Sauti ya Mungu katika dhoruba
(Zaburi ya Daudi)
1 Taz Zab 96:7-9 Mpeni Mwenyezi-Mungu heshima enyi viumbe vya mbinguni,
semeni Mwenyezi-Mungu ni mtukufu na mwenye nguvu.
2Semeni jina la Mwenyezi-Mungu ni tukufu.
Mwabuduni katika mahali pake patakatifu.29:2 mahali pake patakatifu: Tafsiri ya aya 1-2 ni ngumu. Hata hivyo wazo muhimu katika aya hizi ni kwamba watu wanaitwa kukiri ukuu na utukufu wa Mungu. Katika aya zifuatazo huo utukufu na ukuu wa Mungu unazingatiwa na kusisitizwa.
3Sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya maji;
Mungu mtukufu angurumisha radi,
sauti ya Mwenyezi-Mungu yasikika juu ya bahari!
4Sauti ya Mwenyezi-Mungu ina nguvu,
sauti ya Mwenyezi-Mungu imejaa fahari.
5Sauti ya Mwenyezi-Mungu huvunja mierezi;
Mwenyezi-Mungu avunja mierezi ya Lebanoni.
6Huirusha milima ya Lebanoni kama ndama,
milima ya Sirioni29:6 Sirioni: Jina lingine la Hermoni. kama mwananyati.
7Sauti ya Mwenyezi-Mungu hutoa miali ya moto.
8Sauti ya Mwenyezi-Mungu hutetemesha jangwa,
Mwenyezi-Mungu hutetemesha jangwa la Kadeshi.
9Sauti ya Mwenyezi-Mungu huitikisa mivule,29:9 huitikisa mivule: Kiebrania: Humfanya paa azae.
hukwanyua majani ya miti msituni,
na hekaluni mwake wote wasema:
“Utukufu kwa Mungu!”
10Mwenyezi-Mungu ameketi juu ya gharika;
Mwenyezi-Mungu ni mfalme atawalaye milele.
11Mwenyezi-Mungu na awape watu wake nguvu!
Mwenyezi-Mungu na awabariki watu wake kwa amani!
Zaburi29;1-11
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
1 comment:
I have read so many articles about the blogger
lovers however this article is really a pleasant paragraph, keep it up.
Post a Comment