Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Tuesday, 25 June 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 4..


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!

Shauli akamwambia Samueli, “Nimetenda dhambi. Nimeasi amri ya Mwenyezi-Mungu na amri yako, kwa sababu niliwaogopa watu, nikawatii wao. Lakini sasa nakuomba, unisamehe dhambi yangu. Niruhusu nirudi pamoja nawe ili niweze kumwabudu Mwenyezi-Mungu.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote 
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Samueli akamjibu: “Kamwe, siwezi kurudi pamoja nawe. Wewe umeikataa amri ya Mwenyezi-Mungu, naye amekukataa kuwa mfalme juu ya Israeli.” Samueli alipogeuka ili aende zake, Shauli akashika pindo la vazi lake, nalo likapasuka.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomna ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe...

Yahweh tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyovimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Yahwe ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona,masikio ya kusikia sauti yako na kuitii..
Baba wa Mbinguni  tunaomba ukatupe neema ya kufuata
njia zako,tukasimamie Neno lako,amri na sheria zako
siku zote za maisha yetu...
Ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu,ukatufanye chombo chema
ee Mungu wetu nasi tukatumike kama inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi....

Ndipo Samueli alipomwambia Shauli, “Tangu leo Mwenyezi-Mungu ameurarua ufalme wa Israeli kutoka kwako na atampa mtu mwingine miongoni mwa jirani zako aliye bora kuliko wewe. Na Mungu ambaye ni utukufu wa Israeli hadanganyi, wala habadili wazo lake. Yeye si binadamu hata abadili mawazo.”
Tazama watoto wako wenye shida/tabu,wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Mungu wetu tunaomba ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu
kila mmoja na mahitaji yake
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipo kwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kuweza kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele...
Amina...!!


Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,Baba wa Mbinguni aendelee kuwatendea sawasawa na mapenzi yake...
Nawapenda.

Manufaa ya hekima
1Wanangu, sikilizeni mwongozo wa baba yenu,
tegeni sikio mpate kuwa na akili.
2Maana ninawapa maagizo mema,
msiyakatae mafundisho yangu.
3Mimi pia nilikuwa mtoto mwenye baba,
nilikuwa mpole, kipenzi cha mama yangu.
4Baba yangu alinifundisha hiki:
“Zingatia kwa moyo maneno yangu,
shika amri zangu nawe utaishi.
5Jipatie hekima, jipatie ufahamu;
usisahau wala kupuuza maneno yangu.
6Usimwache Hekima, naye atakutunza;
umpende, naye atakulinda.
7Jambo la msingi ni kujipatia hekima;
toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili.
8Mthamini sana4:8 Mthamini sana: Maana yake katika Kiebrania si dhahiri. Hekima, naye atakutukuza;
ukimshikilia atakupa heshima.
9Atakuvika kilemba kizuri kichwani pako,
atakupa taji maridadi.”
10Mwanangu, sikia na kuyapokea maneno yangu,
ili upate kuwa na miaka mingi ya kuishi.
11Nimekufundisha njia ya hekima,
nimekuongoza katika njia nyofu.
12Ukitembea hatua zako hazitazuiwa,
wala ukikimbia hutajikwaa.
13Zingatia mafundisho ya Hekima na usimwache aponyoke,
mshike kwa makini maana yeye ni uhai wako.
14Usijiingize katika njia ya waovu,
wala usifuate mwenendo wa watu wabaya.
15Iepe njia hiyo wala usiikaribie;
jiepushe nayo, uende zako.
16Waovu kamwe hawalali wasipotenda uovu;
hawapati usingizi wasipomkwaza mtu.
17Maana uovu ndicho chakula chao,
ukatili ndiyo divai yao.
18Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri,
ambayo hungaa zaidi na zaidi hata mchana kamili.
19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene,
hawajui kinachowafanya wajikwae.
20Mwanangu, sikiliza kwa makini maneno yangu,
itegee sikio misemo yangu.
21Usiyaache yatoweke machoni pako,
yahifadhi ndani ya moyo wako.
22Maana hayo ni uhai kwa mtu anayeyapata,
ni dawa kwa mwili wake wote.
23Linda moyo wako kwa uangalifu wote,
maana humo zatoka chemchemi za uhai.
24Tenga mbali nawe lugha potovu;
wala midomo yako isitamke maneno madanganyifu.
25Uyaelekeze macho yako mbele kwa ujasiri,
mtazamo wako uwe mbele moja kwa moja.
26 Taz Ebr 12:13 Fikiria njia utakayochukua,
na hatua zako zote zitakuwa kamili.
27Usigeukie kulia wala kushoto;
epusha mguu wako mbali na uovu.

Methali4;1-27

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: