Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 5 October 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;Yobu 9..


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante

 kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Jehovah  Jireh..!Jehovah Nissi..!Jehovah Raah..!
Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shamlom..!
Emanuel-Mungu pamohja nasi..!!
Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni..!



Yesu alipofika huko alikuta Lazaro amekwisha kaa kaburini kwa siku nne. Kijiji cha Bethania kilikuwa karibu na Yerusalemu, umbali upatao kilomita tatu. Wayahudi wengi walikuwa wamefika kwa Martha na Maria kuwafariji kwa kifo cha kaka yao. Basi, Martha aliposikia kwamba Yesu alikuwa anakuja, akaenda kumlaki; lakini Maria alibaki nyumbani. Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa! Lakini najua kwamba hata sasa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa.” Yesu akamwambia, “Kaka yako atafufuka.” Martha akamjibu, “Najua kwamba atafufuka wakati wa ufufuo, siku ya mwisho.” Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uhai. Anayeniamini mimi hata kama anakufa, ataishi; na kila anayeishi na kuniamini, hatakufa kamwe. Je, waamini hayo?” Martha akamwambia, “Ndiyo Bwana! Mimi naamini kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.”





Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha
na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...





Baada ya kusema hayo, Martha alikwenda kumwita Maria, dada yake, akamwambia faraghani, “Mwalimu yuko hapa, anakuita.” Naye aliposikia hivyo, akainuka mara, akamwendea Yesu. Yesu alikuwa hajaingia kijijini, ila alikuwa bado mahali palepale Martha alipomlaki. Basi, Wayahudi waliokuwa nyumbani pamoja na Maria wakimfariji walipomwona ameinuka na kutoka nje ghafla, walimfuata. Walidhani alikuwa anakwenda kaburini kuomboleza.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Mungu wetu

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...




Basi, Maria alipofika mahali pale Yesu alipokuwa na kumwona, alipiga magoti, akamwambia, “Bwana, kama ungalikuwa hapa, kaka yangu hangalikufa!” Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye wanalia pia, alijawa na huzuni na kufadhaika moyoni. Kisha akawauliza, “Mlimweka wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo uone.” Yesu akalia machozi. Basi, Wayahudi wakasema, “Tazameni jinsi alivyompenda!” Lakini baadhi yao wakasema, “Je, huyu aliyemfumbua macho yule kipofu, hakuweza kumfanya Lazaro asife?”




Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba  ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu  unajua haja za mioyo ya kila mmoja
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.


Jibu la Yobu
1Kisha Yobu akajibu:
2 Taz Yobu 4:17 “Kweli najua hivyo ndivyo ilivyo.
Lakini mtu awezaje kuwa mwema mbele ya Mungu?
3Kama mtu angethubutu kushindana naye,
hataweza kufika mbali;
hata kujibu swali moja kati ya elfu.
4Yeye ni mwenye hekima mno na nguvu nyingi,
nani aliyepingana naye, akashinda?
5Yeye huiondoa milima bila yenyewe kutambua,
huibomolea mbali kwa hasira yake.
6Yeye huitikisa dunia kutoka mahali pake,
na nguzo zake zikatetemeka.
7 Taz Bar 2:34-35 Huliamuru jua lisichomoze
huziziba nyota zisiangaze.
8Yeye peke yake alizitandaza mbingu,
na kuyakanyaga mawimbi ya bahari.9:8 na … bahari: Au alilikanyaga dude la baharini mgongoni.
9 Taz Yobu 38:31, Amo 5:8 Ndiye aliyezifanya nyota angani:
Dubu, Orioni, Kilimia, na nyota za kusini.
10Ndiye atendaye makuu yasiyoeleweka,
mambo ya ajabu yasiyo na idadi.
11Loo! Hupita karibu nami nisimwone,
kisha huenda zake bila ya mimi kumtambua.
12Tazama! Yeye huchukua anachotaka;
nani awezaye kumzuia?
Nani awezaye kumwuliza: ‘Unafanya nini?’
13“Mungu hatazuia hasira yake;
chini yake wainama kwa hofu Rahabu9:13 Rahabu: Taz 7:12 na maelezo yake. na wasaidizi wake.
14Nitawezaje basi kumjibu Mungu?
Nitachagua wapi maneno ya kumwambia?
15Ingawa sina hatia, siwezi kumjibu.
Lazima kumwomba anihurumie huyo mshtaki wangu.
16Hata kama ningemwita naye akajibu,
nisingeweza kuamini kuwa ananisikiliza.
17Yeye huniponda kwa dhoruba;
huongeza majeraha yangu bila sababu.
18Haniachi hata nipumue;
maisha yangu huyajaza uchungu.
19Kama ni kushindana, yeye ana nguvu mno!
Na kama ni kutafuta juu ya haki,
nani atakayemleta9:19 atakayemleta: Makala ya Kiebrania: Atanileta. mahakamani?
20Ingawa sina hatia, maneno yangu yenyewe yangenihukumu;
ingawa sina lawama, angenithibitisha kuwa mpotovu.
21Sina lawama, lakini sijithamini.
Nayachukia maisha yangu.
22Yote ni mamoja, kwa hiyo nasema;
Mungu huwaangamiza wema na waovu.
23Maafa yaletapo kifo cha ghafla,
huchekelea balaa la wasio na hatia.
24Nchi ikitiwa watu waovu katika utawala wa mwovu,
Mungu huyafumba macho ya mahakimu wake!
Kama si yeye afanyaye hivyo, ni nani basi?
25“Siku zangu zaenda mbio kuliko mpiga mbio;
zinakimbia bila kuona faida.
26Zapita kasi kama mashua ya matete;
kama tai anayerukia mawindo yake.
27Nasema: ‘Nitasahau lalamiko langu,
niondoe uso wangu wa huzuni na kuwa na furaha!’
28Lakini nayaogopa maumivu yangu yote,
kwani najua Mungu hataniona kuwa sina hatia.
29Ikiwa nitahukumiwa kuwa na hatia,
ya nini basi nijisumbue bure?
30Hata kama nikitawadha kwa theluji,
na kujitakasa mikono kwa sabuni,
31hata hivyo, atanitumbukiza shimoni kwenye uchafu,
na mavazi yangu yataniona kuwa kinyaa.
32Mungu si mtu kama mimi niweze kumjibu,
hata tuweze kwenda mahakamani pamoja.
33Hakuna msuluhishi kati yetu,
ambaye angeamua kati yetu sisi wawili.
34Mungu na aniondolee hiyo fimbo ya kunipiga,
na kitisho chake kisinitie hofu!
35Hapo ningeweza kusema bila kumwogopa;
kwani sivyo nilivyo nafsini mwangu.



Yobu9;1-35

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: