|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Yesu Kristo ndiye aliyekuja kwa maji ya ubatizo wake na kwa damu ya kifo chake. Hakuja kwa maji tu, bali kwa maji na kwa damu. Naye Roho anashuhudia kwamba ni kweli, kwani Roho ni ukweli.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Basi, wako mashahidi watatu: Roho, maji na damu; na ushahidi wa hawa watatu waafikiana. Ikiwa twaukubali ushahidi wa binadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; na huu ndio ushahidi alioutoa Mungu mwenyewe juu ya Mwanae.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetuBaba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza weweRoho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Anayemwamini Mwana wa Mungu anao ushahidi huo ndani yake; lakini asiyemwamini Mungu, anamfanya yeye kuwa mwongo, maana hakuamini ushahidi alioutoa Mungu juu ya Mwanae. Na, ushahidi wenyewe ndio huu: Mungu alitupatia uhai wa milele, na uhai huo uko kwa Bwana. Yeyote aliye na Mwana wa Mungu anao uhai huo; asiye na Mwana wa Mungu, hana uhai.
Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani, Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu, wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru Ukawape macho ya rohoni ee Mungu wetu na masikio ya kusikia sauti yako,Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika maisha yao,Upendo ukadumu kati yao Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mikononi mwako,Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina!! Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake Nawapenda. |
Utenzi wa sifa
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi)
1Nilimngojea Mwenyezi-Mungu kwa uvumilivu,
akanielekea na kukisikia kilio changu.
2Aliniondoa katika shimo la hatari,
alinitoa katika matope ya dimbwi,
akanisimamisha salama juu ya mwamba,
na kuziimarisha hatua zangu.
3Alinifundisha wimbo mpya,
wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa,
na kumtumainia Mwenyezi-Mungu.
4Heri mtu anayemtumainia Mwenyezi-Mungu;
mtu asiyejiunga na watu wenye majivuno,
watu waliopotoka kwa kuabudu miungu ya uongo.
5Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu, umetufanyia mengi ya ajabu,
na mipango yako juu yetu haihesabiki;
hakuna yeyote aliye kama wewe.
Kama ningeweza kusimulia hayo yote,
idadi yake ingenishinda.
6 Taz Ebr 10:5-7 Wewe hutaki tambiko wala sadaka,
tambiko za kuteketeza wala za kuondoa dhambi;
lakini umenipa masikio nikusikie.
7Ndipo niliposema: “Niko tayari;
ninayotakiwa kufanya yameandikwa katika kitabu cha sheria;
8kutimiza matakwa yako, ee Mungu wangu ni furaha yangu,
sheria yako naishika kwa moyo wangu wote!”
9Nimesimulia habari njema za ukombozi,
mbele ya kusanyiko kubwa la watu.
Kama ujuavyo ee Mwenyezi-Mungu,
mimi sikujizuia kuitangaza.
10Sikuuficha moyoni mwangu ukombozi ulionijalia,
nimetangaza daima kuwa wewe ni mwokozi mwaminifu;
sikulificha kusanyiko kubwa la watu
fadhili zako na uaminifu wako.
11Ee Mwenyezi-Mungu, usininyime huruma yako!
Fadhili zako na uaminifu wako vinihifadhi daima.
Sala ya kuomba msaada
(Zaburi 70)
12Maafa yasiyohesabika yanizunguka,
maovu yangu yanikaba hata siwezi kuona;
ni mengi kuliko nywele kichwani mwangu,
nami nimevunjika moyo.
13Upende ee Mwenyezi-Mungu kuniokoa;
ee Mwenyezi-Mungu, uje haraka kunisaidia.
14Wanaonuia kuniangamiza,
na waaibike na kufedheheka!
Hao wanaotamani niumie,
na warudi nyuma na kuaibika!
15Hao wanaonisimanga,
na wapumbazike kwa kushindwa kwao!
16Lakini wote wale wanaokutafuta
wafurahi na kushangilia kwa sababu yako.
Wapendao wokovu wako,
waseme daima: “Mwenyezi-Mungu ni Mkuu!”
17Mimi ni maskini na fukara, ee Bwana;
lakini ee Bwana wewe wanikumbuka.
Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
uje, ee Mungu wangu, usikawie!
Zaburi40;1-17
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment