Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 23 October 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;Yobu 21...





Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Yahweh..!Jehovah..! Adonai..!Elohim..!El Olam..!El Qanna..!
El Elyon..!El shaddai..!Emanueli...!-Mungu pamoja nasi...
Unastahili sifa Mungu wetu,Unastahili kuabudiwa Jehovah,
Unastahili kuhimidiwa Yahweh,Unastahili Kutukuzwa Baba wa Mbinguni....!



Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!



Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.” Yesu akawaambia, “Si lazima waende, wapeni nyinyi chakula.” Lakini wao wakamwambia, “Tunayo mikate mitano tu na samaki wawili.” Yesu akawaambia, “Nileteeni hapa.” Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. Watu wote wakala, wakashiba. Kisha wanafunzi wakakusanya mabaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. Jumla ya waliokula ilikuwa wanaume wapatao 5,000, bila kuhesabu wanawake na watoto.

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Mara, Yesu akawaamuru wanafunzi wake wapande mashua, wamtangulie ngambo ya ziwa wakati yeye anayaaga makundi ya watu. Baada ya kuwaaga watu, alipanda mlimani peke yake kusali. Ilipokuwa jioni, yeye alikuwa huko peke yake, na wakati huo ile mashua ilikwisha fika karibu katikati ya ziwa, lakini ilikumbwa na taabu kwa sababu upepo ulikuwa unaipinga. Usiku, karibu na mapambazuko, Yesu aliwaendea wanafunzi akitembea juu ya maji. Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji waliogopa sana, wakasema, “Ni mzimu!” Wakapiga yowe kwa hofu. Mara, Yesu akasema nao, “Tulieni, ni mimi. Msiogope!” Petro akamwambia, “Bwana, ikiwa ni wewe kweli, amuru nitembee juu ya maji nije kwako.” Yesu akasema, “Haya, njoo.” Basi, Petro akashuka kutoka ile mashua, akatembea juu ya maji, akamwendea Yesu. Lakini alipouona ule upepo, aliogopa, akaanza kuzama; akalia kwa sauti, “Bwana, niokoe!” Hapo, Yesu akaunyosha mkono wake, akamshika na kumwambia, “Ewe mwenye imani haba! Kwa nini uliona shaka?” Kisha wakapanda mashuani, na upepo ukatulia. Wote waliokuwa ndani ya mashua walimsujudia, wakasema, “Hakika wewe ni Mwana wa Mungu.”

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....



Yahweh  tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni

Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu
Baba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Walivuka ziwa, wakafika nchi ya Genesareti. Watu wa huko walipomtambua, wakaeneza habari pote katika sehemu hizo. Basi, wakamletea Yesu wagonjwa wote, wakamwomba awaruhusu waguse tu pindo la vazi lake. Nao wote waliomgusa walipona.

Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani, Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea
Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru
Ukawape macho ya rohoni ee Mungu wetu na masikio ya kusikia
sauti yako,Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika maisha yao,Upendo ukadumu kati yao
 

Baba wa Mbinguni tunayaweke haya yote mikono mwako
tukiamini Mungu wetu utawatendea sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina...!!



Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu
kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee
kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima
Nawapenda. 




Jibu la Yobu

1Kisha Yobu akajibu:
2“Sikilizeni kwa makini maneno yangu;
na hiyo iwe ndiyo faraja yenu.
3Nivumilieni, nami nitasema,
na nikisha sema endeleeni kunidhihaki.
4Je, mimi namlalamikia binadamu?
Ya nini basi, nikose uvumilivu?
5Niangalieni, nanyi mshangae,
fumbeni mdomo kwa mkono.
6Nikifikiri yaliyonipata nafadhaika
nafa ganzi mwilini kwa hofu.
7Kwa nini basi waovu wanaishi bado?
Mbona nguvu zao zaongezeka hata uzeeni?
8Huwaona watoto wao wakifanikiwa;
na wazawa wao wakipata nguvu.
9Kwao kila kitu ni salama bila hofu;
wala kiboko cha Mungu hakiwafikii.
10Naam, ng'ombe wao wote huongezeka,
huzaa bila matatizo yoyote.
11Watoto wao wachanga huwatembeza kama kundi;
na watoto wao hucheza ngoma;
12hucheza muziki wa ngoma na vinubi,
na kufurahia sauti ya filimbi.
13Huishi maisha ya fanaka
kisha hushuka kwa amani kuzimu.
14Humwambia Mungu, ‘Usitusumbue!
Hatutaki kujua matakwa yako.
15Mungu Mwenye Nguvu ni nini hata tumtumikie?
Tunapata faida gani tukimwomba dua?’
16Kufanikiwa kwao si kuko mikononi mwao,
wakiwa wamemweka Mungu mbali na mipango yao?21:16 tafsiri inayolingana na Septuaginta. Kiebrania: Shauri la waovu liko mbali nami.
17“Mara ngapi umepata kuona mwanga wa maisha ya mwovu umezimwa,
wakapata kukumbwa na maafa,
au Mungu amewahi kuwaangamiza kwa hasira yake?
18Hata hivyo, na wapeperushwe kama majani makavu,
wawe kama makapi yanayochukuliwa na dhoruba!
19“Nyinyi mwasema, ‘Mungu amewawekea watoto wao
adhabu ya watu hao waovu.’
Kwa nini hawalipizi wao wenyewe, wapate kutambua!
20Waone wao wenyewe wakiangamia;
waone wenyewe ghadhabu ya Mungu mwenye nguvu.
21Maana wakifa watajali nini juu ya wazawa wao,
wakati siku zao zitakapokuwa zimefika mwisho?
22Je, binadamu aweza kumfunza Mungu maarifa,
Mungu ambaye huwahukumu wakazi wa mbinguni?
23“Mtu hufa katika kilele cha ufanisi wake,
akiwa katika raha mustarehe na salama;
24amejaa mafuta tele mwilini,
na mifupa yake ikiwa bado na nguvu.
25Mwingine hufa na huzuni kubwa moyoni,
akiwa hajawahi kuonja lolote jema.
26Hata hivyo, wote hufa na kuzikwa,
wote hufunikwa na mabuu.
27“Sikilizeni! Mimi nayajua mawazo yenu yote,
na mipango yenu ya kunidharau.
28Eti mwauliza, ‘Iko wapi nyumba ya mkuu?
Iko wapi nyumba alimoishi mwovu?’
29“Je, hamjawauliza wapita njia,
mkakubaliana na ripoti yao?
30Mwovu husalimishwa siku ya maafa,
huokolewa siku ya ghadhabu!
31Ni nani atakayemshutumu mtu mwovu,
au atakayemlipa kwa yote aliyotenda?
32Anapochukuliwa kupelekwa kaburini,
kaburi lake huwekewa ulinzi.
33Watu wengi humfuata nyuma
na wengine wengi sana humtangulia.
Anapozikwa, udongo huteremshwa taratibu.
34Mtawezaje basi, kunifariji kwa maneno matupu?
majibu yenu hayana chochote ila uongo.”



Yobu21;1-34

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: