Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Monday, 22 October 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;Yobu 20...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah ni siku/wiki nyingine tena Mungu wetu ametuchagua
na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Si kwamba sisi tumetenda mema sana wala si kwa nguvu zetu
si kwa utashi wetu wala si kwa akili zetu si kwamba sisi
ni wazuri mno si kwa uwezo wetu sisi kuwa hivi tulivyo leo hii
Ni kwa rehema/neema zake ni kwa mapenzi yake Mungu wetu....

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwa tayari kwa majukumu yetu
Sifa na Utukufu tunakurudshia Mungu wetu....!!




Wakati huo, mtawala Herode alisikia sifa za Yesu. Basi, akawaambia watumishi wake, “Mtu huyu ni Yohane Mbatizaji, amefufuka kutoka kwa wafu; ndiyo maana nguvu za miujiza zinafanya kazi ndani yake.” Herode ndiye aliyekuwa amemtia Yohane nguvuni, akamfunga minyororo na kumtia gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, ndugu yake. Kisa ni kwamba Yohane alikuwa amemwambia Herode, “Si halali kwako kuishi na huyo mwanamke!” Herode alitaka kumuua Yohane, lakini aliogopa watu kwa sababu kwao Yohane alikuwa nabii.


Tazama jana imepita ee Mungu wetu leo ni siku mpya na kesho ni siku nyingine

Jehovah tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
 Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizozifanya kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Jehovah usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote
Yahweh tunaomba ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona
Kwakupigwa kwake sisi tumepata kupona...

Katika sherehe za sikukuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti ya Herodia alicheza mbele ya wageni. Herode alifurahiwa, hata akaahidi kwa kiapo kumpa huyo msichana chochote atakachoomba. Naye, huku akichochewa na mama yake, akaomba, “Nipe papa hapa katika sinia kichwa cha Yohane Mbatizaji.” Mfalme alihuzunika, lakini kwa sababu ya kile kiapo chake na kwa sababu ya wale wageni karamuni, akaamuru apewe. Basi, Herode akatuma mtu gerezani amkate kichwa Yohane. Kichwa chake kikaletwa katika sinia, wakampa yule msichana, naye akampelekea mama yake. Wanafunzi wa Yohane wakaja, wakauchukua mwili wake, wakauzika. Kisha wakaenda kumpasha habari Yesu.
Yahweh tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Baba wa Mbinguni tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Yesu alipopata habari hiyo, aliondoka mahali pale kwa mashua, akaenda mahali pa faragha peke yake. Lakini watu walipata habari, wakamfuata kwa miguu toka mijini. Basi, aliposhuka pwani, aliona umati mkubwa wa watu, akawaonea huruma, akawaponya wagonjwa wao.

Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,wote wanaopotia magumu/majaribu mbalimbali
watoto wako wanaokuomba kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
 kila mmoja na mahitaji yake 
Yahweh tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Jehovah tunaomba ukawaokoe,ukawavushe salama na  kuwalinda
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Baba wa Mbinguni ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako
wakasimaie Neno lako nalo likaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kuomba kwetu
Baba wa Mbinguni ukapokee sala/maombi yetu
Mungu wetu ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami
Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea 
kama inavyompendeza yeye....
Nawapenda.



Hoja ya tatu ya Sofari

1Kisha Sofari, Mnaamathi, akajibu:
2“Fikira zangu zanifanya nikujibu,
wala siwezi kujizuia tena.
3Nasikia maonyo nisiyoweza kuvumilia,
lakini akili yangu yanisukuma nijibu.
4“Wewe labda umesahau jambo hili:
Kwamba tangu zamani Mungu alipomuumba mtu duniani,
5mwovu atajiona ameshinda kwa muda tu,
furaha yake asiyemcha Mungu ni ya muda mfupi tu!
6Mwovu aweza kufana hata kufikia mbingu,
kichwa chake kikafika kwenye mawingu,
7lakini atatupiliwa mbali kama mavi yake.
Waliopata kumjua watajiuliza: ‘Yuko wapi?’
8 Taz Hek 5:14 Atatoweka kama ndoto, asionekane tena,
atafutika kama maono ya usiku.
9Aliyemwona, hatamwona tena,
wala pale alipoishi hapatatambuliwa tena.
10Yeye mwenyewe itambidi kurudisha mali yake yote,
watoto wake wataomba huruma kwa maskini.
11Japo alijisikia amejaa nguvu za ujana,
lakini zote zitalala pamoja naye mavumbini.
12“Mdomoni mwake uovu ni mtamu kama sukari,
anauficha chini ya ulimi wake;
13hataki kabisa kuuachilia,
bali anaushikilia kinywani mwake.
14Lakini ufikapo tumboni huwa mchungu,
mkali kama sumu ya nyoka.
15Mwovu humeza mali haramu na kuitapika;
Mungu huitoa tumboni mwake.
16Anachonyonya mtu mwovu ni sumu ya nyoka;
atauawa kwa kuumwa na nyoka.
17Hataishi kuiona mitiririko ya fanaka,
wala vijito vya mafanikio na utajiri.
18Matunda ya jasho lake atayaachilia,
hatakuwa na uwezo wa kuyaonja,
19kwa sababu amewaangamiza maskini na kuwaacha,
amenyakua nyumba ambazo hakuzijenga.
20“Kwa vile ulafi wake hauna mwisho,
hataweza kuokoa chochote anachothamini.
21Baada ya kula hakuacha hata makombo,
kwa hiyo fanaka yake yote haitadumu.
22Kileleni mwa fanaka dhiki itamvamia,
balaa itamkumba kwa nguvu zote.
23Akiwa anajishughulisha kushibisha tumbo,
Mungu atamletea ghadhabu yake
imtiririkie kama chakula chake.
24Labda ataweza kuepa upanga wa chuma,
kumbe atachomwa na upanga wa shaba.
25Mshale utachomolewa kutoka mwilini mwake;
ncha yake itatolewa mgongoni mwake ikingaa,
vitisho vya kifo vitamvamia.
26Hazina zake zitaharibiwa,
moto wa ajabu utamteketeza;
kilichobaki nyumbani mwake kitateketezwa.
27Mbingu zitaufichua uovu wake,
dunia itajitokeza kumshutumu.
28Mali zake zitanyakuliwa
katika siku ya ghadhabu ya Mungu.
29Hicho ndicho apewacho mtu mwovu kutoka kwa Mungu,
ndicho mwovu alichopangiwa na Mungu.”



Yobu20;1-29

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: