Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Friday, 28 June 2019

Kikombe Cha Asubuhi ; Methali 7...

Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Tumshukuru Mungu wetu katika yote...

Asante  Mungu wetu kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu


Utukuzwe ee Mungu wetu,usifiwe Baba wa Mbinguni

Neema yako yatutosha  Mungu wetu..!

Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo,” akasema baadaye kwa njia ya Daudi maneno yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiwe wakaidi.”
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba utupe neema ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea,Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe na yule mwovu na kazi zake zote,Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa  Damu ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti,
Yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....

Kama Yoshua angekuwa amewapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine. Kwa hiyo, basi, bado kuna kupumzika kwa watu wa Mungu. Maana, kila aingiaye mahali pa pumziko la Mungu atapumzika kutoka katika kazi yake kama vile pia Mungu alivyopumzika kutoka kazi yake. Basi, tujitahidi kuingia katika pumziko hilo, ili asiwepo yeyote miongoni mwetu atakayekataa kutii kama walivyofanya wao.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa 
katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki ridhiki zetu
ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi tunaomba ukatupe neema ya kuweza
kuwabariki wenye kuhitaji
Yahweh tusipungukiwe katika mahitaji yetu
Mungu wetu ukatupe kama inavyokupendeza wewe



Jehovah tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Baba wa Mbinguni tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu

Mungu  wetu ukaonekane katika maisha yetu popote tupitapo na ikajulikane kwamba upo 

Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
Ukatufanye barua njema ee Mungu wetu nasi tukasomeke kama
inavyokupendeza wewe
Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...

Neno la Mungu ni hai na lina nguvu; ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Hukata kabisa mpaka mahali ambapo moyo na roho hukutana, mpaka pale vikutanapo viungo vya mwili na uboho. Neno hilo huchambua nia na fikira za mioyo ya watu. Hakuna kiumbe chochote kilichofichika mbele ya Mungu; kila kitu kimefunuliwa wazi mbele ya macho yake yeye ambaye kwake tutapaswa kutoa hoja ya matendo yetu.
Tazama wenye shida/tabu,Mungu wetu tunaomba
 ukawaguse kila mmoja na mahitaji yake
Baba wa Mbinguni tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda
kinyume nawe
Mungu wetu ukawape neema ya kujiombea,macho ya rohoni,masikio yakusikia sauti yako,wakafuate njia zako nazo zikawaweke huru
Mungu wetu tunaomba ukasikie kulia kwao
Baba wa Mbinguni tunomba ukawafute machozi yao
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao
Mungu wetu tunaomba ukawatendee sawasawa na mapenzi yako
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele
Amina....!!!


Wapendwa katika Kristo Yesu asanteni sana
kwakuwanami/kunisoma

Mungu Baba aendelee kuwabariki na kuwatendea
kama inavyompendeza yeye
Amani ya Bwana wetu Yesu Kristo na upendo wa Mungu Baba
ukae nanyi daima....
Nawapenda.

1Mwanangu, yashike maneno yangu,
zihifadhi kwako amri zangu.
2Zifuate amri zangu nawe utaishi;
yalinde mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.
3Yafunge vidoleni mwako;
yaandike moyoni mwako.
4Iambie Hekima: “Wewe ni dada yangu”,
na Busara “Wewe ni rafiki yangu”.
5Vitakulinda mbali na mwanamke mbaya,
vitakuepusha na maneno matamu ya mwanamke mgeni.

Mwanamke mwasherati
6Siku moja dirishani mwa nyumba yangu,
nilichungulia nje kupitia viunzi vya dirisha,
7nikawaona vijana wengi wajinga,
na mmoja hasa aliyekuwa mpumbavu.
8Huyo alikuwa akitembea kwenye barabara ile,
karibu na kona alikoishi mwanamke fulani.
Basi akashika njia iendayo nyumbani kwa mwanamke huyo.
9Ilikuwa yapata wakati wa jioni,
giza na usiku vilikuwa vimeanza kuingia.
10Punde kijana akakutana na huyo mwanamke;
amevalia kama malaya, ana mipango yake.
11Alikuwa mwanamke wa makelele na mkaidi;
miguu yake haitulii nyumbani:
12Mara barabarani, mara sokoni,
katika kila kona ya njia hakosekani akivizia.
13Alimkumbatia kijana huyo na kumbusu,
na kwa maneno matamu, akamwambia:
14“Ilinilazimu kutoa tambiko zangu;
leo hii nimekamilisha nadhiri yangu.
15Ndio maana nimetoka ili nikulaki,
nimekutafuta kwa hamu nikakupata.
16Nimetandika kitanda changu vizuri,
kwa shuka za rangi za kitani kutoka Misri.
17Nimekitia manukato, manemane, udi na mdalasini.
18Njoo tulale pamoja mpaka asubuhi;
njoo tujifurahishe kwa mahaba.
19Mume wangu hayumo nyumbani,
amekwenda safari ya mbali.
20Amechukua bunda la fedha;
hatarejea nyumbani karibuni.”
21Alimshawishi kwa maneno mengi ya kubembeleza;
kijana akashawishika kwa maneno yake matamu.
22Hapo akamfuata huyo mwanamke moja kwa moja,
kama ng'ombe aendaye machinjioni,
kama paa arukiaye mtegoni.
23Hakutambua kwamba hiyo itamgharimu maisha yake,
mpaka alipojikuta amekuwa kama amechomwa mshale moyoni,
amekuwa kama ndege aliyenaswa wavuni.
24Sasa wanangu, nisikilizeni;
yategeeni sikio maneno ya kinywa changu.
25Msikubali kuongozwa na mwanamke kama huyo,
wala msipitepite katika mapito yake.
26Maana amewaangusha wanaume wengi;
ni wengi mno hao aliowachinja.
27Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu,
ni mahali pa kuteremkia mautini.

Methali7;1-27

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: