|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana
Tumshukuru Mungu wetu kila wakati Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Uabudiwe Jehovah,Uhimidiwe Yahweh,Matendo yako ni makuu mno, Matendo yako ni ya ajabu,Matendo yako yanatisha Hakuna kama wewe ee Mungu wetu,Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni...!!
Ndugu zangu, watu wa Mungu ambao mmeitwa na Mungu, fikirini juu ya Yesu Mtume na Kuhani Mkuu wa imani tunayoiungama. Yeye alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua kufanya kazi yake kama vile Mose alivyokuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu. Lakini Yesu anastahili heshima kubwa kuliko Mose maana mjenzi wa nyumba hupata heshima zaidi kuliko hiyo nyumba yenyewe. Kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini Mungu ndiye mjenzi wa vitu vyote. Mose alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Bwana kama mtumishi, na alinena juu ya mambo ambayo Mungu atayasema hapo baadaye. Lakini Kristo ni mwaminifu kama Mwana mwenye mamlaka juu ya nyumba ya Mungu. Sisi wenyewe ni nyumba yake kama tukiendelea kuwa hodari na thabiti katika kile tunachotumainia.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...
Kwa hiyo, basi, kama asemavyo Roho Mtakatifu: “Kama mkisikia sauti yake leo, msiwe wakaidi kama wakati ule waliponiasi kama wakati ule wa majaribio kule jangwani. Huko wazee wenu walinijaribu na kunichunguza, ingawa walishuhudia matendo yangu kwa miaka arubaini! Kwa sababu hiyo niliwakasirikia watu hao nikasema, ‘Fikira za watu hawa zimepotoka, hawajapata kamwe kuzijua njia zangu’. Basi, nilikasirika, nikaapa: ‘Hawataingia mahali pangu pa pumziko.’ Basi ndugu, jihadharini asije akawako yeyote miongoni mwenu aliye na moyo mbaya hivyo na asiyeamini hata kujitenga na Mungu aliye hai. Maadamu hiyo “Leo” inayosemwa katika Maandiko bado inatuhusu sisi, mnapaswa kusaidiana daima, ili mtu yeyote miongoni mwenu asidanganywe na dhambi na kuwa mkaidi. Maana sisi tunashirikiana na Kristo ikiwa tutazingatia kwa uthabiti tumaini tulilokuwa nalo mwanzoni.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Mungu wetu ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Maandiko yasema hivi: “Kama mkisikia sauti yake leo, msiwe wakaidi kama wakati ule waliponiasi.” Ni akina nani waliosikia sauti ya Mungu wakamwasi? Ni wale wote walioongozwa na Mose kutoka Misri. Mungu aliwakasirikia akina nani kwa miaka arubaini? Aliwakasirikia wale waliotenda dhambi, maiti zao zikatapakaa kule jangwani. Mungu alipoapa: “Hawataingia mahali pangu pa pumziko,” alikuwa anawasema akina nani? Alikuwa anasema juu ya hao walioasi. Basi, twaona kwamba hawakuingia huko kwa sababu hawakuamini.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na kuwalinda Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye.... Nawapenda. |
|
Waimbaji wa hekaluni
1Mfalme Daudi na viongozi wa Walawi, waliwateua baadhi ya wana wa Asafu, wa Hemani, na wa Yeduthuni, kuongoza katika huduma ya kutabiri kwa kutumia vinubi, na vinanda na matoazi. Hii ndiyo orodha ya wale waliochaguliwa kuongoza ibada, pamoja na aina ya kazi iliyofanywa na kila kikundi. 2Wana wanne wa Asafu: Zakuri, Yosefu, Nethania na Asharela. Wao walikuwa chini ya uongozi wa Asafu aliyetabiri wakati wote chini ya uongozi wa mfalme. 3Wana sita wa Yeduthuni: Gedalia, Seri, Yeshaya, Shimei, Hashabia na Matithia. Wao walikuwa chini ya uongozi wa baba yao; na walitabiri kwa kutumia vinubi, na wakamshukuru na kumtukuza Mwenyezi-Mungu. 4Wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, Yeremothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti-ezeri, Yoshbekasha, Malothi, Hothiri na Mahaziothi. 5Mungu alimpa Hemani, mwonaji wa mfalme, hawa watoto wa kiume kumi na wanne, na wa kike watatu, kama alivyoahidi ili kumtukuza. 6Wanawe wote walipiga muziki kwa matoazi, vinanda na vinubi, kwenye ibada katika nyumba ya Mwenyezi-Mungu wakiwa chini ya uongozi wa baba yao. Asafu, Yeduthuni na Hemani walikuwa chini ya amri ya mfalme. 7Idadi yao pamoja na wale ndugu zao Walawi waliofundishwa kumwimbia Mwenyezi-Mungu, wote waliokuwa stadi, ilikuwa 288. 8Wote, wakubwa kwa wadogo, waalimu kwa wanafunzi, walitumia kura katika kupanga kazi zao.
9Kura ya 1 ilimwangukia Yosefu wa jamaa ya Asafu; ya 2 Gedalia pamoja na ndugu zake na wanawe kumi na wawili; 10ya 3 Zakuri pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 11ya 4 ilimwangukia Seri pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 12ya 5 Nethania; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 13ya 6 Bukia; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 14ya 7 Asharela; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 15ya 8 Yeshaya; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 16ya 9 Matania; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 17ya 10 Shimei; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 18ya 11 Azareli; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 19ya 12 Hashabia; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 20ya 13 Shebueli; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 21ya 14 Matithia; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 22ya 15 Yeremothi; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 23ya 16 Hanania; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 24ya 17 Yoshbekasha; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 25ya 18 Hanani; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 26ya 19 Malothi; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 27ya 20 Eliatha; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 28ya 21 Hothiri; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili; 29ya 22 Gidalti; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili, 30ya 23 Mahaziothi; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili, 31ya 24 ilimwangukia Romamti-ezeri; pamoja na wanawe na ndugu zake kumi na wawili.
1Mambo ya Nyakati25;1-31
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment