Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana Tumshukuru Mungu wetu kila wakati Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Uabudiwe Jehovah,Uhimidiwe Yahweh,Matendo yako ni makuu mno, Matendo yako ni ya ajabu,Matendo yako yanatisha Hakuna kama wewe ee Mungu wetu.. Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni...!!
Moyo wangu umejaa mawazo mema: Namtungia mfalme shairi langu, ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi. Wewe u mzuri kuliko wanadamu wote, maneno yako ni fadhili tupu. Kwa hiyo Mungu amekubariki milele. Jifunge upanga wako, ewe shujaa! Wewe ni mtukufu na mwenye fahari. Songa mbele kwa utukufu upate ushindi, utetee ukweli na kulinda haki. Mkono wako utende mambo makuu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...
Mishale yako ni mikali, hupenya mioyo ya maadui za mfalme; nayo mataifa huanguka chini yako. Kiti chako cha enzi ni imara, chadumu milele kama cha Mungu. Wewe watawala watu wako kwa haki. Wapenda uadilifu na kuchukia uovu. Kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekuteua, na kukupa furaha kuliko wenzako. Mavazi yako yanukia marashi na udi, wanamuziki wakuimbia katika majumba ya pembe za ndovu. Binti za wafalme ni baadhi ya wanaokulaki, naye malkia amesimama kulia kwako, amevaa mapambo ya dhahabu safi ya Ofiri.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Mungu wetu ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Sikiliza binti, ufikirie! Tega sikio lako: Sahau sasa watu wako na jamaa zako. Uzuri wako wamvutia mfalme; yeye ni bwana wako, lazima umtii. Watu wa Tiro watakuletea zawadi; matajiri watataka upendeleo wako. Binti mfalme anaingia mzuri kabisa! Vazi lake limefumwa kwa nyuzi za dhahabu. Akiwa amevalia vazi la rangi nyingi, anaongozwa kwa mfalme, akisindikizwa na wasichana wenzake; nao pia wanapelekwa kwa mfalme. Kwa furaha na shangwe wanafika huko, na kuingia katika jumba la mfalme. Ee mfalme, utapata watoto wengi watakaotawala mahali pa wazee wako; utawafanya watawale duniani kote. Nitalifanya jina lako litukuzwe katika vizazi vyote, nayo mataifa yatakusifu daima na milele.
Baba wa Mbinguni tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na kuwalinda Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu Mungu wetu ukawatendee kama inavyokupendeza wewe Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea sawasawa na mapenzi yake.... Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima....
Nawapenda. |
No comments:
Post a Comment