Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 31 January 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 51...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo..
Yahweh..!Jehovah..! Adonai..!Elohim..!El Olam..!El Qanna..!
El Elyon..!El shaddai..!Emanueli...!-Mungu pamoja nasi...
Unastahili sifa Mungu wetu,Unastahili kuabudiwa Jehovah,
Unastahili kuhimidiwa Yahweh,Unastahili Kutukuzwa Baba wa Mbinguni....!


Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, wawapokeeni katika makao ya milele.

Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribu Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Yeyote aliye mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu katika mambo makubwa; na yeyote asiye mwaminifu katika mambo madogo, hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa. Kama basi, nyinyi si waaminifu kuhusu mali mbaya za dunia, ni nani atakayewakabidhi zile mali za kweli? Na kama nyinyi si waaminifu kuhusu mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewakabidhi mali yenu wenyewe?


Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji

Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni
tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....



Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako

Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka...
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu...
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako

Yahwe tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetu Baba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza weweRoho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

“Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali pamoja.”

Tazama watoto wako wanaokutafuta/kukuomba kwa bidii na imani, Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukaonekane katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea
Kufuata njia zako nazo zikawaweke huru
Ukawape macho ya rohoni ee Mungu wetu na masikio ya kusikia
sauti yako,Ukawaokoe na kuwalinda,ukawaponye kimwili na kiroho
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao,Amani ikatawale katika maisha yao,Upendo ukadumu kati yao

Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako tukiamini Mungu wetu utawatendea sawasawa na mapenzi yako 
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele Amina...!!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwanami/kunisoma Mungu Baba aendelee
kuwabariki na kuwatendea kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na Upendo wa Mungu wa Mungu Baba ukae nanyi daima
Nawapenda.

Kuomba msamaha
(Kwa Mwimbishaji. Zaburi ya Daudi baada ya kukemewa na nabii Nathani kwa kosa lake na Bathsheba)
1Nihurumie, Ee Mungu,
kadiri ya fadhili zako;
ufutilie mbali makosa yangu,
kadiri ya wingi wa huruma yako.
2Unioshe kabisa hatia yangu;
unisafishe dhambi yangu.
3Nakiri kabisa makosa yangu,
daima naiona waziwazi dhambi yangu.
4 Taz Rom 3:4 Nimekukosea wewe peke yako,
nimetenda yaliyo mabaya mbele yako.
Uamuzi wako ni wa haki
hukumu yako haina lawama.
5Mimi ni mkosefu tangu kuzaliwa kwangu,
mwenye dhambi tangu tumboni mwa mama yangu.
6Wewe wataka unyofu wa ndani;
hivyo nifundishe hekima moyoni.
7Unitakase kwa husopo,51:7 Husopo: Husopo ni jina la mmea mmoja wa majani madogo laini ambao ulitumiwa katika ibada za kutakasa. nitakate;
unioshe niwe mweupe pe.
8Nijaze furaha na shangwe,
nifurahishe tena, mimi ambaye uliniponda.
9Ugeuke, usiziangalie dhambi zangu;
uzifute hatia zangu zote.
10Uniumbie moyo safi, ee Mungu,
uweke ndani yangu roho mpya na thabiti.
11Usinitupe mbali nawe;
usiniondolee roho yako takatifu.
12Unifanye nifurahi tena kwa kuniokoa,
utegemeze ndani yangu moyo wa utii.
13Hapo nitawafunza wakosefu njia yako,
nao wenye dhambi watarudi kwako.
14Uniokoe na hatia ya umwagaji damu,
ee Mungu, Mungu mwokozi wangu,
nami nitaimba kwa sauti kuwa umeniokoa.
15Uniwezeshe kusema, ee Bwana,
midomo yangu itangaze sifa zako.
16Kwa kweli wewe hupendezwi na tambiko,
ama sivyo mimi ningalikutolea.
Wewe huna haja na tambiko za kuteketezwa.
17tambiko yangu kwako ee Mungu, ni moyo mnyofu;
wewe, ee Mungu, hukatai moyo mnyofu na mtiifu.
18Ee Mungu, upende kuutendea mema mji wa Siyoni;
uzijenge tena upya kuta za mji wa Yerusalemu.
19Hapo utapendezwa na tambiko za kweli:
Sadaka za kuteketezwa na za kuteketezwa nzima;
mafahali watatolewa tambiko madhabahuni pako.



Zaburi51;1-19

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: