Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Sunday, 2 September 2018

Natumaini Jumapili ni njema/inaendelea vyema;Burudani-No Longer Slaves - Jonathan David & Melissa Helser ,Who You Say I Am - Hillsong Worship,Passion - Let It Be Jesus ft. Christy Nockels




Wapendwa/Waungwana;Nawatakia kila la heri,baraka na amani....





+


















Neno La Leo;Wafilipi 2;12-18

Mwanga kwa ulimwengu

12Wapenzi wangu, nilipokuwa nanyi mlinitii daima, na hata sasa niwapo mbali nanyi endeleeni kutii. Fanyeni kazi kwa hofu na tetemeko kwa ajili ya ukombozi wenu, 13kwani Mungu ndiye afanyaye kazi daima ndani yenu, na kuwapeni uwezo wa kutaka na kutekeleza mambo yanayopatana na mpango wake mwenyewe.
14Fanyeni kila kitu bila kunungunika na bila ubishi, 15ili mpate kuwa watu safi, wasio na lawama, kama watoto wanyofu wa Mungu wanaoishi katika ulimwengu mbaya na uliopotoka. Mtangara kati yao kama nyota zinavyoliangaza anga, 16mkishika imara ujumbe wa uhai. Na hapo ndipo nami nitakapokuwa na sababu ya kujivunia katika siku ile ya Kristo, kwani itaonekana dhahiri kwamba bidii yangu na kazi yangu havikupotea bure.
17Hata ikiwa nitatolewa mhanga pamoja na imani yenu iliyo tambiko kwa Mungu, basi, nafurahi sana na kuwashirikisha nyinyi nyote furaha hiyo. 18Hali kadhalika nanyi mnapaswa kufurahi na kunishirikisha mimi furaha yenu.











"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: