Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 16 November 2018

Kikombe Cha Asubuhi ;Yobu 39...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante

 kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Jehovah  Jireh..!Jehovah Nissi..!Jehovah Raah..!
Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shamlom..!
Emanuel-Mungu pamohja nasi..!!
Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni..!

Habari Njema ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu. Ilianza kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Mungu alisema, ‘Namtuma mjumbe wangu akutangulie, ambaye atakutayarishia njia yako.’ Sauti ya mtu anaita jangwani: ‘Mtayarishieni Bwana njia yake, nyosheni barabara zake.’”

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha

na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona...

Yohane Mbatizaji alitokea jangwani, akahubiri kwamba watu watubu na kubatizwa ili Mungu awasamehe dhambi zao. Watu kutoka sehemu zote za Yudea na wenyeji wote wa Yerusalemu walimwendea, wakaziungama dhambi zao, naye akawabatiza katika mto Yordani.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu

Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Mungu wetu

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Yohane alikuwa amevaa vazi lililofumwa kwa manyoya ya ngamia, na ukanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. Naye alihubiri akisema, “Baada yangu anakuja mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, ambaye mimi sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.”


Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba  ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu  unajua haja za mioyo ya kila mmoja
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

1“Je, wajua mbuzi wa milimani huzaa lini,
au umewahi kuona kulungu akizaa?
2Je, wajua huchukua mimba kwa muda gani,
au siku yenyewe ya kuzaa waijua?
3“Wajua wakati watakapochuchumaa kuzaa,
wakati wa kuzaa watoto wao?
4Watoto wao hupata nguvu,
hukua hukohuko porini,
kisha huwaacha mama zao na kwenda zao.
5“Nani aliyemwacha huru pundamwitu?
Nani aliyewaacha waende kwa kuwafungua?
6Mimi niliwapa jangwa liwe makao yao,
mbuga zenye chumvi kuwa makazi yao.
7Hujitenga kabisa na makelele ya miji,
hasikilizi kelele ya kumfanyisha kazi.
8Hutembeatembea milimani kupata malisho,
na kutafuta chochote kilicho kibichi.
9“Je, nyati atakubali kukutumikia?
Au je, atakubali kulala zizini mwako?
10Je, waweza kumfunga nyati kamba kulima shamba,
au avute jembe la kulimia?
11Je, utamtegemea kwa kuwa ana nguvu nyingi
na kumwacha akufanyie kazi zako nzito?
12Je, wamtazamia nyati akuvunie mavuno yako,
na kuleta nafaka mahali pa kupuria?
13“Mbuni hupigapiga mabawa yake kwa madaha,
lakini hawezi kuruka kama korongo.39:13 aya hii katika Kiebrania si dhahiri.
14Mbuni huyaacha mayai yake juu ya ardhi
ili yapate joto mchangani;
15lakini hajui kama yanaweza kukanyagwa,
au kuvunjwa na mnyama wa porini.
16Mbuni huwatendea wanawe ukatili kama si wake,
hata kazi yake ikiharibika yeye hana wasiwasi;
17kwa sababu nilimfanya asahau hekima yake,
wala sikumpa sehemu yoyote ya akili.
18Lakini akianza kukimbia,
humcheka hata farasi na mpandafarasi.
19“Je, Yobu, ndiwe uliyewapa farasi nguvu,
ukawavika shingoni manyoya marefu?
20Je, ni wewe unayemfanya farasi aruke kama nzige?
Mlio wake wa maringo ni wa ajabu!
21Huparapara ardhi mabondeni kwa pupa;
hukimbilia kwenye mapigano kwa nguvu zake zote.
22Farasi huicheka hofu, na hatishiki;
wala upanga hauwezi kumrudisha nyuma.
23Silaha wachukuazo wapandafarasi,
hugongana kwa sauti na kungaa juani.
24Farasi husonga mbele, akitetemeka kwa hasira;
tarumbeta iliapo, yeye hasimami.
25Kila ipigwapo tarumbeta, yeye hutoa sauti;
huisikia harufu ya vita toka mbali,
huusikia mshindo wa makamanda
wakitoa amri kwa makelele.
26“Je, mwewe amejifunza kwako jinsi ya kuruka,
na kunyosha mabawa yake kuelekea kusini?
27Je, tai hupaa juu kwa amri yako,
na kuweka kiota chake juu milimani?
28Tai hufanya makazi yake juu ya miamba mirefu,
na ncha kali za majabali ndizo ngome zake.
29Kutoka huko huotea mawindo,
macho yake huyaona kutoka mbali.
30 Taz Mat 24:28; Luka 17:37 Makinda yake hufyonza damu;
pale ulipo mzoga ndipo alipo tai.”


Yobu39;1-30

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: