Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 11 June 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; 1Mambo ya Nyakati 23...




Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua
na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!




Hapo zamani, Mungu alisema na babu zetu mara nyingi kwa namna nyingi kwa njia ya manabii, lakini siku hizi za mwisho, amesema nasi kwa njia ya Mwanae. Yeye ndiye ambaye kwa njia yake Mungu aliumba ulimwengu, akamteua avimiliki vitu vyote. Yeye ni mngao wa utukufu wa Mungu, na mfano kamili wa hali ya Mungu mwenyewe, akiutegemeza ulimwengu kwa neno lake lenye nguvu. Baada ya kuwatakasa binadamu dhambi zao, ameketi huko juu mbinguni, upande wa kulia wa Mungu Mkuu.


Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tuaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya 
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza
 kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi
wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza 
ili sisi tupate kupona

Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...





Mwana ni mkuu kuliko malaika, kama vile jina alilopewa na Mungu ni kuu kuliko jina lao. Maana Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Wewe ni Mwanangu; mimi leo nimekuwa Baba yako.” Wala hakusema juu ya malaika yeyote: “Mimi nitakuwa Baba yake, naye atakuwa Mwanangu.” Lakini Mungu alipokuwa anamtuma Mwanae, mzaliwa wa kwanza, ulimwenguni alisema: “Malaika wote wa Mungu na wamwabudu.” Lakini kuhusu malaika, alisema: “Amewafanya malaika wake kuwa upepo, na wahudumu wake ndimi za moto.”



Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...




Lakini kuhusu Mwana, Mungu alisema: “Kiti chako cha enzi, ee Mungu, chadumu milele na milele! Wewe wawatawala watu wako kwa haki. Wewe wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Ndiyo maana Mungu, Mungu wako, amekuweka wakfu na kukumiminia furaha kubwa kuliko wenzako.” Na tena: “Bwana, wewe uliumba dunia hapo mwanzo, mbingu ni kazi ya mikono yako. Hizo zitatoweka, lakini wewe wabaki daima, zote zitachakaa kama vazi. Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilishwa kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule daima, na maisha yako hayatakoma.” Mungu hakumwambia kamwe hata mmoja wa malaika wake: “Keti upande wangu wa kulia, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.” Malaika ni nini ila roho wanaomtumikia Mungu na ambao hutumwa kuwasaidia wale watakaopokea wokovu?



Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na  kuwalinda
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.

1Daudi alipokuwa mzee wa miaka mingi, alimtawaza Solomoni mwanawe awe mfalme wa Israeli.

Kazi ya Walawi

2Mfalme Daudi aliwakusanya wakuu wote wa Israeli, makuhani na Walawi. 3Walawi wote wanaume wenye umri wa miaka thelathini na zaidi, wakahesabiwa. Jumla yao ilikuwa 38,000. 4Hao, Daudi aliwagawanya: 24,000 kati yao wawe wasimamizi wa kazi ya nyumbani kwa Mwenyezi-Mungu, 6,000 wawe maofisa na waamuzi, 54,000 wawe mabawabu, na 4,000 wawe waimbaji, wakimsifu Mwenyezi-Mungu kwa ala za muziki alizotengeneza mfalme mwenyewe kwa madhumuni hayo. 6Daudi aliwagawanya Walawi katika makundi matatu kulingana na koo za kabila la Lawi: Ukoo wa Gershoni, ukoo wa Kohathi na ukoo wa Merari.
7Wana wa Gershoni walikuwa wawili: Ladani na Shimei. 8Ladani alikuwa na wana watatu: Yehieli mkuu wao, Zethamu na Yoeli. 9Wana wa Shimei walikuwa watatu: Shelomithi, Hazieli na Harani. Hawa walikuwa viongozi wa ukoo wa Ladani. 10Wana wa Shimei walikuwa viongozi wanne: Yahathi, Zina, Yeushi na Beria. 11Yahathi ndiye aliyekuwa mkuu wao, akifuatiwa na Ziza. Lakini Yeushi na Beria, kwa vile hawakuwa na wana wengi, walichukuliwa na ukoo mmoja.
12Wana wa Kohathi walikuwa wanne: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. 13Wana wa Amramu walikuwa Aroni na Mose. Aroni aliteuliwa awe akiweka wakfu vyombo vitakatifu kabisa, pia wazawa wake daima wafukizie ubani mbele za Mwenyezi-Mungu, wakimtumikia na kuwabariki watu katika jina la Mwenyezi-Mungu milele. 14Lakini wana wa Mose, mtu wa Mungu, hutajwa miongoni mwa kabila la Lawi. 15Wana wa Mose walikuwa Gershomu na Eliezeri. 16Aliyekuwa mkuu miongoni mwa wana wa Gershomu ni Shebueli. 17Eliezeri alikuwa na mwana mmoja tu; Rehabia, naye alikuwa kiongozi. Lakini Rehabia alikuwa na wana wengi sana. 18Ishari alimzaa Shelomithi, kiongozi wa kabila zima. 19Wana wa Hebroni walikuwa wanne: Mkuu wao alikuwa Yeria, wa pili Amaria, wa tatu Yahazieli na wa nne Yekameamu. 20Wana wa Uzieli walikuwa wawili: Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.
21Merari alikuwa na wana wawili: Mali na Mushi. Wana wa Mali walikuwa wawili: Eleazari na Kishi. 22Eleazari alifariki bila kupata mtoto wa kiume, ila mabinti tu. Mabinti hao waliolewa na binamu zao, wana wa Kishi. 23Wana wa Mushi walikuwa watatu: Mali, Ederi na Yeremothi.
24Hao ndio wana wa Lawi kulingana na koo zao. Kila mmoja wao aliyetimiza umri wa miaka ishirini na zaidi, aliandikishwa kwa jina, na alishiriki katika huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. 25Daudi alisema, “Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, amewapa watu wake amani, naye ataishi Yerusalemu milele. 26Kwa hiyo, Walawi hawatahitaji tena kulibeba hema takatifu au vyombo vyake vya ibada.” 27Kulingana na maagizo ya mwisho aliyotoa Daudi, Walawi wote waliofikia umri wa miaka ishirini waliandikishwa. 28Lakini wajibu wao ulikuwa ni kuwasaidia makuhani wa ukoo wa Aroni katika huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu; kuzitunza nyua na vyumba, kuvisafisha vyombo vitakatifu vyote na kufanya kazi zinazohusu huduma ya nyumba ya Mwenyezi-Mungu. 29Pamoja na hayo, walisaidia katika kazi ya mikate mitakatifu, unga mwembamba na sadaka ya nafaka, maandazi yasiyotiwa chachu, sadaka iliyookwa; sadaka iliyochanganywa na mafuta; pia sadaka katika kazi ya upimaji wa wingi wa sadaka na ukubwa wake 30na walisimama kumshukuru na kumsifu Mwenyezi-Mungu kila siku asubuhi na jioni, 31na wakati wa siku za Sabato, mwezi mwandamo na sikukuu, hapo sadaka za kuteketezwa zilipotolewa kwa Mwenyezi-Mungu. Sheria ziliwekwa kuhusu idadi ya Walawi walioagizwa kufanya kazi hizo daima mbele ya Mwenyezi-Mungu. 32Kwa hiyo, ulikuwa ni wajibu wao kutunza hema la mkutano na mahali patakatifu, na kuwasaidia ndugu zao makuhani, wazawa wa Aroni, kwenye ibada katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu.






1Mambo ya Nyakati23;1-32

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: