Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 4 September 2018

Kikombe Cha Asubuhi ; Nehemia 9...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana..
Tumshukuru Mungu wetu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Baba wa Upendo,Baba wa faraja,Baba wa huruma,Baba wa Baraka
Mungu mwenye nguvu,Mungu mwenye kuponya
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo,Muweza wa yote
Wewe ni mwanzo na wewe ni mwisho,Alfa na Omega...!!


Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Sifa na Utukufu tunakurudishia wewe ee Mungu wetu....!!




Yesu alizaliwa mjini Bethlehemu, mkoani Yudea, wakati Herode alipokuwa mfalme. Punde tu baada ya kuzaliwa kwake, wataalamu wa nyota kutoka mashariki walifika Yerusalemu, wakauliza, “Yuko wapi mtoto, Mfalme wa Wayahudi, aliyezaliwa? Tumeiona nyota yake ilipotokea mashariki, tukaja kumwabudu.” Mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, yeye pamoja na wakazi wote wa Yerusalemu. Basi, akawaita pamoja makuhani wakuu wote na waalimu wa sheria, akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?” Nao wakamjibu, “Mjini Bethlehemu, mkoani Yudea. Ndivyo nabii alivyoandika:


Tazama Jana imepita ee Mungu wetu Leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingineJehovah...
Yahweh tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha

na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti 

yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....




‘Ee Bethlehemu nchini Yudea, wewe si mdogo kamwe kati ya miji maarufu ya Yudea; maana kwako atatokea kiongozi atakayewaongoza watu wangu, Israeli.’” Hapo, Herode aliwaita faraghani hao wataalamu wa nyota, akawauliza wakati hasa ile nyota ilipowatokea. Kisha akawatuma Bethlehemu akisema, “Nendeni mkachunguze kwa makini habari za mtoto huyo. Mkisha mpata nileteeni habari ili nami niende kumwabudu.” Baada ya kumsikiliza mfalme, hao wataalamu wa nyota wakaenda. Kumbe ile nyota waliyokuwa wameiona upande wa mashariki iliwatangulia hata ikaenda kusimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto. Walipoiona hiyo nyota, walifurahi mno. Basi, wakaingia nyumbani, wakamwona yule mtoto pamoja na Maria mama yake; wakapiga magoti, wakamsujudia. Kisha wakafungua hazina zao, wakampa zawadi: Dhahabu, ubani na manemane. Mungu aliwaonya katika ndoto wasimrudie Herode; hivyo wakarudi makwao kwa njia nyingine.


Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....



Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii

 Mungu wetu ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu

Baba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Tukawe barua njema  ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...





Baada ya wale wageni kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto, akamwambia, “Amka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake, mkimbilie Misri. Kaeni huko mpaka nitakapokuambia, maana Herode anakusudia kumuua huyu mtoto.” Hivyo, Yosefu aliamka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, akaondoka usiku, akaenda Misri. Akakaa huko mpaka Herode alipokufa. Jambo hilo lilifanyika ili neno alilosema Bwana kwa njia ya nabii litimie: “Nilimwita Mwanangu kutoka Misri.”


Mungu Baba tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabuwote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na  kuwalinda
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.


Watu wanaungama dhambi zao

1Siku ya ishirini na nne ya mwezi huo wa saba, watu wa Israeli walikusanyika, wakifunga na kuvaa mavazi ya magunia na kujipaka udongo kichwani kuonesha majuto yao. 2Wakati huo, walikuwa wamejitenga mbali na watu wa mataifa mengine, wakasimama na kuungama dhambi zao na maovu ya babu zao. 3Kwa muda wa kama masaa matatu, walisimama huku sheria ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, inasomwa. Na kwa masaa matatu yaliyofuata, walikuwa wakitubu na kumwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.
4Kuliwekwa jukwaa la Walawi; hapo walisimama Yeshua, Bani, Kadmieli, Shebania, Buni, Sherebia, Bani na Kenani. Wakamwomba kwa sauti kubwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wao.
5Walawi, yaani: Yeshua, Kadmieli, Bani, Hashabuea, Sherebia, Hodia, Shebania na Pethahia wakawaambia watu;
“Simameni na kumsifu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Msifuni milele na milele!
Na watu walisifu jina lako tukufu,
ambalo hutukuka kuliko baraka na sifa zote.”

Sala ya toba

6Ezra akaomba kwa sala ifuatayo:
“Wewe peke yako ndiwe Mwenyezi-Mungu;
ndiwe uliyefanya mbingu na jeshi lake lote,
dunia na vyote vilivyomo,
bahari na vyote vilivyomo;
nawe ndiwe unayevihifadhi hai,
na jeshi lote la mbinguni lakuabudu wewe.
7Wewe ndiwe Mwenyezi-Mungu,
Mungu uliyemchagua Abramu,
ukamtoa toka Uri ya Wakaldayo
na kumpa jina Abrahamu.
8Ukamwona kuwa yu mwadilifu mbele yako;
ukafanya agano naye kuwapa wazawa wake nchi ya Wakanaani,
Wahiti, Waamori, Waperizi, Wayebusi na Wagirgashi.
Na ahadi yako ukaitimiza;
kwani wewe u mwaminifu.
9“Uliyaona mateso ya babu zetu
walipokuwa nchini Misri,
na walipokuomba msaada kwenye Bahari ya Shamu
uliwasikia.
10Ulifanya ishara na maajabu dhidi ya Farao,
watumishi wake wote
na watu wote wa nchi yake;
kwani ulijua kuwa
waliwakandamiza babu zetu.
Ukajipatia umaarufu uliopo mpaka leo.
11Uliigawa bahari katikati mbele yao,
nao wakapita katikati ya bahari,
mahali pakavu.
Lakini ukawatupa Wamisri waliowafuatia
kama jiwe zito ndani ya maji mengi.
12Mchana uliwaongoza kwa mnara wa wingu,
na usiku uliwaongoza kwa mnara wa moto
ili kuwamulikia njia ya kuendea.
13Kule mlimani Sinai
ulishuka toka mbinguni na kuzungumza nao.
Ukawapa maagizo safi, sheria za kweli,
kanuni nzuri na amri.
14Kwa njia ya Mose, mtumishi wako,
ukawajulisha Sabato yako takatifu
na ukawaagiza kuzifuata amri,
kanuni na sheria ulizowaamrisha.
15Walipokuwa na njaa,
ukawapa chakula kutoka mbinguni.
Walipokuwa na kiu
ukawapa maji kutoka kwenye mwamba.
Ukawaagiza kuichukua nchi uliyokuwa umewaahidi.
16Lakini wao na babu zetu wakawa na kiburi
na wakawa na shingo ngumu
wakakataa kufuata maagizo yako.
17Wakakataa kutii;
wasiyakumbuke maajabu uliyofanya miongoni mwao.
Wakawa na shingo zao ngumu,
wakajichagulia kiongozi wa kuwarudisha
utumwani nchini Misri.
Bali wewe Mungu u mwepesi kusamehe,
mwenye neema na huruma,
wewe hukasiriki upesi.
U mwenye fadhili nyingi, na hukuwatupa.
18Hata walipojitengenezea sanamu ya ndama na kusema,
‘Huyu ndiye mungu wetu
aliyetutoa kutoka nchi ya Misri,’
wakawa wamefanya kufuru kubwa.
19Wewe kwa huruma zako nyingi
hukuwatupa kule jangwani.
Mnara wa wingu
uliowaongoza mchana haukuondoka,
wala mnara wa moto
uliowamulikia njia usiku, haukuondoka.
20Ukawapa roho yako njema kuwashauri;
ukawapa mana kuwa chakula chao na maji ya kunywa
ili kutuliza kiu chao.
21Ukawatunza jangwani kwa miaka arubaini
na hawakukosa chochote;
mavazi yao hayakuchakaa
wala nyayo zao hazikuvimba.
22“Ukawaruhusu kushinda falme na mataifa,
ukawafanyia mengi kila upande.
Wakaishinda nchi ya Heshboni
alikotawala mfalme Sihoni;
na tena wakaishinda nchi ya Bashani
alikotawala mfalme Ogu.
23Wazawa wao ukawafanya wawe wengi
kama nyota za mbinguni;
ukawaleta katika nchi
uliyowaahidi babu zao.
24Hivyo, hao wazawa wakaja na kuimiliki nchi;
uliwashinda wakazi wa nchi hiyo,
Wakanaani, ukawatia mikononi mwao,
pamoja na wafalme wao,
watu wao na nchi yao ili wawatende wapendavyo.
25Miji yenye ngome wakaiteka,
wakachukua nchi yenye utajiri,
majumba yenye vitu vingi vizuri,
visima vilivyochimbwa,
mashamba ya mizabibu na mizeituni
pamoja na miti yenye matunda kwa wingi.
Hivyo wakala,
wakashiba na kunenepa
na kuufurahia wema wako.
26Lakini hawakuwa waaminifu kwako.
Wakakuasi,
wakaiacha sheria yako
na kuwaua manabii waliowaonya
ili wakurudie wewe.
Wakakufuru sana.
27Hivyo, ukawatia katika mikono ya adui zao,
nao wakawatesa.
Lakini wakiwa katika mateso yao,
wakakulilia, nawe ukawasikia kutoka mbinguni.
Na kwa huruma zako nyingi,
ukawapelekea viongozi wa kuwaokoa;
nao wakawakomboa toka mikononi mwao.
28Lakini amani ilipopatikana
wakatenda dhambi tena mbele yako,
nawe ukawaacha watiwe katika
mikono ya adui zao wawatawale.
Hata hivyo, walipotubu na kukulilia
ukawasikiliza kutoka mbinguni.
Na kwa kulingana na huruma zako nyingi,
ukawaokoa mara nyingi.
29Ukawaonya ili wairudie sheria yako.
Hata hivyo, kwa kiburi chao,
wakaacha kuzitii amri zako.
Wakayaasi maagizo yako,
ambayo kwayo mtu akiyatii, ataishi.
Wakawa wajeuri
pia wakafanya shingo zao ngumu,
na wakakataa kuwa watiifu.
30Ukawavumilia kwa miaka mingi,
na kuwaonya kwa njia ya roho yako
kwa kupitia manabii wako;
hata hivyo hawakusikiliza.
Basi ukawaacha
ukawatia mikononi mwa mataifa mengine.
31Hata hivyo,
kutokana na huruma zako nyingi,
hukuwaacha waangamie kabisa au kuwatupa,
kwani wewe u Mungu mwenye neema
na huruma.
32Kwa hiyo, ee Mungu wetu,
Mungu Mkuu,
mwenye nguvu na wa kutisha,
wewe unalishika agano lako
na una fadhili nyingi.
Mateso yaliyotupata, sisi,
wafalme wetu, wakuu wetu,
makuhani wetu, manabii wetu,
babu zetu na watu wako wote
tangu wakati wa wafalme wa Ashuru mpaka leo,
usiyaone kuwa ni madogo.
33Hata hivyo,
unayo haki kwa kutuadhibu hivyo;
kwani wewe umekuwa mwaminifu
ambapo sisi tumekuwa watenda maovu.
34Wafalme wetu, wakuu wetu,
makuhani wetu na babu zetu
hawajaishika sheria yako
wala kujali amri yako
na maonyo yako uliyowapa.
35Hawakukutumikia katika ufalme wao,
wala walipoyafurahia mema yako mengi uliyowajalia kwa wingi,
katika nchi kubwa na yenye rutuba uliyowapa
hawakuyaacha matendo yao maovu.
36Na leo tumekuwa watumwa;
tu watumwa katika nchi uliyowapa babu zetu
wafurahie matunda na vipawa vyake vyema.
37Kwa sababu ya dhambi zetu,
utajiri wa nchi hii
unawaendea wafalme uliowaleta kututawala.
Wanatutawala wapendavyo
hata na mifugo yetu
wanaitendea wapendavyo,
tumo katika dhiki kuu.”
Watu wanatia sahihi mapatano
38 9:38 Kiebrania 10:1 Kutokana na haya yote yaliyotokea, sisi tunaweka agano imara na wakuu wetu kwa maandishi; Walawi na makuhani wanatia sahihi zao na mhuri wao.



Nehemia9;1-38

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: