe, huwa kimebarikiwa milele.”



1Mambo ya Nyakati17;1-27


Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: