Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Wednesday, 26 June 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 5...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Shauli akajibu, “Nimefanya dhambi. Hata hivyo, unistahi sasa mbele ya wazee wa watu wangu na Waisraeli. Niruhusu nirudi pamoja nawe ili nikamwabudu Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.” Basi, Samueli akarudi pamoja naye mpaka Gilgali na Shauli akamwabudu Mwenyezi-Mungu.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kisha Samueli akasema, “Nileteeni hapa Agagi mfalme wa Waamaleki.” Agagi akamwendea Samueli akiwa mwenye furaha kwani alifikiri, “Uchungu wa kifo umepita.” Samueli akasema, “Kwa kuwa upanga wako umewafanya akina mama wengi wasiwe na watoto, ndivyo na mama yako atakavyokuwa bila mtoto miongoni mwa akina mama.” Akamkatakata Agagi vipandevipande mbele ya Mwenyezi-Mungu huko Gilgali.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe

Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Kisha, Samueli akaenda Rama; na mfalme Shauli akarudi nyumbani kwake huko Gibea. Tangu siku hiyo, Samueli hakumwona tena Shauli, mpaka siku alipofariki. Hata hivyo Samueli alimlilia Shauli. Naye Mwenyezi-Mungu alisikitika kwamba alikuwa amemtawaza Shauli mfalme juu ya Israeli.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....

Nawapenda.

Onyo dhidi ya uasherati
1Mwanangu, sikia hekima yangu,
tega sikio usikilize elimu yangu.
2Ndipo utakapoweza kuhifadhi busara,
na midomo yako izingatie maarifa.
3Mdomo wa mwanamke mpotovu ni mtamu kama asali,
maneno yake ni laini kuliko mafuta;5:3-5 Kuhusu aya 3-5 Taz pia 2:16; 7:6-27; 22:14; Mhu 7:26
4lakini hatimaye ni mchungu kama pakanga,
ni mkali kama upanga wenye makali kuwili.
5Nyayo zake zaelekea chini mautini,
hatua zake zaenda kuzimu.
6Yeye haijali njia ya uhai,
njia zake ni za kutangatanga, wala hajui.
7Sasa enyi wanangu, nisikilizeni,
wala msisahau maneno ya kinywa changu.
8Iepushe njia yako mbali naye,
wala usiukaribie mlango wa nyumba yake.
9Usije ukawapa wengine heshima yako,
na wakatili miaka yako;
10wageni wasije wakajishibisha kwa mali yako,
na jasho lako likaishia nyumbani kwa mgeni.
11Mwishoni mwa maisha yako utaomboleza
wakati mwili wako utakapoangamizwa.
12Hapo utasema, “Jinsi gani nilivyochukia nidhamu,
na kudharau maonyo moyoni mwangu!
13Sikuisikiliza sauti ya waalimu wangu,
wala kuwategea sikio wakufunzi wangu.
14Sasa niko karibu kuangamia kabisa
mbali na jumuiya ya watu.”
15Mkeo ni kama kisima cha maji safi:
Kunywa maji ya kisima chako mwenyewe.
16Ya nini chemchemi zako zitawanywe mbali,
na vijito vya maji barabarani?
17Hiyo ni yako wewe mwenyewe,
wala usiwashirikishe watu wengine.
18Chemchemi yako na ibarikiwe,
umfurahie mke uliyemwoa ukiwa kijana.
19Ni mzuri kama ayala, apendeza kama paa.
Mahaba yake yakufurahishe kila wakati,
umezwe daima na pendo lake.
20Mwanangu, ya nini kutekwa na mwanamke mwasherati?
Ya nini kumkumbatia kifuani mwanamke mgeni?
21Kumbuka njia za mtu zi wazi mbele ya Mwenyezi-Mungu;
yeye anaona kila hatua anayochukua binadamu.
22Mtu mwovu hunaswa kwa uovu wake mwenyewe;
hukamatwa katika tanzi za dhambi yake mwenyewe.
23Yeye hufa kwa utovu wa nidhamu,
huangamia kwa sababu ya upuuzi wake mkuu.

Methali5;1-23

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: