Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 27 March 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Zaburi 90...



Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Yeremia akasema, Mwenyezi-Mungu alinena nami akasema: “Hanameli, mwana wa baba yako mdogo Shalumu, atakujia na kusema: ‘Nunua shamba langu lililoko Anathothi, maana wewe ni ndugu yangu kabisa, na unayo haki ya kulikomboa.’” Kisha binamu yangu Hanameli alinijia katika ukumbi wa walinzi kama alivyonifahamisha Mwenyezi-Mungu, akaniambia, “Nunua shamba langu lililoko Anathothi katika nchi ya Benyamini maana wewe una haki ya kulikomboa. Linunue kwa faida yako.” Ndipo nilipotambua kwamba lilikuwa kweli neno la Mwenyezi-Mungu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Basi, nililinunua shamba hilo lililoko Anathothi, kutoka kwa binamu yangu Hanameli, nikamlipa bei yake shekeli kumi na saba za fedha. Nikaitia sahihi hati ya kumiliki, nikaipiga mhuri, nikawaita mashahidi na kuipima ile fedha katika mizani. Kisha, nilichukua ile hati ya kumiliki niliyoipiga mhuri, ambayo ilikuwa na masharti na kanuni, pamoja na nakala nyingine iliyokuwa wazi.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....
Yahweh  tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni

Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Mungu wetu ukaonekane katika maisha yetuBaba wa Mbinguni tukanene yaliyo yako
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


Nilimpa hiyo hati ya ununuzi Baruku mwana wa Neria mwana wa Maaseya, mbele ya binamu yangu Hanameli na mashahidi waliokuwa wametia sahihi hati ya ununuzi, na mbele ya Wayahudi wote waliokuwa wameketi katika ukumbi wa walinzi. Mbele ya watu wote hao, nilimpa Baruku maagizo yafuatayo:
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Jehovah ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake...
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao....
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako,
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele....
Amina..!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,
Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake...

Nawapenda.

KITABU CHA NNE
(Zaburi 90–106)
Mungu wa milele na binadamu kiumbe
(Sala ya Mose, mtu wa Mungu)
1Ee Bwana, tangu vizazi vyote,
wewe umekuwa usalama90:1 neno kwa neno: Makao; hati nyingine: Kimbilio. wetu.
2Kabla ya kuwapo milima,
kabla hujauumba ulimwengu;
wewe ndiwe Mungu, milele na milele.
3Wamwambia binadamu, “Rudi mavumbini!”
Naye binadamu hurudi mavumbini alimotoka!
4 Taz 2Pet 3:8 Kwako miaka elfu ni kama siku moja tu,
ni kama jana ambayo imekwisha pita;
kwako ni kama mkesha mmoja wa usiku!
5Wawafutilia mbali watu kama ndoto!
Binadamu ni kama nyasi zinazochipua asubuhi:
6Asubuhi huchipua na kuchanua,
jioni zimekwisha nyauka na kukauka.
7Hasira yako inatuangamiza;
tunatishwa na ghadhabu yako.
8Maovu yetu umeyaweka mbele yako;
dhambi zetu za siri ziko wazi mbele yako.
9Kwa hasira yako maisha yetu yatoweka,
yanaisha kama pumzi.
10Miaka ya kuishi ni sabini,
au tukiwa wenye afya, themanini;
lakini yote ni shida na taabu!
Siku zapita mbio, nasi twatoweka mara!
11Nani anayetambua uzito wa hasira yako?
Nani anayejali matokeo ya ghadhabu yako?
12Utufundishe ufupi wa maisha yetu
ili tuweze kuwa na hekima.
13Urudi, ee Mwenyezi-Mungu!
Utakasirika hata lini?
Utuonee huruma sisi watumishi wako.
14Utushibishe fadhili zako asubuhi,
tushangilie na kufurahi maisha yetu yote.
15Utujalie sasa miaka mingi ya furaha,
kama ulivyotupa miaka mingi ya shida na taabu.
16Utuoneshe matendo yako sisi watumishi wako;
uwaoneshe wazawa wetu uwezo wako mtukufu.
17Utufadhili ee Bwana, Mungu wetu;
uzitegemeze kazi zetu,
uzifanikishe shughuli zetu.



Zaburi90;1-17

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: