|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!! Baada ya hayo, Yesu alipitia mijini na vijijini akitangaza Habari Njema za ufalme wa Mungu. Wale kumi na wawili waliandamana naye. Pia wanawake kadhaa ambao Yesu alikuwa amewatoa pepo wabaya na kuwaponya magonjwa, waliandamana naye. Hao ndio akina Maria (aitwaye Magdalene), ambaye alitolewa pepo wabaya saba; Yoana mke wa Kuza, mfanyakazi mkuu wa Herode; Susana na wengine kadhaa. Hao wanawake walikuwa wakiwatumikia kwa mali yao wenyewe. Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Wakati mmoja kundi kubwa la watu lilikuwa linakusanyika, na watu walikuwa wanamjia Yesu kutoka kila mji. Naye akawaambia mfano huu: “Mpanzi alikwenda kupanda mbegu zake. Alipokuwa akipanda hizo mbegu, nyingine zilianguka njiani, na wapita njia wakazikanyaga na ndege wakazila. Nyingine zilianguka penye mawe, na baada ya kuota zikanyauka kwa kukosa maji. Nyingine zilianguka kati ya miti ya miiba. Ile miti ya miiba ilipoota ikazisonga. Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikaota na kuzaa asilimia mia.” Baada ya kusema hayo, akapaza sauti, akasema, “Mwenye masikio na asikie!”
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetuBaba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza weweRoho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Wanafunzi wake Yesu wakamwuliza maana ya mfano huo. Naye akajibu, “Nyinyi mmejaliwa kujua siri za ufalme wa Mungu, lakini hao wengine sivyo; ila hao huambiwa kwa mifano, ili wakitazama wasiweze kuona, na wakisikia wasifahamu.
Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani, Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu, wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru Ukawape macho ya rohoni ee Mungu wetu na masikio ya kusikia sauti yako,Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika maisha yao,Upendo ukadumu kati yao Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mikononi mwako,Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina!! Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake Nawapenda. |
Sifa kwa wema wa Mungu
(Zaburi ya Daudi alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki)
1Nitamtukuza Mwenyezi-Mungu nyakati zote,
sitaacha kamwe kuzitamka sifa zake.
2Mimi nitaona fahari juu ya Mwenyezi-Mungu,
wanyonge wasikie na kufurahi.
3Mtukuzeni Mwenyezi-Mungu pamoja nami,
sote pamoja tulisifu jina lake.
4Nilimwomba Mwenyezi-Mungu naye akanijibu,
na kuniondoa katika hofu zangu zote.
5Mgeukieni Mungu mpate kufurahi;
nanyi hamtaaibishwa kamwe.
6Maskini alimlilia Mwenyezi-Mungu, naye akamsikia,
na kumwokoa katika taabu zake zote.
7Malaika wa Mwenyezi-Mungu huwalinda wote wamchao,
na kuwaokoa katika hatari.
8 Taz 1Pet 2:3 Jaribuni mwone Mwenyezi-Mungu alivyo mwema.
Heri mtu anayekimbilia usalama kwake.
9Mcheni Mwenyezi-Mungu enyi watakatifu wake;
maana wenye kumcha hawatindikiwi na kitu.
10Hata wanasimba hutindikiwa na kuona njaa;
lakini wanaomtafuta Mwenyezi-Mungu hawakosi chochote chema.
11Njoni enyi vijana mkanisikilize,
nami nitawafundisha kumcha Mwenyezi-Mungu.
12 Taz 1Pet 3:10-12 Je, watamani kufurahia maisha,
kuishi maisha marefu na kufurahia mema?
13Basi, acha kusema mabaya,
na kuepa kusema uongo.
14Jiepushe na uovu, utende mema;
utafute amani na kuizingatia.
15Mwenyezi-Mungu huwaangalia waadilifu,
na kusikiliza malalamiko yao;
16lakini huwapinga watu watendao maovu,
awafutilie mbali kutoka duniani.
17Waadilifu wakimlilia Mwenyezi-Mungu yeye huwasikia,
na kuwaokoa katika taabu zao zote.
18Mwenyezi-Mungu yu karibu na waliokufa moyo;
huwaokoa wote waliokata tamaa kabisa.
19Mateso ya mwadilifu ni mengi,
lakini Mwenyezi-Mungu humwokoa kutoka yote.
20 Taz Yoh 19:36 Huvilinda viungo vya mwili wake wote,
hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.
21Ubaya huwaletea waovu kifo;
wanaowachukia waadilifu wataadhibiwa.
22Mwenyezi-Mungu huokoa maisha ya watumishi wake,
wote wanaomkimbilia hawataadhibiwa.
Zaburi34;1-22
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment