Swahili na Waswahili

Swahili na Waswahili
Waswahili na Mswahili Rachel Siwa...Pamoja Daima!!

Thursday, 20 June 2019

Kikombe Cha Asubuhi ;Tunamshukuru Mungu tumemaliza kitabu cha Zaburi...Leo tunaanza Kitabu Cha Methali 1..


Shalom,Habari za Asubuhi,Hamjambo,Mmeamkaje?

Haleluyah Mungu wetu yu mwema sana,Tunamshukuru Mungu kwa kutupa nafasi ya
 kupitia kitabu cha "ZABURI" Ni matumaini yangu kuna mengi tumejifunza...

Leo tunapokwenda anza kupitia Kitabu cha "METHALI " tunamuomba
Mungu wetu akatupe macho ya rohoni na akili ya kuelewa katika kujifunza NENO lake..


Tumshukuru Mungu katika yote....

Mungu wetu Baba yetu,Muumba wetu Muumba wa Mbingu na Nchi
Muumba wa vyote vilivyomo vinavyoonekana na visivyoonekana
Mungu wa walio hai,Mungu  mwenye huruma,Mungu wa upendo
Mungu wa Abrahamu,Isaka na Yakobo...
Asante kwa wema na fadhili zako kwetu
Asante kwa ulinzi wako kwetu wakati wote
Asante kwa kutuchagua tena na kutupa
kibali cha kuendelea kuiona leo hii
Asante kwa pumzi/uzima,afya na kuwatayari kwa majukumu yetu

Neema yako yatutosha ee Mungu wetu....!!


Shauli aliwashinda Waamaleki kuanzia Havila hadi Shuri, mashariki ya Misri. Alimteka mfalme Agagi wa Waamaleki akiwa hai. Akawaua watu kwa makali ya upanga.
Baba wa Mbinguni tunakuja mbele zako tukijinyenyekeza,tukijishusha na kujiachilia mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba utusamehe dhambi zetu zote tulizo zifanya
Kwakuwaza,kwakunena,kwakutenda,kwakujua/kutojua
Baba wa Mbinguni nasi tunaomba ukatupe neema
ya kuweza kuwasamehe wale wote waliotukosea
Usitutie majaribuni Mungu wetu tunaomba utuepushe
na yule mwovu na kazi zake zote
Jehovah ututakase miili yetu na akili zetu
Baba wa Mbinguni tunaomba utufunike kwa Damu
ya Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo wa Nazareti
yeye aliteseka kwanza ili sisi tupate kupona....


Lakini Shauli na watu wake hawakumuua Agagi, wala kondoo bora kabisa, ng'ombe wazuri, ndama, wanakondoo na chochote kile kilichokuwa kizuri hawakukiangamiza. Lakini vitu vyote vibaya na visivyo na thamani waliviangamiza.
Mungu wetu tunaomba ukabariki kazi za mikono yetu
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe ubunifu na maarifa katika utendaji
Jehovah nasi tukatende sawasawa na mapenzi yako
Yahweh tunaomba ukabariki ridhiki zetu ziingiazo/zitokazo
Mungu wetu nasi ukatupe neema ya kuweza kuwabariki wenye kuhitaji
Tusipungukiwe katika mahitaji yetu Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe kama inavyokupendeza wewe....
Yahweh  tunayaweka maisha yetu mikononi mwako
Mungu wetu tunaomba ukabariki nyumba/ndoa zetu,
watoto,wazazi wetu,familia/ndugu na wote wanaotuzunguka
Jehovah tunaomba ulinzi wako kwetu na kwa vyote tunavyo vimiliki
Yahweh tunaomba ukatubariki tuingiapo/tutokapo
Mungu wetu tunaomba ukavibariki vyote tunavyoenda kugusa/kutumia
Baba wa Mbinguni ukavitakase kwa Damu ya Bwana wetu Yesu Kristo
Mungu wetu ukatamalaki na kutuatamia
Baba wa Mbinguni tukawe salama rohoni

Yahweh ukatupe akili ya kutambua mema na mabaya
Mfalme wa amani amani yako ikatawale katika maisha yetu
Mungu wetu ukatupe macho ya kuona na masikio ya kusikia 
sauti yako na kuitii
Baba wa Mbinguni tunaomba ukatupe neema ya kufuata njia zako
Yahweh tukasimamie Neno lako amri na sheria zako siku zote 
za maisha yetu
Neema zako zikawe nasi Nuru yako ikaangaze katika maisha yetu
ukatuguse kwa mkono wako wenye nguvu
Ukatufanye chombo chema ee Mungu wetu nasi tukatumike kama
inavyokupendeza wewe

Roho Mtakatifu akatuongoze katika yote na tukawe na kiasi...


