|
Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?
Tumshukuru Mungu katika yote....
Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana Mungu wa walio hai,Mungu mwenye huruma,Mungu wa upendo Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...Asante kwa wema na fadhili zako kwetu Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote Asante kwa kutuchagua tena na kutupa kibali cha kuendelea kuiona leo hii Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: “Tajiri mmoja alikuwa na karani wake. Huyu karani alichongewa kwamba alitumia ovyo mali ya tajiri wake. Yule tajiri akamwita, akamwambia: ‘Ni mambo gani haya ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu, kwa maana huwezi kuwa karani tena.’
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....
Yule karani akafikiri: ‘Bwana wangu amenifukuza kazi ya ukarani; nitafanya nini? Kwenda kulima siwezi; kwenda kuombaomba kama maskini ni aibu. Naam, najua la kufanya, ili nitakapofukuzwa kazi, watu waweze kunikaribisha nyumbani kwao.’
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....
Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu, watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetuBaba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza weweRoho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....
Basi, akawaita wadeni wa bwana wake, mmojammoja, akamwambia yule wa kwanza: ‘Unadaiwa kiasi gani na bwana wangu?’ Yeye akamjibu: ‘Mapipa 100 ya mafuta ya zeituni.’ Yule karani akamwambia: ‘Chukua hati yako ya deni, keti haraka, andika hamsini.’ Kisha akamwuliza mdeni mwingine: ‘Wewe unadaiwa kiasi gani?’ Yeye akamjibu: ‘Magunia 100 ya ngano.’ Yule karani akamwambia: ‘Chukua hati yako ya deni, andika themanini.’ “Basi, yule bwana akamsifu huyo karani asiye mwaminifu, kwa kuwa alitumia busara. Kwa maana watu wa dunia hii wana busara zaidi na mambo yao kuliko watu wa mwanga.”
Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani, Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu, wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru Ukawape macho ya rohoni ee Mungu wetu na masikio ya kusikia sauti yako,Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika maisha yao,Upendo ukadumu kati yao Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako,kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!
Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami, Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake...
Nawapenda.
|
Ibada ya kweli
(Zaburi ya Asafu)
1Mungu wa nguvu50:1 Mungu wa nguvu: Hivyo, kadiri ya makala ya Kiebrania; au Mungu Mkuu. Mwenyezi-Mungu, amenena,
amewaita wakazi wa dunia,
tokea mawio ya jua hadi machweo yake.
2Kutoka Siyoni, mji mzuri mno,
Mungu anajitokeza, akiangaza.
3Mungu wetu anakuja, na sio kimyakimya:
Moto uunguzao wamtangulia,
na dhoruba kali yamzunguka.
4Kutoka juu anaziita mbingu na dunia;
zishuhudie akiwahukumu watu wake:
5“Nikusanyieni waaminifu wangu,
waliofanya agano nami kwa tambiko!”
6Mbingu zatangaza uadilifu wa Mungu;
kwamba Mungu mwenyewe ni hakimu.
7“Sikilizeni watu wangu, ninachosema!
Israeli, natoa ushahidi dhidi yako.
Mimi ni Mungu! Mimi ni Mungu wako!
8Sikukaripii kwa sababu ya tambiko zako;
hujaacha kunitolea tambiko za kuteketeza.
9Kwa kweli sina haja na fahali wa zizi lako,
wala beberu wa mifugo yako;
10maana wanyama wote porini ni mali yangu,
na maelfu ya wanyama milimani ni wangu.
11Ndege wote wa mwitu ni mali yangu,
na viumbe vyote hai mashambani ni vyangu.
12Kama ningeona njaa singekuambia wewe,
maana ulimwengu na vyote vilivyomo ni vyangu.
13Je, wadhani nala nyama ya fahali,
au Kunywa damu ya mbuzi?
14Shukrani iwe ndio tambiko yako kwa Mungu
mtimizie Mungu Aliye Juu ahadi zako.
15Uniite wakati wa taabu,
nami nitakuokoa, nawe utaniheshimu.”
16Lakini Mungu amwambia mtu mwovu:
“Ya nini kuzitajataja tu sheria zangu?
Kwa nini unasemasema juu ya agano langu?
17Wewe wachukia kuwa na nidhamu,
na maneno yangu hupendi kuyafuata.
18Ukimwona mwizi unaandamana naye,
na wazinzi unashirikiana nao.
19Uko tayari daima kunena mabaya;
kazi ya ulimi wako ni kutunga uongo.
20Wakaa kitako kumsengenya binadamu mwenzako,
naam, kumchongea ndugu yako mwenyewe.
21Umefanya hayo yote nami nimenyamaa.
Je, wadhani kweli mimi ni kama wewe?
Lakini sasa ninakukaripia,
ninakugombeza waziwazi.
22“Fikirini vizuri jambo hili, enyi msionijali,
la sivyo nitawaangamizeni,
wala hapatakuwa na wa kuwaokoeni.
23Anayenipa shukrani kama tambiko yake,
huyo ndiye anayeniheshimu;
yeyote anayedumu katika njia yangu,
huyo ndiye nitakayemwokoa.”
Zaburi50;1-23
Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)
"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.
No comments:
Post a Comment