|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu wetu katika yote...
Asante Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetuAsante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu
Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni Neema yako yatutosha Mungu wetu..!
Sikilizeni anachosema Mwenyezi-Mungu: “Wewe nabii, nenda ukailalamikie milima, navyo vilima visikie sauti yako.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti, Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.....
Sikilizeni kesi ya Mwenyezi-Mungu enyi milima, sikilizeni enyi misingi ya kudumu ya dunia! Mwenyezi-Mungu anayo kesi dhidi ya watu wake. Yeye atatoa mashtaka dhidi ya Waisraeli.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe
Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Mungu wetu Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama inavyokupendeza wewe Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Enyi watu wangu, nimewatendea nini? Nimewachosha kwa kitu gani? Nijibuni! Mimi niliwatoa nchini Misri; niliwakomboa kutoka utumwani; niliwapeni Mose, Aroni na Miriamu kuwaongoza. Enyi watu wangu, kumbukeni njama za Balaki mfalme wa Moabu, na jinsi Balaamu mwana wa Beori alivyomjibu. Kumbukeni yaliyotukia njiani kati ya Shitimu na Gilgali. Kumbukeni mtambue matendo yangu ya kuwaokoa!”
Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu Yahweh tunaomba ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake Mungu wetu unajua haja za mioyo ya kila mmoja Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao Jehovah ukaonekane katika maisha yao Nuru yako ikaangaze katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina....!!!
Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba ukae nanyi daima.... Nawapenda. |
KITABU CHA PILI
(Zaburi 42–72)
Sala ya Mkimbizi42-43 Zaburi 42 na 43 bila shaka zilikuwa wimbo mmoja hapo awali kama inavyoonekana dhahiri katika marudio ya aya ya 6 Zab 42 katika aya ya 11 na katika Zab 43 aya ya 5.
(Kwa Mwimbishaji. Utenzi wa Wakorahi)
1Kama paa atamanivyo maji ya kijito,
ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu!
2Naona kiu ya Mungu, kiu ya Mungu aliye hai.
Nitafika lini kwake na kuuona uso wake?
3Machozi yamekuwa chakula changu mchana na usiku,
waliponiambia kila siku: “Yuko wapi Mungu Wako!”
4Nakumbuka tena mambo haya
kwa majonzi moyoni mwangu:
Jinsi nilivyokwenda na umati wa watu,
nikawaongoza kwenda nyumbani kwa Mungu
wakipiga vigelegele vya shukrani;
umati wa watu wakifanya sherehe!
5Mbona nasononeka hivyo moyoni?
Kwa nini nahangaika hivyo ndani mwangu?
Nitamtumainia Mungu,
maana nitamsifu tena
yeye aliye msaada wangu na Mungu wangu.
6Nimesongwa na huzuni moyoni mwangu,
kwa hiyo ninakukumbuka wewe, ee Mungu,
kutoka katika eneo la Yordani,
kutoka mlima Hermoni na Mizari.
7Nimeporomoshewa mafuriko ya maji
mafuriko ya maji yaja karibu
nayo yaita maporomoko mapya.
Mawimbi na mapigo yako yamenikumba.
8Mwenyezi-Mungu atanijalia fadhili zake mchana;
nami nimwimbie wimbo wa sifa usiku,
nimwombe Mungu anipaye uhai.
9Namwambia Mungu, mwamba wangu:
“Kwa nini umenisahau?
Yanini niende huko na huko nikiomboleza
kwa kudhulumiwa na adui yangu?”
10Nimepondwa kwa matukano yao,
wanaponiuliza kila siku:
“Yuko wapi, Mungu wako!”
11Mbona nasononeka hivyo moyoni?
Kwa nini nahangaika hivyo?
Nitamtumainia Mungu,
maana nitamsifu tena Mungu,
aliye msaada wangu na Mungu wangu.
Zaburi42;1-11
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment