Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo.. Yahweh..!Jehovah..! Adonai..!Elohim..!El Olam..!El Qanna..! El Elyon..!El shaddai..!Emanueli...!-Mungu pamoja nasi... Unastahili sifa Mungu wetu,Unastahili kuabudiwa Jehovah, Unastahili kuhimidiwa Yahweh,Unastahili Kutukuzwa Baba wa Mbinguni....!
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Yesu
aliwaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na
mimi pia. Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama isingekuwa
hivyo, ningalikwisha waambieni. Sasa nakwenda kuwatayarishieni nafasi.
Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi, nitarudi na kuwachukueni kwangu,
ili nanyi muwe pale nilipo mimi. Mnajua njia ya kwenda huko
ninakokwenda.” Thoma akamwuliza, “Bwana, hatujui unakokwenda,
tutawezaje basi, kuijua hiyo njia?” Yesu akamjibu, “Mimi ni njia, na
ukweli na uhai. Hakuna awezaye kwenda kwa Baba ila kwa kupitia kwangu.
Ikiwa mnanijua mimi, mnamjua na Baba yangu pia. Na tangu sasa, mnamjua,
tena mmekwisha mwona.” Filipo akamwambia, “Bwana, tuoneshe Baba, nasi
tutatosheka.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Yesu
akamwambia, “Nimekaa nanyi muda wote huu, nawe Filipo hujanijua?
Aliyekwisha niona mimi amemwona Baba. Unawezaje basi, kusema: ‘Tuoneshe
Baba?’ Je, huamini kwamba mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani
yangu? Maneno ninayowaambieni siyasemi kwa mamlaka yangu; Baba aliye
ndani yangu anafanya kazi yake. Mnapaswa kuniamini ninaposema kwamba
mimi niko ndani ya Baba naye Baba yuko ndani yangu. Ama sivyo, aminini
kwa sababu ya mambo ninayofanya. Kweli nawaambieni, anayeniamini
atafanya mambo ninayofanya mimi; naam, atafanya hata makuu zaidi, kwani
ninakwenda kwa Baba. Na chochote mtakachoomba kwa jina langu nitafanya,
ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba chochote kwa jina langu,
nitawafanyieni.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu Baba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
“Mkinipenda
mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba naye atawapeni Msaidizi
mwingine, atakayekaa nanyi milele. Yeye ni Roho wa ukweli. Ulimwengu
hauwezi kumpokea kwa sababu hauwezi kumwona wala kumjua. Lakini nyinyi
mnamjua kwa sababu anabaki nanyi na yu ndani yenu. “Sitawaacha nyinyi
yatima; nitakuja tena kwenu. Bado kidogo nao ulimwengu hautaniona
tena, lakini nyinyi mtaniona; na kwa kuwa mimi ni hai, nanyi pia mtakuwa
hai. Siku ile itakapofika mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, nanyi
mko ndani yangu, nami ndani yenu. Azipokeaye amri zangu na kuzishika,
yeye ndiye anipendaye. Naye anipendaye mimi atapendwa na Baba yangu,
nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” Yuda (si yule Iskarioti)
akamwambia, “Bwana, itawezekanaje wewe kujidhihirisha kwetu na si kwa
ulimwengu?” Yesu akamjibu, “Mtu akinipenda atashika neno langu, na Baba
yangu atampenda, nasi tutakuja kwake na kukaa naye. Asiyenipenda
hashiki maneno yangu. Na neno mlilosikia si langu, bali ni lake Baba
aliyenituma. “Nimewaambieni mambo haya nikiwa bado pamoja nanyi,
lakini Msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu,
atawafundisheni kila kitu na kuwakumbusheni yote niliyowaambieni.
Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu, wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru Ukawape macho ya rohoni ee Mungu wetu na masikio ya kusikia sauti yako,Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika maisha yao,Upendo ukadumu kati yao....
“Nawaachieni
amani; nawapeni amani yangu. Siwapi nyinyi kama vile ulimwengu
ufanyavyo. Msiwe na wasiwasi, wala msifadhaike. Mlikwisha sikia
nikiwaambieni: ‘Ninakwenda zangu, kisha nitarudi tena kwenu.’ Kama
mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu ninakwenda kwa Baba, maana yeye
ni mkuu kuliko mimi. Nimewaambieni haya sasa kabla hayajatokea, ili
yatakapotokea mpate kuamini. Sitasema nanyi tena mambo mengi, maana
mtawala wa ulimwengu huu anakuja. Kwangu mimi hawezi kitu; lakini
ulimwengu unapaswa kujua kwamba nampenda Baba, na ndiyo maana nafanya
kila kitu kama Baba alivyoniamuru. Simameni, tutoke hapa!
Tazama wafiwa Mungu wetu tunaomba ukawe mfaraiji wao
wakapate uvumilivu na amani katika wakati wao mgumu Baba wa Mbinguni tunayaweke haya yote mikono mwako tukiamini Mungu wetu utawatendea sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima Nawapenda.
| |
No comments:
Post a Comment