“Ninajuta kwamba nimemfanya Shauli kuwa mfalme. Yeye ameacha kunifuata mimi na hajatimiza amri zangu.” Samueli alikasirika, akamlilia Mwenyezi-Mungu usiku kucha.
Mungu wetu tunawaweka mikononi mwako wenye shida/tabu,
wote wanaopitia magumu/majaribu mbalimbali
Jehovah ukawaguse kwa mkono wako wenye nguvu kila mmoja na mahitaji yake...
Mungu wetu tunaomba ukawasamehe pale walipokwenda kinyume nawe
Yahweh tunaomba ukawape neema ya kujiombea,kufuata njia zako nazo zikawaweke huru...
Nuru yako ikaangaze katika maisha yao....
Baba wa Mbinguni tunayaweka haya yote mikononi mwako,
Kwakuwa Ufalme ni wako Nguvu na Utukufu hata Milele....
Amina..!

Asanteni sana wapendwa katika Kristo Yesu kwakuwa nami,
Mungu Baba aendelee kuwatendea sawasawa na mapezni yake...
Nawapenda.

Umuhimu wa methali
1 Taz 1Fal 4:32 Hizi ni methali za Solomoni mfalme wa Israeli, mwana wa Daudi. 2Methali hizi zawapatia watu hekima na nidhamu; zawafanya waelewe maneno ya busara, 3zawafanya kuwa na nidhamu, utaratibu, uadilifu, haki na kutenda kwa usawa. 4Huwapatia wajinga werevu na vijana maarifa na hadhari. 5Mwenye hekima azisikie na kuongeza elimu yake, naye mwenye busara apate mwongozo. 6Mtu aelewe methali na mifano, maneno ya wenye hekima na vitendawili vyao.
7 Taz Yobu 28:28; Zab 111:10; Meth 9:10 Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa,
lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.

Mawaidha kwa vijana
8Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,
wala usiyapuuze mafundisho ya mama yako;
9hayo yatakupamba kilemba kichwani pako,
kama mkufu shingoni mwako.
10Mwanangu, usikubali kushawishiwa na wenye dhambi.
11Wakisema: “Twende tukamvizie mtu na kumuua;
njoo tukawashambulie wasio na hatia!
12Tutawameza kama Kuzimu wakiwa hai,
watakuwa kama wale washukao Shimoni.
13Tutajitwalia mali zote za thamani,
nyumba zetu tutazijaza nyara.
14Njoo ushirikiane nasi,
vyote tutakavyopata tutagawana.”
15Wewe mwanangu usiandamane nao,
uzuie mguu wako usifuatane nao.
16Maana wao wako mbioni kutenda maovu,
haraka zao zote ni za kumwaga damu.
17Mtego utegwao huku ndege anaona,
mtego huo wategwa bure.
18Wao huvizia na kujiangamiza wao wenyewe,
hutega mtego wa kujinasa wao wenyewe.
19Ndivyo zilivyo njia za waishio kwa ukatili;
ukatili huyaangamiza maisha ya wakatili.

Hekima inaita
20 Taz Meth 8:1-3 Hekima huita kwa sauti barabarani,
hupaza sauti yake sokoni;
21huita juu ya kuta,
hutangaza penye malango ya mji:1:21 malango ya mji: Hapa ndipo mahali walipokutana watu kutatua matatizo na kesi zao.
22“Enyi wajinga! Mpaka lini mtapenda kuwa wajinga?
Mpaka lini wenye dharau watafurahia dharau zao,
na wapumbavu kuchukia maarifa?
23Sikilizeni maonyo yangu;
nitawamiminia mawazo yangu,
nitawajulisha maneno yangu.
24Kwa kuwa nimewaita mkakataa kusikiliza,
nimewapungia mkono mje mkakataa,
25mkapuuza mashauri yangu yote,
wala hamkuyajali maonyo yangu,
26nami pia nitayachekelea maafa yenu,
nitawadhihaki mnapokumbwa na hofu,
27hofu itakapowakumba kama tufani,
maafa yenu yatakapowavamia kama kimbunga,
wakati udhia na dhiki vitakapowapata.
28Hapo ndipo mtakaponiita lakini sitaitika;
mtanitafuta kwa bidii lakini hamtanipata.
29Kwa kuwa mliyachukia maarifa,
wala hamkuchagua kumcha Mwenyezi-Mungu;
30maadamu mlikataa shauri langu,
mkayapuuza maonyo yangu yote;
31basi, mtakula matunda ya mienendo yenu,
mtavimbiwa kwa hila zenu wenyewe.
32Maana wajinga hujiua kwa ukaidi wao,
wapumbavu hujiangamiza kwa kujiamini kwao.
33Lakini kila anisikilizaye atakaa salama,
atatulia bila kuogopa mabaya.”


Methali1;1-33

Biblia Habari Njema kwa Watu Wote(BHN)

"Swahili Na Waswahili"Mbarikiwe.

No comments: