Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 12 February 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 59...


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante

 kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Jehovah  Jireh..!Jehovah Nissi..!Jehovah Raah..!
Jehovah Rapha..!Jehovah Shammah..!Jehovah Shamlom..!
Emanuel-Mungu pamohja nasi..!!
Neema yako yatutosha Baba wa Mbinguni..!

watu wafurahiao kutenda maovu, na kupendezwa na upotovu wa maovu; watu ambao mienendo yao imepotoka, nazo njia zao haziaminiki.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona.....

Hekima itakuwezesha kumkwepa mwanamke mwasherati, mwanamke malaya wa maneno matamu; mwanamke amwachaye mwenzi wa ujana wake, na kulisahau agano la Mungu wake. Nyumba yake yaelekea kuzimu, njia zake zinakwenda ahera. Yeyote amwendeaye kamwe harudi, wala hairudii tena njia ya uhai.

Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu wetu tunaomba ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya Baba wa Mbinguni ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo Mungu wetu

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Kwa hiyo utafuata mfano wa watu wema, na kuzingatia mienendo ya waadilifu. Maana wanyofu wataipata nchi, na waaminifu watadumu ndani yake. Lakini waovu wataondolewa nchini, na wenye hila watangolewa humo.
Tazama wenye shida/tabu,watoto wako wanaokutafuta kwa bidii na imani
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
Yahweh tunaomba  ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu  unajua haja za mioyo ya kila mmoja
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Jehovah ukaonekane katika maisha yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.


Sala ya kuomba ulinzi wa Mungu
(Kwa Mwimbishaji: Mtindo “Usiharibu”. Utenzi wa Daudi wakati Shauli alipotuma wapelelezi wamuue)
1Ee Mungu wangu, uniokoe na maadui zangu;
unikinge na hao wanaonishambulia.
2Uniokoe na hao wanaotenda maovu;
unisalimishe kutoka kwa hao wauaji!
3Tazama! Wananivizia waniue;
watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu.
4Bila ya kosa, hatia au dhambi yangu,
wanakimbia, ee Mwenyezi-Mungu, kujiweka tayari.
Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu,
ukatazame na kunisaidia!
5Uinuke, ee Mwenyezi-Mungu,
Mungu Mwenye Nguvu, Mungu wa Israeli.
Uamke, uwaadhibu hao watu wasiokujua;
usiwaache hao wanaopanga ubaya.
6Kila jioni maadui hao hurudi
wakibweka kama mbwa,
na kuzungukazunguka mjini.
7Tazama, ni matusi tu yatokayo mdomoni mwao,
maneno yao yanakata kama upanga mkali;
tena wanafikiri hakuna anayewasikia.
8Lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawacheka;
unawapuuza hao watu wote wasiokujua.
9Nitakungoja, ewe uliye nguvu yangu;
maana wewe, ee Mungu, u ngome yangu.
10Mungu wangu utanijia na fadhili zako,
utaniwezesha kuwaona maadui zangu wameshindwa.
11Usiwaue mara moja, watu wangu wasije wakasahau;
ila uwayumbishe kwa nguvu yako, uwaporomoshe chini.
Ee Bwana, wewe ndiwe ngao yetu!
12Wao hutenda dhambi kwa yote wasemayo,
kwa hiyo na wanaswe katika kiburi chao!
Kwa sababu ya laana na uongo wao,
13uwateketeze kwa hasira yako,
uwateketeze wasiwepo tena;
ili watu wote wajue kuwa wewe ee Mungu
watawala wazawa wa Yakobo
hata mpaka miisho ya dunia.
14Kila jioni maadui hao hurudi
wakibweka kama mbwa,
na kuzungukazunguka mjini.
15Hupitapita huko na huko wakitafuta mlo,
na wasipotoshelezwa hunguruma.
16Lakini mimi nitaimba sifa za nguvu yako;
nitashangilia asubuhi juu ya fadhili zako;
maana wewe umekuwa ngome yangu
na kimbilio langu wakati wa taabu.
17Ewe uliye nguvu yangu, nitakuimbia sifa;
ee Mungu, wewe u ngome yangu;
Mungu mwenye kunifadhili!


Zaburi59;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: